TAARIFA KWA UMMA
USHAURI WA HALI YA USALAMA NA USAFIRI KWA RAIA WA TANZANIA WANAOISHI AU KUSAFIRI MASHARIKI YA KΑΤΙ
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inafuatilia kwa karibu hali ya usalama inayoendelea katika eneo la Mashariki ya Kati. Kutokana na mazingira ya kiusalama yanayoendelea, Serikali inatoa ushauri kwa raia wa Tanzania wanaoishi au wanaopanga kusafiri kwenda katika eneo hilo, ikiwemo Bahrain, Israel, Kuwait, Qatar, Falme za Kiarabu (UAE) na Oman.
Serikali inapenda kuwajulisha wananchi kuwa, kwa nyakati kama hizi, usaidizi wa kibalozi ana kwa ana unaweza kuwa na mipaka kulingana na eneo alipo mhusika na hali halisi ya kiusalama. Hivyo, raia wote
wanahimizwa kuchukua tahadhari stahiki na kufuata maelekezo ya mamlaka husika.
Watanzania waliopo katika eneo la Mashariki ya Kati wanashauriwa kuzingatia maelekezo yafuatayo:
- Kuepuka kufanya safari za kwenda au kutoka Mashariki ya Kati katika kipindi hiki.
- Kubaki katika makazi mnayoishi inapowezekana.
- Kufuata maagizo yanayotolewa na mamlaka za maeneo husika na kuwa waangalifu wakati wote.
- Kuepuka maeneo yenye shughuli za usalama/kijeshi katika maeneo mnayoishi.
- Kutumia njia rasmi za mawasiliano na taarifa.
- Kuhifadhi pasipoti na vitambulisho vya Tanzania sehemu salama na inayopatikana haraka endapo kutatokea dharura.
Serikali inawasihi Watanzania walioko Mashariki ya Kati kujisitiri kwa uangalifu na kuendelea kufuatilia mawasiliano rasmi ya Ubalozi na ya dharura. Aidha, Watanzania wanaombwa kujisitiri kwa usajili kupitia kiunganishi kifuatacho kwa ajili ya ufuatiliaji wa karibu:
Ministry of Foreign Affairs and East African Co-operation, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Oversees Foreign Relations, conducts diplomacy; creates foreign policy; operates embassies and provides visa and passport service; as well as working with other...
Kwa dharura au maswali zaidi, wasiliana na Ubalozi wa Tanzania ulio karibu kama ifuatavyo: