Bush Dokta
JF-Expert Member
- Apr 11, 2023
- 24,831
- 45,154
Leo mtashuhudia miujiza jinsi risasi zitagoma kutoka kwenye Magazine.Jana niliweka uzi hapa nikionya watawala kuwa unyanyasaji ukizidi, unafanya watu wafike point of no return na wanakuwa tayari kwa lolote: kuuwawa, kuumiziwa, kufungwa jela, n.k.
Nilisema kadri watu wanavyouwawa, kuteswa, kupotezwa, n.k, wanaobaki wanajengea ujasiri na wanafikia hatua wanaona na wao hawana tena cha kupoteza na hiki ndio sasa kinakwenda kutumia. Tunakwenda kubaya.
Leo kupitia mtandao wa X, viongozi wakuu wa CHADEMA (Mbowe na Lissu) wameonyesha kuwa wako tayari kwa lolote hata kama ni kwa kupoteza uhai wao wataandamana(wamethibitisha maneno yangu)
Nilitamani sana maneno niliyoyasema mimi yangesemwa na watu wenye kuheshimika na wenye ushawishi katika jamiii, labda ujumbe ungewafikia watu wengi zaidi na ungepewa uzito.
Ni bahati mbaya watu wenye ushawishi wamechagua kukaa kimya, ila nawaambia mtawasikia wakitoa kauli baada ya mambo kuharibu.
Tunamshukuru Mzee Butiku kwa kusema aliyoyasema walau yeye katimiza wajibu wake.
Katibu Mkuu wa CCM, Dr. Nchimbi hakuwa serious katika hotuba yake ya hivi karibuni, hivyo sioni kama alikuwa na msaada wowote kwa chama chake na Taifa kwa ujumla.
Uzi husika ni huu:
Unyanyasaji wa wapinzani wakati wa Magufuli na huu wa Rais Samia kunawafanya wapinzani kufikia "The point of no return"
Muendelezo wa unyanyasaji wa viongozi wa upinzani hasa kuanzia zama za Magufuli na sasa wakati huu wa Rais Samia, una impact moja: kuwafanya wapinzani kuwa jasiri huku msingi mkuu wa huo ujasiri ni kuona au kuamini kuwa kwa sasa hawana tena cha kupoteza kwani kama ni kuteswa, wameshateswa...www.jamiiforums.com
Niliyoyasema ndio haya yameanza kutimia:
Mungu wetu sio Mungu Dhaifu