Tahadhari: Huyu ni tapeli wa Kujiaminisha?

Na wewe ni yuleyule, mbona picha zote mbili zimepigwa siku moja sehemu moja. Picha ya kwanza inaonesha shati alilovaa ndilo alilovaa Moro na ukuta unaoonekana Ubungo ndio unaonekana Moro. Kwa hali hii atakuwa amekuambukiza kusema uongo au nia yako ni kutuonesha unayo gari yenye kamera, kama ni hivyo hongera.
 
Picha na video zote ni za Morogoro. Kama umeangalia vizuri hiyo picha imekuwa captured toka kwenye video hiyohiyo ya Morogoro.
 
Polis hawa hawa
 
Miaka hiyo nipo dukan mwenge nauza nguo. Akaja mzee mtu mzima. Akasalimia then akaniambia mwanangu Mimi baba yako nina shida ya nguo unaona nilizovaa zilivyoisha na kweli amevaa matambara ya kutosha. Kabla cjamjibu akashuka chini akapiga sala flan ya kiislam huku akinisih Mungu atanibariki. Basi mi nakuonea huruma nikamfungia nguo za kutosha na viatu juu. Haijapita mwez mzee akajichanganya dukan kwangu kkoo kwa style ile ile nilimtukana akaondoka kimya kimya.
 
Utashangaa kusikia huyo jamaa nimekumbana naye Dar, Morogoro na Mbeya. Mbeya nami nikiwa napita kama mgeni, nikiwa nimepaki gari pembeni ya barabara, huku mwenyeji wangu kaniachia usukani, (mwenyeji aliingia ofisi za ardhi) mara paapu, akatokea huyo jamaa (anachagua watu). Akajifanya alikuwa anafanya kazi kama intern ofisi za ardhi Mbeya kipindi cha Lukuvi. Akasema hawajalipwa bado pesa za miezi kadhaa, hivyo anaomba msaada aisitiri familia yake. Nikasema bwana mimi miguu hata haijapoa moto na ndio nimefika tu Mbeya kwa mtu, kawaombe wenyeji wenye pesa. Aliniharibia siku. Dar vuupu, karibu na Mlimani City, story zilezile, mara mji kasoro bahari akajihusisha na SUA kusoma Master. Nikamwambia shida ukiwa tapeli unahitaji usiwe unasahau, ukisahau utakuja kukamatwa. Nilidhani Afro zangu au rangi yangu ni rahisi kunikumbuka na kunikwepa. Nikamwambia utakufa maskini.

Huyo mjamaa ukisema huna pesa, au ukashtuka, atakufanya nafsi yako ijutie. Utajiona kama shetani, kumbe yeye ni tapeli kubwa. Wako wengi matapeli wa namna hiyo.

 
Watu kama hawa ndio wanaharibia wenye shida, dhiki na uhitaji hasa.

Nakumbuka mwaka 2017 nikiishi Ubungo nilitingwa sina kazi na sina hata mia mbovu MFUKONI sikuweza kuamini ilinibidi niombe kwa wasamaria hata hela ya kula njaa ilinikung'uta balaa

Akatokea mwanafunzi mmoja wa Udsm pale Mabibo hostel akanipiga tafu kwa kunipa 2k ndio nikaweza kupata chakula.

Natamani leo hii ningeweza hata kumtambua yule bro nimshukuru kwa moyo mkuu but ndio hivo tena.
Ninachoweza na mimi ni kusaidia pale ninapoweza until my last time.
 

Mara nyingi ukitendewa wema na mtu sio rahis sana kurudisha wema kwake isipokuwa cha kufanya tenda wema kwa wengine. Jinsi unavyotamani kumpata na kumshukuru ndivyo Mungu alivyombariki na kufikisha shukrani zako kwake kupitia kwa watu wengine. Amani ya Mungu itawale kwako
 
Mimi juzi kati nilikuwa natoka tu kwenye ATM mahali, nakutana na kijana ananisimisha eti!

Kiukweli sikujishughulisha kabisa kusimama au kumsikiliza!! Maana nilijua angeniletea tu zile story za kuokota madini ya almasi, au kujifanya ana shida.
 
Nazan hii tabia yakuomba nakujipatia pesa zabwerere inakautamu flan ivi .sasa mimi juzi tu hapa mzee mmoja kanifuata nakunipanga kijana sijala nisaidie nikaona sio kesi nikazama mfukon nikampa pesa kdg ,nimetembea hatua kama 6 nageuka nyuma nakuta anampanga tena dada mmoja nae bila hiana akazana kwene pochi akampa pesa ,chap akavuka rod akaenda kijiwe cha bodaboda nako akaanza kuwapanga sema wengi wakawa wanachomoa mpaka mmoja akajitolea kumpa chochote ndio akachomoka.nikajisemea kumbe uyu mzee mhuni nakwasiku itakuwa anakusanya maokoto yakutosha tu
 
Humu wapo sana katika sekta ya kuabisha watu wanafurahi sana ila sasa ukiwa unahitaji kazi hawakupi mtaji hawakupi.

Yaani maisha huwa ni mazuri endapo ukimkalisha nakumwambia sema ukweli usaidike naje tukijikusanya tukakufungulia kitu kidogo ujisogeze kimaisha wewe na watoto.

Humu mna ngo's nyingi ila kuwasaidia wenzenu mbaya kabisa . Hamtaki . Mtu kachanganyikiwa he needs help sio unafikoa hadi ubamrekodi yanini wewe mtoa mada unajiona halafu unajiita Amani ya Mungu huna hayaa
 
pole sana ungekufa aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…