Nadharia ya ubeberu na ukoloni mamboleo leo ilitoka wapi? Niwape shule kidogo juu ya nadharia hii ya watu waliofilisika kifikra kwa kushindwa kwao wakajifichia kwenye kutupia lawama mabeberu.
Wapigania Uhuru wa afrika waliwadanganya kwa kuwaaminisha waafrika kwa wawasaidie kuwaondoa madarakani wakoloni ili watakapowaondoa madarakani watakula mema ya nchi. Kumbe ilikuwa ni janjajanja ya wapigania Uhuru wawaondoe wakoloni kisha wajimilikishe ukoloni ili kujifisadi matunda ya Uhuru. Tumeona baada ya kuwaondoa wakoloni weupe kwa mbwembwe ikiwemo kuwatambia ya kwamba warudi baada ya mda mfupi watakuta wameleta maendeleo makubwa afrika kuliko walioleta wakoloni weupe afrika. Kuna general wa Vita wa uingereza msome anaitwa Bernard Montgomery akawambia wenzake Hawa wanataka Uhuru wapeni lakini awatofika mbali Hawa watarudi tena kukuombeni misaada. Baada ya wapigania Uhuru kupata madaraka wakajigeuza kuwa wakoloni weusi kwa kuwageukia waafrika kwa kuwafanyia unyama na ukatili wa Hali ya juu waafrika kuliko hata ukatili waliofanyiwa na wakoloni weupe. Wakawauwa, wakachinja, wakaiba pesa za waafrika na kuzificha mabenk ya ulaya, wakajilimikishia mapande makubwa ya ardhi na Mali nyingi huku wakiwaacha waafrika wengi wakitopea kwenye ufukara kwa kuuwa uchumi wa nchi zao (Mugabe,) kumiliki karibu nusu ya ardhi ya raia wao ( moi, Kenyatta, odinga) kuiba pesa afrika na kuficha ulaya kujenga mahekalu ulaya ( mobutu, Mugabe, abacha, Jameih,) kuwauwa wapinzani wao ( abacha, Mugabe, mobutu, kamuzu, gwema, bokassa, nk?).
Baada ya kuuwa uchumi mzuri walioachiwa na wakoloni Hawa wakoloni weusi wakaja na falsafa za neno mabeberu na ukoloni mamboleo kwa kuwatumia waandishi Kama kina Walter Rodney na kufundisha mitaala yenye kupandikiza chuki kwa wakoloni mashuleni lengo kuu ni kufichia udhaifu wao wa kushindwa kwao kuwaletea waafrika maendeleo, maana wananchi waliwauliza maendeleo yapo wapi unafuu upo wapi mbona hakuna elimu Bora, afya Bora, ajira mlizotuahidi Kama zilivyokuwa tele na bora kabla ya Uhuru? Ili kukwepa lawama na aibu wakoloni weusi wakaamua kuwatupia lawama wengine kwa kuwaita mabeberu Mara sijui ukoloni mamboleo ( kutupia lawama wengine juu ya kushindwa kwako) lengo kukwepa macho ya wananchi baada ya kukosa walichikitegemea wakati wa kupigania uhuru. Ukiangalia tofauti ya maisha kabla na baada ya Uhuru unakuta waafrika wanaishi maisha duni Sana dhoofu Hali kuliko hata kabla ya Uhuru.
Swali la kujiuliza why tuliokuwa nao sawa kiuchumi wao wameendelea? Kama kutawaliwa Ni kikwazo? China ilitawaliwa na japani, india na Uingereza, Algeria, Tunisia, morocco na ufaransa, usa ilitawaliwa na Uingereza, america ya kusini na france, nk why wao wameendelea. Ukistudy unakuta kutoendelea kwa afrika kunatokana na internal factors zaidi kuliko external factors tofauti na tunavyoaminishwa na waliosoma zamani Kama kina Walter Rodney na kina Prof Lumumba.
Huwezi kuwa na maendeleo kwa kujitenga na kuwa kisiwa, Hakuna taifa lililoshirikiana na mabeberu likawa fukara ( brazil, uturuki, south korea, india, Dubai, Qatar, china, Malaysia, indonesia, nk)
Kwann wakoloni weusi wanawachukia mabeberu ni kwa sababu mabeberu ni kikwazo kwao juu ya kuminya Uhuru na demokrasia, maana watawala wa kiafrica ujiona salama zaidi kutawala masikini wanyonge ( future less people) thus upenda kuwasomesha namba watu ili wawe masikini waweze kuwatawala thus upenda kuwashughulikia wasomi na matajiri kwa maana ili kundi lina exposure kubwa Sana na huwezi kulipropaganda sawa na lile kundi la futereless people.
Hoja za mabeberu na ukoloni mamboleo ni hoja za watu waliosoma sylbus za zamani na waliofilisika kifikra awajui chochote kuhusu modern economic integration.