Tafsiri sahihi ya ubeberu

Tafsiri sahihi ya ubeberu

From now,onwards all chadema's gays/guys! I declare them as stupid gang.
Ha Ha Ha usipoteze muda wako na unaowaita stupid gang. Lakini kumbuka huna monopoly ya matusi na matusi ni dalili ya kushindwa hoja au kukosa ustarabu.
 
Hivi nyie vichwa mapambo kuichosha miguu, muambiwe kwa kikara ndio mtaelewa?

Inamaana hamjui au ni kusudi tuu? Hamkumbuku Rais Magufuli alikutana na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania na akaahidi uchaguzi huru na haki?
Tunayoyaona wanatendewa wapinzani ndio uchaguzi huru na haki?Mchakato wa kampeni umeonesha dalili kuwa kuna ukandamizwaji wa haki kwa upande wa upinzani!Kuongea ni jambo moja ila kutekeleza ni jambo jingine!
Msiwe vichwa maji misukule ya lumumba!
 
Hao mabeberu mbona hamuwataji majina tukawajua?
Hawa hapa ubeberu , ukoloni mamboleo ni hoja za watu waliofilisika kifikra
 

Attachments

  • FB_IMG_1602419043888.jpg
    FB_IMG_1602419043888.jpg
    10.2 KB · Views: 2
Kwa kifupi, Beberu hapa Tanzania....Ni mtu yoyote anayempinga Magufuli!
Kama Ni Mtanzania litaongezeka neno anatumikia na Mabeberu!
 
download.jpeg

Beberu hilo hapo. Cheki jamaa anavyolishangaa[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wanajamvi,

Kumekuwa na Upotoshaji mkubwa Kuhusu ubeberu na mabeberu wenyewe. Hili huenda linafanywa makusudi au kwa kutokujua.

Nilipokuwa shule ya msingi nilifundishwa kuwa ubeberu (imperialism) ni ubepari uliokomaa na kuvuka mipaka. Watu waliosoma kipindi changu wanakumbuka hili. Tafsiri hii ni tafsiri rahisi na nzuri.

Wanahistoria wanajua kuwa ukoloni haujaisha ila umebadili fomu kutoka kuwa ukoloni wa kiutawala, kijeshi na kiuchumi mpaka kuwa ukoloni mamboleo (neocolonialism). Njia kubwa ya kueneza ukoloni mamboleo ni kwa kupitia ubeberu.

Ubeberu upo zaidi kiuchumi, yaani baadhi ya matajiri (Filth billionaires) hasa kutoka nchi za magharibi na makampuni makubwa (multinational companies) ambao Wana nguvu ya kuweka viongozi madarakani hutawala uchumi wa dunia kupitia ubeberu hivyo hao ndio wanakuwa "mabeberu".

Ubeberu unatekelezwa zaidi Afrika kutokana na sababu nyingi ikiwemo ukweli kuwa Afrika ndio bara pekee lililobaki na rasilimali nyingi. rejee sababu za ukoloni: kutafuta masoko kwa bidhaa za viwanda vyao, malighafi kwa viwanda vyao, ardhi n.k, Mahitaji hayo yangali hai mpaka sasa. Lakini ubeberu pia unatekelezwa zaidi Afrika kutokana na ukweli pia baadhi ya viongozi wetu ni dhaifu dhhofu li hali huku wakiutukuza umagharibi na kuutweza uafrika wao.

Ili iwe rahisi kwa ubeberu kufanya kazi, kunapandikizwa viongozi vibaraka ambao hao wanakuwa ni "yes sir" mbele ya mabeberu. Akipatikana kiongozi imara ambaye hataki ujinga, huyu atapigwa vita na kusukiwa mipango ya kung'olewa kwani ni hatari kwa uchumi wa mabeberu. Kiongozi huyu ataitwa kila majina. Chukulia mfano ufuatao:

Uko bandari na unapiga dili zako na kila siku unakomba mshiko wa nguvu. Mara paap! anakuja meneja anakata na kuziba mirija you're ya rushwa na ize mane, utampenda? Lazima mtakaa kama kamati ya roho mbaya ili kuona jinsi ya kumshughulikia.

Sisi Kama nxhi tumeamua kulinda rasilimali zetu, hi maana yake ni kuwa tumetangaza vita ya kiuchumi. Kuishinda hii asiwadanganye mtu, Magufuli haiwezi peke yake. Ni lazima tuungane, tuwe wazalendo na kuweka maslahi ya Tanzania mbele.

Mabeberu wananguvu sana lakini wanatafuta chanzo kutoka ndani ya nchi. Tukiwa wamoja, hawawezi penya.

Nahitimisha kwa kusema sio kila utawala, nchi au kampuni za magharibi ni za kibeberu bali zile tuu zinazotenda ubeberu.

#ubeberuupotuwemacho

Amani Msumari
Tanga
Magu anapambana kweli kulinda rasilimali za tanzania ila tatizo lake ambalo halivumiliki hata kidogo ni udikteta kwa wenye hizo rasilimali anazojifanya kuzilinda huku anafanya mambo BILA kuwashirikisha wananchi na pia ukatili wake umevuka mipaka havumiliki tena na hajui kula na vipofu sasa amewagusa mikono wameshtuka na hatofanikisha njama zozote kila kitu kimebuma na kuwa wazi huwezi kupambana na mabeberu huku unaumiza wananchi wako na wanakuchukia lazima MABEBERU WAKUBINUE JUU CHINI halafu wananchi wako watafanya sherehe NI HERI BEBERU MWEUPE KULIKO BEBERU JEUSI 😂😂😂😂😂😂
 
Naona tafsiri hii inakuja wakati ambapo Bashiru anaenda kuongea na mabeberu!Lumumba mnachekesha sana!Wakati Lissu anaenda kuongea na mabalozi mlipayuka sana kuwa Mabeberu wanakutana na Lissu!Leo ni zamu ya Bashiru,mnakuja na tafsiri kibao.

Aisee! Sio kwa kujitoa ufahamu kwa kiwango hiki aisee!
Mkuki kwa binadamu....mchungu.

Wanatupa burudani, tuongeze siku za kuishi.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Nimekukubali hapo kamati ya roho mbaya. Hawa ndio masdui wa ndani ya nchi. Kimsingi wako na wabaendeleza mapambano yao ya vita dhidi ya serikali ya JPM' wako. Jambo jema serikali hii imeonesha kuanza kulipa uzito unaostahili suala la kupambana na maadui wa ndani aka kamati ya roho mbaya. Mbinu za hawa naadui wa ndani zinashirikisha na wale wa nje ya Tanzania. Wanao mkono katika kampeni za Lissu' kuanzia ratiba yake.

Ni wakati sasa kwa serikali bila ya kuchelewa kulisimamia kwa njia nyengine na mahususi kama vile kuanzishwa kitengo maalumu na kikawezesha vizuri tu kwa raslimali zote muhimu ili kupambana nao. Wako na wamedhamiria kwelikweli hawatanii.
 
Ubeberu unaotutesa ni huu wa akina Mayanga Constraction na Dotto james mtoto wa dada
Bila kumsahau Mtoto mwingine wa Dada Furaha ambaye anakatwa jina ili aandaliwe nafasi nyingine ya kuteuliwa
 
Magu anapambana kweli kulinda rasilimali za tanzania ila tatizo lake ambalo halivumiliki hata kidogo ni udikteta kwa wenye hizo rasilimali anazojifanya kuzilinda huku anafanya mambo BILA kuwashirikisha wananchi na pia ukatili wake umevuka mipaka havumiliki tena na hajui kula na vipofu sasa amewagusa mikono wameshtuka na hatofanikisha njama zozote kila kitu kimebuma na kuwa wazi huwezi kupambana na mabeberu huku unaumiza wananchi wako na wanakuchukia lazima MABEBERU WAKUBINUE JUU CHINI halafu wananchi wako watafanya sherehe NI HERI BEBERU MWEUPE KULIKO BEBERU JEUSI 😂😂😂😂😂😂

Hii ni lishaizungumzia umetumia silaha ya kujengea mtu hofu kumshambulia Mh Rais wa JMT na Amiri Jeshi Mkuu. Ila kwa JPM tumaneno hutu hatufui dafu. Mbinu hii mliitumia sana wakati wa Kikwete na mlifanikiwa na ilikuwa miradi yenye kuandikiwa andiko la kiutekelezaji ili kuondoa hofu ya rais asiye jiamini na mtegemea mngolitini.
 
Nadharia ya ubeberu na ukoloni mamboleo leo ilitoka wapi? Niwape shule kidogo juu ya nadharia hii ya watu waliofilisika kifikra kwa kushindwa kwao wakajifichia kwenye kutupia lawama mabeberu.
Wapigania Uhuru wa afrika waliwadanganya kwa kuwaaminisha waafrika kwa wawasaidie kuwaondoa madarakani wakoloni ili watakapowaondoa madarakani watakula mema ya nchi. Kumbe ilikuwa ni janjajanja ya wapigania Uhuru wawaondoe wakoloni kisha wajimilikishe ukoloni ili kujifisadi matunda ya Uhuru. Tumeona baada ya kuwaondoa wakoloni weupe kwa mbwembwe ikiwemo kuwatambia ya kwamba warudi baada ya mda mfupi watakuta wameleta maendeleo makubwa afrika kuliko walioleta wakoloni weupe afrika. Kuna general wa Vita wa uingereza msome anaitwa Bernard Montgomery akawambia wenzake Hawa wanataka Uhuru wapeni lakini awatofika mbali Hawa watarudi tena kukuombeni misaada. Baada ya wapigania Uhuru kupata madaraka wakajigeuza kuwa wakoloni weusi kwa kuwageukia waafrika kwa kuwafanyia unyama na ukatili wa Hali ya juu waafrika kuliko hata ukatili waliofanyiwa na wakoloni weupe. Wakawauwa, wakachinja, wakaiba pesa za waafrika na kuzificha mabenk ya ulaya, wakajilimikishia mapande makubwa ya ardhi na Mali nyingi huku wakiwaacha waafrika wengi wakitopea kwenye ufukara kwa kuuwa uchumi wa nchi zao (Mugabe,) kumiliki karibu nusu ya ardhi ya raia wao ( moi, Kenyatta, odinga) kuiba pesa afrika na kuficha ulaya kujenga mahekalu ulaya ( mobutu, Mugabe, abacha, Jameih,) kuwauwa wapinzani wao ( abacha, Mugabe, mobutu, kamuzu, gwema, bokassa, nk?).
Baada ya kuuwa uchumi mzuri walioachiwa na wakoloni Hawa wakoloni weusi wakaja na falsafa za neno mabeberu na ukoloni mamboleo kwa kuwatumia waandishi Kama kina Walter Rodney na kufundisha mitaala yenye kupandikiza chuki kwa wakoloni mashuleni lengo kuu ni kufichia udhaifu wao wa kushindwa kwao kuwaletea waafrika maendeleo, maana wananchi waliwauliza maendeleo yapo wapi unafuu upo wapi mbona hakuna elimu Bora, afya Bora, ajira mlizotuahidi Kama zilivyokuwa tele na bora kabla ya Uhuru? Ili kukwepa lawama na aibu wakoloni weusi wakaamua kuwatupia lawama wengine kwa kuwaita mabeberu Mara sijui ukoloni mamboleo ( kutupia lawama wengine juu ya kushindwa kwako) lengo kukwepa macho ya wananchi baada ya kukosa walichikitegemea wakati wa kupigania uhuru. Ukiangalia tofauti ya maisha kabla na baada ya Uhuru unakuta waafrika wanaishi maisha duni Sana dhoofu Hali kuliko hata kabla ya Uhuru.
Swali la kujiuliza why tuliokuwa nao sawa kiuchumi wao wameendelea? Kama kutawaliwa Ni kikwazo? China ilitawaliwa na japani, india na Uingereza, Algeria, Tunisia, morocco na ufaransa, usa ilitawaliwa na Uingereza, america ya kusini na france, nk why wao wameendelea. Ukistudy unakuta kutoendelea kwa afrika kunatokana na internal factors zaidi kuliko external factors tofauti na tunavyoaminishwa na waliosoma zamani Kama kina Walter Rodney na kina Prof Lumumba.
Huwezi kuwa na maendeleo kwa kujitenga na kuwa kisiwa, Hakuna taifa lililoshirikiana na mabeberu likawa fukara ( brazil, uturuki, south korea, india, Dubai, Qatar, china, Malaysia, indonesia, nk)
Kwann wakoloni weusi wanawachukia mabeberu ni kwa sababu mabeberu ni kikwazo kwao juu ya kuminya Uhuru na demokrasia, maana watawala wa kiafrica ujiona salama zaidi kutawala masikini wanyonge ( future less people) thus upenda kuwasomesha namba watu ili wawe masikini waweze kuwatawala thus upenda kuwashughulikia wasomi na matajiri kwa maana ili kundi lina exposure kubwa Sana na huwezi kulipropaganda sawa na lile kundi la futereless people.
Hoja za mabeberu na ukoloni mamboleo ni hoja za watu waliosoma sylbus za zamani na waliofilisika kifikra awajui chochote kuhusu modern economic integration.
 
Beberu hana nafasi mbele ya GPM. Tuungane tumsaidie kwani ni kazi ngumu kupambana na beberu.
 
Back
Top Bottom