TAHADHARI: Hali ya Usalama Mashariki ya Kati na Mwongozo kwa Watanzania

Fascinating

Senior Member
Joined
May 14, 2025
Posts
146
Reaction score
351
Wakuu,

Nimeona ni vyema tushirikishane taarifa muhimu iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (ya tarehe 02 Februari 2026) kuhusu usalama wa ndugu zetu waliopo au wanaopanga kusafiri kuelekea nchi za Mashariki ya Kati.

Kutokana na hali ya usalama inayoendelea katika ukanda huo, Serikali imetoa ushauri maalum kwa Watanzania waliopo nchi kama Bahrain, Israel, Kuwait, Qatar, Falme za Kiarabu (UAE), na Oman.

Mambo Muhimu ya Kuzingatia:

Ili kuhakikisha usalama wako au wa ndugu yako aliyeko huko, Wizara inasisitiza yafuatayo:

  • Epuka Safari: Inashauriwa kuepuka safari za kwenda au kutoka Mashariki ya Kati kwa sasa.
  • Baki Nyumbani: Ikiwezekana, baki katika makazi unayoishi na epuka maeneo yenye shughuli za kijeshi au operesheni za usalama.
  • Fuata Mamlaka: Zingatia maelekezo yote yanayotolewa na mamlaka za maeneo husika na uwe mwangalifu wakati wote.
  • Tunza Nyaraka: Hakikisha pasipoti yako na vitambulisho vya Tanzania viko sehemu salama lakini vinapatikana kwa haraka ikitokea dharura.
  • Mawasiliano: Tumia njia rasmi pekee kupata taarifa na epuka uvumi.

Usajili wa Diaspora (Muhimu Sana!)

Serikali inawaomba Watanzania wote waliopo Mashariki ya Kati kujisajili mara moja kupitia tovuti rasmi ili kurahisisha ufuatiliaji wa karibu na kutoa msaada pale unapohitajika.

Jisajili hapa:

Kumbuka: Usaidizi wa kibalozi wa ana kwa ana unaweza kuwa na mipaka kulingana na hali ya usalama ya eneo husika. Hivyo, kuchukua tahadhari binafsi ni jambo la msingi.

Kwa dharura yoyote, wasiliana na Ubalozi wa Tanzania ulio karibu nawe au tumia barua pepe ya Wizara: [email protected].

Tupashane habari na tuendelee kuwaombea ndugu zetu usalama.

2026-03-03 10.24.08.jpg
 
TAARIFA KWA UMMA
USHAURI WA HALI YA USALAMA NA USAFIRI KWA RAIA WA TANZANIA WANAOISHI AU KUSAFIRI MASHARIKI YA KΑΤΙ
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inafuatilia kwa karibu hali ya usalama inayoendelea katika eneo la Mashariki ya Kati. Kutokana na mazingira ya kiusalama yanayoendelea, Serikali inatoa ushauri kwa raia wa Tanzania wanaoishi au wanaopanga kusafiri kwenda katika eneo hilo, ikiwemo Bahrain, Israel, Kuwait, Qatar, Falme za Kiarabu (UAE) na Oman.

Serikali inapenda kuwajulisha wananchi kuwa, kwa nyakati kama hizi, usaidizi wa kibalozi ana kwa ana unaweza kuwa na mipaka kulingana na eneo alipo mhusika na hali halisi ya kiusalama. Hivyo, raia wote
wanahimizwa kuchukua tahadhari stahiki na kufuata maelekezo ya mamlaka husika.

Watanzania waliopo katika eneo la Mashariki ya Kati wanashauriwa kuzingatia maelekezo yafuatayo:
  • Kuepuka kufanya safari za kwenda au kutoka Mashariki ya Kati katika kipindi hiki.
  • Kubaki katika makazi mnayoishi inapowezekana.
  • Kufuata maagizo yanayotolewa na mamlaka za maeneo husika na kuwa waangalifu wakati wote.
  • Kuepuka maeneo yenye shughuli za usalama/kijeshi katika maeneo mnayoishi.
  • Kutumia njia rasmi za mawasiliano na taarifa.
  • Kuhifadhi pasipoti na vitambulisho vya Tanzania sehemu salama na inayopatikana haraka endapo kutatokea dharura.

Serikali inawasihi Watanzania walioko Mashariki ya Kati kujisitiri kwa uangalifu na kuendelea kufuatilia mawasiliano rasmi ya Ubalozi na ya dharura. Aidha, Watanzania wanaombwa kujisitiri kwa usajili kupitia kiunganishi kifuatacho kwa ajili ya ufuatiliaji wa karibu:

Kwa dharura au maswali zaidi, wasiliana na Ubalozi wa Tanzania ulio karibu kama ifuatavyo:

1772522725351.png
 
K’manina zao. Hivyo vita kwa siku nne vimeua watu ambao hawafiki hata elfu moja. Wao mazafakas kwa siku mbili tatu waliua thousands of innocent Tanzanians. They’re more dangerous than that war!
 
Vipi kwa wanaoenda iran, mbona hawajakumbukwa?
 
Back
Top Bottom