Kumbe serikali ya DRC ikitumia njia ya vita haiwezi kuvimaliza vita vya mashariki dhidi ya M23 bali mazungumzo, kwa sababu M23 hawapo tayari kuondoka Mashariki ya DRC kwa sababu wanaichukulia ni ardhi yao ya asili.
Maoni yangu:
1. Banyamulenge (Wanyarwanda wa DRC) wapewe uhuru Mashariki ya DRC wawe na nchi yao kwa sababu inaonekana Wakongoman hawapo tayari kuchangamana na Banyamulenge labda wanamuogopa Kagame.
2. Serikali ya DRC itende haki kwa Banyamulenge huko Mashariki ya DRC.
Habari kamili:
Wanyamulenge walijipata upande wa Congo wakati wakoloni walipokata mipaka mipya ya mataifa ya Afrika katika miaka ya 1900. Baadhi ya wenyeji wa ufalme wa zamani wa Rwanda kutoka kabila la Abanyamulenge ndio wanaounda kundi la M23.
Akielezea chanzo cha tatizo la Wanyamulenge katika mkutano ulioandaliwa New York na taasisi ya amani, International Peace Academy mwaka 1996, aliyekuwa Rais wa Tanzania Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliilaumu serikali ya Zaïre kwa kusababisha mzozo wa ya kikabila kwa kushindwa kusitisha unyanyasaji.
''Wanyamulenga sio wahamiaji waliokuja Zaïre. Ufalme wa Rwanda uliganywa kati ya Ubelgiji na Ujerumani. Na Ubelgiji ulichukua theluthi mbili ya ufalme wa Rwanda…Tunaposema heshimu mpaka uliowekwa na Ujerumani na Ubelgiji, pia tunapaswa kuwaheshimu watu uliowapokea chini ya mgawanyo'', alisema Nyerere na kuongeza kuwa: Huwezi kugeuka na kusema si raia wa nchi hii. Je utawarejesha peke yao au utawarudisha na kipande chao cha ardhi?...huwezi kusema nenda nyumbani!, nyumbani wapi?''.
Katika kujenga hoja yake, Nyerere alitoa mfano wa kabila la Wamasai wa Tanzania na Wamasai wa Kenya na kusema hawawezi kuambiwa warudi Kenya ama Tanzania kwa kuwa nchi yao ya asili iligawanywa katika makoloni mawili ya Waingereza na Wajerumani na baada ya uhuru wamejikuta wapo katika nchi mbili tofauti.
Vita vya mara kwa mara
M23 inasema kuwa inapigania maslahi ya Wakongomani wanaozungumza Kinyarwanda, ambao wamekuwa wakinyanyaswa na hata kuuawa na serikali ya Kinshasa.
Waasi wa M23 pia wanailamu serikali ya DRC pia kuyaunga mkono makundi ya waasi yanayoendesha harakati zao nchini Kongo, wakiwemo wapiganaji wa jamii ya Kihutu kutoka Rwanda waliotorokea DRC mwaka 1994 baada mauaji ya kimbari, kuwaangamiza ili kuwalazimisha kurudi Rwanda, shutuhuma ambazo serikali ya DRC inazikanusha.
Madai hayo mawili pia yanaungwa mkono na Rwanda, na ndiyo chimbuko la nchi hiyo kuhusishwa na kulaumiwa kwa kuwaunga mkono na kuwafadhili waasi wa M23 na harakati zao nchini DRC.
Suala la ubaguzi dhidi ya Wakongomani wanaozungumza Kinyarwanda (Wanyamulenge) lipo tangu enzi ya utawala wa Mobutu Sese Seko, DRC ikiitwa Zaïre. Wanyamulenge wanaozungumza Kinyarwanda wanaopatikana zaidi katika maeneo ya Kivu wamekuwa wakisema wamenyanyaswa tangu miaka ya 1960 na wamekuwa wakiambiwa "warudi nyumbani" Rwanda.
Uhusiano wa karibu wa Rwanda na M23 unathibitika pia kwa ukaribu wa baadhi ya wakuu kundi hilo na utawala wa Kigali. Kamanda mkuuwa kijeshi wa M23 Sultani Makenga, alipigana chini ya Paul Kagame wakati huo akiongoza waasi kutwaa madaraka Kigali dhidi ya iliyokuwa serikali ya Rwanda na kukomesha mauaji ya Kimbari mwaka 1994. Na baada ya hapo, Makenga pamoja na Banyamulenge wengine waliomuunga mkono Kagame walijiunga na makundi mengine ya wanamgambo na kushirikiana na jeshi la Rwanda kumpindua Mobutu Sese Seko na hatimaye kumuwezesha Laurent-Désiré Kabila kuingia madarakani.
Usuluhishi
Juhudi za upatanishi wa kikanda juu ya utatuzi wa mzozo wa DRC, M23 na Rwanda kupitia mazungumzo ya Nairobi na ya Luanda yaliyoongozwa na Rais wa Angola João Lourenço na Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta na kutumwa kwa vikosi vya Afrika Mashariki, na vile vya SADC zimeshindwa kupata suluhu ya amani kufikia sasa katika eneo hilo la mashariki mwa DRC.
Kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kinachofahamika kama MONUSCO ambacho kimekuwa DRC kwa miaka takriban 30 pia kimeshindwa kumaliza mzozo wa Mashariki mwa DRC.
Pande zote pia zimekuwa zikilaumiana kwa kukiuka makubaliano ya amani, ambayo yangeweza kuleta suluhu la mzozo huo.
Mchambuzi wa masuala ya kidiplomasia Dkt. Nicodemus Minde anasema suluhu la mzozo wa DRC litapatikana kwa njia ya kisiasa na kidiplomasia na sio kwa hatua za kijeshi ambazo zimekuwa zikishuhudiwa.
Jambo la kwanza ''Kunapaswa kuwa na muktadha wa kufahamu ni nini kinachoendelea, Rwanda, DRC – Kwa wasuluhishaji ni muhimu kuangalia chimbuko kihistoria zaidi na kufahamu chimbuko la mzozo. Tukifahamu historia ya vita na malumbano itakuwa ni njia nzuri'', anasema Dkt. Minde.
Kulingana naye suluhu ya sasa ni kuwakutanisha mahasimu na kuwaleta katika meza ya mazungumzo. Hata hivyo anasema mzozo huu hauna suluhisho moja tu.
''Mzozo huu unahitaji suluhisho la usitishaji mapigano, suluhisho la muda mfupi la utekelezaji wa michakato ya amani inayoendelea kwa mfano mchakato wa Luanda uliokwama kutokana na Rwanda kutokubaliana nao, na mchakato wa Nairobi uliosusiwa na Rais wa DRC Felix Tschidekedi''.
Aidha anasema suluhu nyingine inayoweza kudumu ni ''Kuiunganisha michakato hii miwili ambayo itawaleta wahusika wa mzozo huu kutoka EAC na SADC kwa kuwa ndio wanaoelewa zaidi hali halisi ya mzozo wa DRC na chimbuko lake.''
Viongozi wa SADC na EAC wanatarajiwa kukutana jijini Dar Es Salaam Ijumaa na Jumamosi ya wiki hii kujadiliana kuhusu mgogoro huo.
Funzo lililopatikana miaka 12 iliyopita ni kuwa vita peke yake haviwezi kumaliza mgogoro huu.
Chanzo: BBC Swahili