Tahadhari! Bahari Ina Roho Na Inaweza Kukuua

Tahadhari! Bahari Ina Roho Na Inaweza Kukuua

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
1,213
Reaction score
2,938
Bahari inakuona, inakusikia na inaweza kufanya maamuzi ya ajabu juu yako mpaka watu wakashangaa 😳 unapoiangalia Bahari unaona ni maji tu ila bahari ina uhai, yaani Bahari inajua nini kinaendelea, nini cha kufanya, inajua kila kitu.

Mtawala Xerxes 1 wa Persia aliamua kuiadhibu Bahari baada ya kuona imeharibu daraja alilokuwa amelijenga, akawaita wanajeshi wake wakaanza kuichapa baada ya hapo akalijenga tena daraja na Bahari haikulibomoa tena. Hii inaonesha ni kwa namna gani Bahari ina uhai.

Niliona hata kwenye video moja kuna mwanamke alikuwa akiingia kwenye Bahari anapigwa na mawimbi, ni kama Bahari inachafuka. Ilitaka kumuua ila cha ajabu watu walipokuwa wakimchukua na kumpeleka nje, Bahari inatulia, hakuna mawimbi. Akienda kuingia tu, mawimbi yanaanza kupiga tena, ni kwamba Bahari ilikuwa inamkataa. Watu wenye asili ya moto ndiyo wengi wanaoongoza kufa baharini, kama asili yako ni moto usipende sana kuogelea baharini utakufa.
 
Sasa thread kama hizi kuna vitu mi huwa naona mnakosea elezea toa facts zako ili watu waelewe, huwezi kusema MAJI, HEWA, MOTO, ARDHI alafu huyo mtu atafute mnajimu aliyekaribu naye. Wewe mwaga madude hapa kama kukupinga tukupinge vinginevyo utakuwa unafosi ulichokiandika tukubaliane nacho tu.

Kwasababu swala la bahari kuwa na uhai halina uthibitisho isipukuwa ina support viumbe walio hai ungetuelezea sasa.

Pia kutokana na astrology/zodiac kuna signs hugawanywa katika elements nne: ndiyo hizo moto, maji, hewa na ardhi sasa ndiyo useme kivipi au na wewe umeyasoma sehemu tu umekuja kuyamwaga humu.

🤷
 
Back
Top Bottom