Habari mkuu
mshana jr shukrani sana kwa mada yako. Siku ya kwanza nilipoona uzi wako huu, sikuamini kwa asilimia 100% kile ulichokuwa umeandika. Lakini ilipofika mwezi wa tisa, nilirudi nyumbani, na baada ya kuchukua albamu, niliangalia picha za utotoni(ndizo pekee nilizonazo). Nilipoangalia picha ya mahafali ya darasa la saba, mimi peke yangu katika picha, ndiye niliyekuwa nimevaa shati tofauti na wengine. Niliporudisha kumbukumbu, nikakumuka, tulikuwa tumepanga kununua kitenge flani, siku ya kununua kitenge hicho, wenzangu walikwenda bila kunishirikisha. Walirudi na kunionyesha kitenge walichonunua, na nilipojitahidi kutafuta, nilitafuta hadi nikachoka na wakanishauri nitafute angalau kinachokaribiana rangi. Kifupi, nina mfumo tofauti na hao wote wa uingizaji wa hela. Wao wote wameaajiriwa serikalini, kasoro mimi.