Ndio hivyo huku usipokuwa makini utaumizwa sana.
Juzi juzi hapo kuna mtu tumezoeana kawaida ananisalimiaga PM. Hiyo siku akaja akaniomba kama nina info za mdada mmoja humu. Nikamuuliza ni nini akanipa mkasa mzima. Sasa na yeye anachotaka ni adate naye halafu ampige picha za nyuchi kisha atafute namna ya kumdhalilisha. Mimi nikamwambia sina na ni kweli sina maana mimi huwa sihangaiki kumjua mtu yeyote humu. Na hata ningemjua mimi huwa sinaga bifu ya kudumu na mtu hadi nimfanyie hivo. Mimi tukipishana tukichambana yanaisha kesho yake nipo fresh labda yeye aamue kuyabeba.
Sasa huyu mtu ana ID mbili na ninajua atasoma hapa. Akatumia ID yake nyingine ambayo nayo ipo active ndio akatumia kumtafuta huyu dada. Mimi nawaona tu Kwenye Post wanachat mavibe kama yote hadi natamani nimtonye kwamba anachat na adui. Na anaandaliwa mtego tu. Ila nitamwambia tu .
Hii ilishanitokea mimi pia. Kuna mwanaume nilimdabua humu kisawasawa[emoji23][emoji23]. Kumbe kayabeba bhana. Sasa si akatumia ID yake nyingine kunifuata? Ananisalimia PM na ananiambia ni namna gani anavutiwa na michango yangu kumbe anani seti.
Sasa siku tukachat chat kwenye majukwaa kuna mtu akaja kuniambia hivi unajua fulani ndio yule yule uliyemtukana juzi juzi[emoji23][emoji23]. Nikasema kuuuumbe sasa na mimi nikawa nimejua naenda naye namna anavyotaka tuende. Hadi akaja akajua kwamba nimemshtukia.