Tafsiri ya picha katika ulimwengu wa kiroho

Tafsiri ya picha katika ulimwengu wa kiroho

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Picha zinaongea, picha zinaishi picha zinatoa ujumbe maalum usioonekana kwa macho ya kawaida mpaka wakati ufike

Ukipata muda chukua album yako ya picha pitia picha za zamani ulizopiga na marafiki ndugu jamaa na hata watu usiowafahamu

- angalia mpangilio wa jinsi watu walivyosimama au kukaa nk
- angalia mpangilio wa rangi au mavazi
- angalia body language

Kwa mshangao wa ajabu utakuta kwenye picha fulani watu fulani waliosimama pamoja siku huyo au kuchuchumaa au kuvaa nguo za aina moja nk

- wote wamekufa
- wote ni matajiri
- wote wameoa/wameolewa nyumba moja
- wote tabia zao zinafanya nk

Kwa mshangao mkubwa angalia body language utajikuta unaona kabisa hao

- walikuja kuoana
- walikuja kuwa maadui wakubwa
- walikuja kuwa marafiki wa damu nk

Tunapojipanga tupige piga na kubadili badili mikao na nafasi si kwa akili zetu bali kuna nguvu nje ya ufahamu wetu nguvu ya kiroho ndio inafanya kazi

Ni nguvu hiyo inayoamua:

Usimame wapi na kwa nini
Ukae wapi na kwa nini
Ufuatane na nani na kwa nini
Umtazame nani na kwa nini

Ni nguvu ya uvutano kwenye ulimwengu wa roho inayotengeneza matukio yote haya na huja kudhihirika baada ya kipindi fulani kupita...haya yanatokea si kwa utashi wetu wala uamuzi wetu wala nguvu zetu

Sijapata picha nyingine lakini naomba kuweka hii

- angalia mfanano wa rangi za mavazi
- body language
- nafasi kwenye kusimama
- umbali na ukaribu

Unafikiri walipanga kwa makusudi huu mkao?

1472526319303.jpg
 
mh,sijaelewa bado katika hiyo picha mshana jr inamaana lipu na dr inawezekana kuwa kuna kitu nyuma ya pazia kimewalazimu kufanya waliyoyafanya?
Hata wenyewe hawakuwa wanajua nini kitakuja kutokea baadae (hata kama labda kulikuwa kuna kitu wanafanya kwa siri) lakini yale ya kiroho yale ya sirini yalikuja kutokea na kutimia.
 
Picha ni sehemu ya mwili wako iliyo nje yake wachawi na waganga huroga katika baadhi ya matukio kwa kutumia picha na kinacholeta uhai uhalisia na mawasiliano ya kiroho ni sura.
 
Back
Top Bottom