Tafsiri halisi ya neno Mswahili

Tafsiri halisi ya neno Mswahili

Walihojiwa na kilichongaza ni jinsi walivyo point out
kuwa sio watu wa kawaida tu hawajui historia vizuri bali mpaka Waandishi wa habari
mfano waandishi wengi wanauita uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid ,
wana changanya na Karume
so inakuwa 'Sheikh Amri Abeid Karume'
watu wawili tofauti wanachanganywa....
Achilia mbali vitabu vya magwiji wa Lugha ya Kiswahili kama hao kuwa available Kenya zaidi
kuliko Tanzania...

:help::help:
 
Walihojiwa na kilichongaza ni jinsi walivyo point out
kuwa sio watu wa kawaida tu hawajui historia vizuri bali mpaka Waandishi wa habari
mfano waandishi wengi wanauita uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid ,
wana changanya na Karume
so inakuwa 'Sheikh Amri Abeid Karume'
watu wawili tofauti wanachanganywa....
Achilia mbali vitabu vya magwiji wa Lugha ya Kiswahili kama hao kuwa available Kenya zaidi
kuliko Tanzania...

Hivi umeshagundua kuwa vituo vingi vya runinga vya Kenya hutumia Kiswahili sanifu zaidi kuliko vya kwetu?

Napenda sana wale watangazaji wa NTV mimi....
 
Hivi umeshagundua kuwa vituo vingi vya runinga vya Kenya hutumia Kiswahili sanifu zaidi kuliko vya kwetu?

Napenda sana wale watangazaji wa NTV mimi....


Mfano sisi infrastructure tunaita eti miundo mbinu
Wakenya wanaita miundo-msingi...
mimi naona wakenya wako sawa...sisi tunaharibu lugha
 
mswahili ni mtu wa ajabu ajabu asiyejitambua. wivu wa kijinga. mbeya. mnoko. wengi wanaishi uswahilin.
uzunguni hakuna mswahili kila mtu anaishi kivyake bila kufatiliana kama waswahili.

asante kwa ujumbe mzuri uliotupa. tutakuwa makin na waswahili.
Uzunguni wenyewe tabia zao za kupenda ushoga na juzi wamepitisha sheria ya ndoa za wanaume kwa wanaume na vyeti vya ndoa wanapewa vipi unaipenda hii tabia uzunguni?
 
uswahili ni tabia na waswahili ni wale wenye kuuvaa uswahili kwa tabia zao.

awe anaishi masaki au kwa mtogole kama wana tabia za kiswahili wote ni waswahili bila kujali rangi zao au makabila yao.

tabia za kiswahili wala si njema na hakuna anayependa tabia za kiswahili.

ni tabia zinazorudisha nyuma maendeleo yetu.

tabia ya umbea ya kiswahili kule kwa mtogole fulani ataupiga umbea kwenye kijiwe au na mashosti wake. kule uzunguni atapiga umbea kwenye facebook au kwenye mitandao.
 
Mswahili ni nani????
Hilo ni swali la kumi, "Maendeleo ya kiswahili" necta Olevel
1. Mswahili ni mtu anaeongea kiswahili
2. Mswahili ni mtu aliezaliwa pwani ya Afrika mashariki
3. Mswahili ni mtu mmbea
4.Mswahili ni mtu anaependa kuvaa vibarakashee
5.Mswahili ni mtu muongo asietunza ahadi

Total marks kumi ech point 2marks

Wewe jiangalie unafall wapi
 
jina la mtu
mtu anayezungumza kiswahili
 
swali;mswahili ni nani?

Mtu mwenye asili ya mwambao wa pwani ya Bahari ya hindi, alie na asili ya kutumia kiswahili kama lugha yake ya asili na asiekuwa na lugha nyingine ya asili.
Kimjinimjini, mswahili ni mtu asie na maadili, anaeamini sana imani za kishirikina hata pale ambapo logic inaonyesha kuwa jambo ni la kawaida, asieaminika, pamoja na kuwa mwenye tabia ambazo ni kinyume na ustaarabu wa kawaida.
 
Mtu mwenye asili ya mwambao wa pwani ya Bahari ya hindi, aliye na asili ya kutumia kiswahili kama lugha yake ya asili na asiyekuwa na lugha nyingine ya asili.
Kimjinimjini, mswahili ni mtu asiye na maadili, anayeamini sana imani za kishirikina hata pale ambapo logic inaonyesha kuwa jambo ni la kawaida, asiyeaminika, pamoja na kuwa mwenye tabia ambazo ni kinyume na ustaarabu wa kawaida.

Kwenye nyekundu ulijisahau kidogo, vinginevyo nakubaliana na maelezo yako kwa asilimia tisini na tisa ila hapo kwenye samawati ungeweka neno "mantiki" lingefaa zaidi. Asante.
 
Mswahili ni yeyote mwenye asili ya
pwani ya afrika mashariki,
huwasiliana kwa lugha ya kiswahili,
ni binadamu mwenye fikra sahihi, ni
mdadisi, hughani mang'amuzi kwa
lugha ya kiswahili!...........
 
Mswahili ni yeyote mwenye asili ya
pwani ya afrika mashariki,
huwasiliana kwa lugha ya kiswahili,
ni binadamu mwenye fikra sahihi, ni
mdadisi, hughani mang'amuzi kwa
lugha ya kiswahili!...........

shukrani mkuu
 
shukrani mkuu

1. Mkaazi wa Upwa wa Afrika Mashariki (Kutokea Sofala hadi Barawa, Somalia na visiwa vilivyo ndani yake)
2. Mtu yeyote anayezungumza lugha ya Kiswahili
3. Mkaazi wa maeneo duni yanayofahamika kama 'Uswahilini'
4. Mtu mwenye tabia za zinazoonekana za ajabu kwa watu walioamili ustaarabu wa kisasa. Unaweza kusikia "Anapenda sana umbea, ana mambo ya Kiswahili.
5. Anayeamini au kushiriki katika Ushirikina nae huitwa Mswahili.

Naamini nimejibu swali lako kwa kiasi fulani, karibu!
 
Back
Top Bottom