Tafsiri ya picha katika ulimwengu wa kiroho

Tafsiri ya picha katika ulimwengu wa kiroho

IMG_20210303_205415_951.jpg
 
Kaka ile safari yangu ya ziara ya mashariki ya kati ilishindikana kwa sababu anuwai..ila bado mipango ipo

Ipo siku utatoboa na yote mipango ya Mungu
Ipo siku tunaweza kuwa safarini pamoja au tukakutana [emoji106]
 
Tusubiri vumbi litulie...sasa hivi si vema kusema kitu kuna TAHARUKI
Sawa kaka acha tuvute subira....hakika muda ni mwalimu,mimi na wewe tunaweza kaa kimya ila muda ukifika utaongea wenyewe...............subiri niipitie tena ile thread ya karma niongeze maarifa kwa muda huu
 
Picha zinaongea, picha zinaishi picha zinatoa ujumbe maalum usioonekana kwa macho ya kawaida mpaka wakati ufike

Ukipata muda chukua album yako ya picha pitia picha za zamani ulizopiga na marafiki ndugu jamaa na hata watu usiowafahamu

  • angalia mpangilio wa jinsi watu walivyosimama au kukaa nk
  • angalia mpangilio wa rangi au mavazi
  • angalia body language

Kwa mshangao wa ajabu utakuta kwenye picha fulani watu fulani waliosimama pamoja siku huyo au kuchuchumaa au kuvaa nguo za aina moja nk

  • wote wamekufa
  • wote ni matajiri
  • wote wameoa/wameolewa nyumba moja
  • wote tabia zao zinafanya nk

Kwa mshangao mkubwa angalia body language utajikuta unaona kabisa hao

  • walikuja kuoana
  • walikuja kuwa maadui wakubwa
  • walikuja kuwa marafiki wa damu nk

Tunapojipanga tupige piga na kubadili badili mikao na nafasi si kwa akili zetu bali kuna nguvu nje ya ufahamu wetu nguvu ya kiroho ndio inafanya kazi

Ni nguvu hiyo inayoamua:

Usimame wapi na kwa nini
Ukae wapi na kwa nini
Ufuatane na nani na kwa nini
Umtazame nani na kwa nini

Ni nguvu ya uvutano kwenye ulimwengu wa roho inayotengeneza matukio yote haya na huja kudhihirika baada ya kipindi fulani kupita...haya yanatokea si kwa utashi wetu wala uamuzi wetu wala nguvu zetu

Sijapata picha nyingine lakini naomba kuweka hii

  • angalia mfanano wa rangi za mavazi
  • body language
  • nafasi kwenye kusimama
  • umbali na ukaribu

Unafikiri walipanga kwa makusudi huu mkao?

Yap wamependeza
 
Back
Top Bottom