Unique Flower
JF-Expert Member
- Apr 19, 2019
- 12,838
- 25,282
Ukimsaidia akarudia kile unamriport kabisa polisi ila hajasaidiwa . Mie najuaAlikuwa Ubungo, then Tabata then Morogoro
Unataka Tapeli awe vipi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukimsaidia akarudia kile unamriport kabisa polisi ila hajasaidiwa . Mie najuaAlikuwa Ubungo, then Tabata then Morogoro
Unataka Tapeli awe vipi?
Naomba nikiri hoja yangu imelenga kuleta hoja vijana wajitume na sio kuwa ombaomba ilihali wana nguvu.
View attachment 2933415
Mwaka 2023 mwezi wa 5 nikiwa natembea maeneo ya Ubungo jirani na NBC bank alikuja kijana ambaye anaonekana kwenye video hapa na akaniambia yeye ni mwalimu amemaliza SUA na amepata kazi Songwe hivyo anaomba nimuongezee nauli ili aweze kufika. Alinifuata kwa nidhamu na kwa namna alivyokuwa akiongea (Angalia hata hii video hapa anavyojieleza kwa ustadi) niliamini kweli ni mtu mwenye elimu yake na pengine kweli hana kazi ndio amepata. Nikaona si vibaya nikijigeuza kuwa malaika wa zamu kwake ili afanikishe safari ya kwenda Songwe alipodai amepata kazi. Nikamuuliza nauli akanitajia na na akasema aka niasi kidogo kama elfu 10, nikampa, Sikumbuki ni kiasi gani ila kama sio kwenye 40,000 maana nilihakikisha nampa nauli ya kumfikisha. Akanishukuru sana akanipa na namba yake but sikuiSave kiukweli (Good enough alikuwa na smartphone)
Tarehe 10 Machi, Mwaka 2024 nikiwa kwenye gari nimetoka Mazimbu naenda mjini, nimefika na kusimama sehemu ya mataa, Mtu yuleyule niliyemsaidia nauli ya kwenda Songwe kwenye kazi, nimekutana nae tena na akagonga kioo na kuomba nisimame mbele baada ya mataa. Mawazo yangu nikajua pengine ameniona na amenikumbuka anataka kunishukuru kwa msaada niliowahi kumpa, Baada ya kuvuka mataa na kusimama kumsikiliza pengine anashukuru kwa msaada wa awali, nikashangaa analeta maombi ya aina ileile.
Bahati mbaya baada ya kumwambia siku nyingine aliondoka na wakat namuita ili nimkumbushe akawa ameondoka hakutaka hata kusikiliza. Wakati namtafakari hasa kuwaza umbali wa kutoka relini ambako amedai aliponiona ndio amenikimbilia, nikakumbuka kuwa Dashboard camera yangu ilikuwa on nikataka kuprove kweli aliniona tangu relini? nikaendelea kujiridhisha kuwa ni Muongo.
Baada ya kutembea takriban Mita 400 kutoka relini, (sehemu ambayo yeye alisema ndipo aliniona na kunikimbilia) ndipo alionekana akitembea kuelekea uelekeo ambao nilikuwa nakwenda kupitia camera ya mbele. Nilipofika usawa wake mbele kidogo ndipo alionekana kuangalia gari kupitia camera ya kulia. ndipo akaamua kuja na kuvuka upande wa abiria kama anavyoonekana kupitia camera ya nyuma. na hatimaye maelezo yake ni kama anavyoonekana kupitia camera ya kushoto japo hajaonekana vizuri.
Tujihadhari na huyu mtu ni wazi atakuwa ndio mchezo wake kujipatia pesa kwa udanganyifu na pengine kafanya hivyo mikoa mingi.
Tazama Video nilipokutana nae Morogoro
View: https://youtu.be/sd2-OcpDkv0
UPDATE ZA ZA WADAU WENGINE WALIOKUTANA NA HUYU BWANA:

Kweli aiseeeeWananusa sana.. kuna muonekano mtu ukiwa nao ni wa Hela hela... unashawishi watu wa aina hii wakusogelee/wakusemeshe..
Kuna namna fulani mtu ukitokea maeneo mbalimbali.. unanukia hela... humalizi safari bila kuombwa ombwa hela hovyo..
Exactly.. kama mnuko wa Shida/umaskini..Kweli aiseeee
Kuna namna pesa huwa inapiga kelele...
Wanachokifanya watu kama huyu aliyerekodiwa ndio kinasababisha watu wenye uwezo wa kutusaidia wasitusaidie kwa sababu kuna wachache matapeli kama hawa wametuharibia na wote tunaonekana hatusaidiki/matapeli. Huyu anachokifanya ni Uovu, hivyo kuuweka wazi uovu sio jambo baya. Usimtetee.Humu wapo sana katika sekta ya kuabisha watu wanafurahi sana ila sasa ukiwa unahitaji kazi hawakupi mtaji hawakupi.
Yaani maisha huwa ni mazuri endapo ukimkalisha nakumwambia sema ukweli usaidike naje tukijikusanya tukakufungulia kitu kidogo ujisogeze kimaisha wewe na watoto.
Humu mna ngo's nyingi ila kuwasaidia wenzenu mbaya kabisa . Hamtaki . Mtu kachanganyikiwa he needs help sio unafikoa hadi ubamrekodi yanini wewe mtoa mada unajiona halafu unajiita Amani ya Mungu huna hayaa
Wewe ni mtu wa 7 sasa kumkumbuka mtu yuleyuleDaaah, hawa ndo wanasababisha watu waishi kama wanyama....
Kwa huruma na ubinadamu, nilimtumia kiasi cha pesa kwenye simu, apate nauli ya kwenda Songwe, kula njiani na kumtumia mama watoto wake kwa ajili ya chakula cha jioni hiyo.
Alinifuata nikiingia kwenye ka-mini supermarket pale Goba, nikipanga ninunue vilevi nikaburudike, nika ahirisha ili kutoa msaada!
Pumbavu sana!
Acha tu mzee 🤣pole sana ungekufa aisee
🙏🙏 Sahihi mkuuMara nyingi ukitendewa wema na mtu sio rahis sana kurudisha wema kwake isipokuwa cha kufanya tenda wema kwa wengine. Jinsi unavyotamani kumpata na kumshukuru ndivyo Mungu alivyombariki na kufikisha shukrani zako kwake kupitia kwa watu wengine. Amani ya Mungu itawale kwako
Na mimi namkumbuka vizuri sana. Nilikutana nae mwaka jana Mbezi, Dar maeneo ya jirani na Magufuli bus terminal. Alinisimamisha na kunipa mkono wa salaam ambao mimi sikuupokea nikijifanya kupiga chafya ya ghafla maana uwa sina kawaida ya kushikana mikono na mtu nisiyemfahamu. Akaanza kunieleza kuwa ni mmoja wa watumishi wa serikali waliotumbuliwa kwa vyeti feki na sasa anatafuta nauli elfu 30 akapande magari ya IT ili awahi kazi aliyoitiwa Songwe. Uongeaji wake ndiyo huo huo wa kuchanganya lugha ya kiswahili na kiingereza maana alishajua akikutana na watu wa aina fulani akitumia mbinu hiyo ya kuchanganya lugha atawafanya kumwamini na kumsaidia. Mimi pamoja na kumsikiliza nilimshitukia na hivyo nikamwambia hapa nilipo nami sina kitu. Ajabu baada ya kumwambia vile alisonya na kuondoka kwa hasira. Wakati anaondoka kwa staili ile nilimpazia sauti na kumwambia "Oya wewe vipi? Nimekusikiliza shida yako nami nimekwambia sina hela halafu unanisonya?! Huna lolote wewe ni msanii tu na hapa kwangu umekwama". Yeye akaendelea kwenda na hasira zake. Kiukweli baada ya kuwa ameondoka baadae mimi moyoni nilibaki najilaumu kwa kumwambia maneno yale ya kumsindikizia maana pengine kweli alikuwa na shida na siyo kwamba alikuwa akifanya utapeli. Sasa kwa kumwona kwenye video hii na kwa kusoma shuhuda za wadau nimejipongeza kwa kutokupoteza hela yangu kwa tapeli maana kiukweli hela ya kumpa nilikuwa nayo mfukoni.Wewe ni mtu wa 7 sasa kumkumbuka mtu yuleyule
Yaani umkomoe kwa kwenda nae stendi na kumkatia tiketi? Kama haendi hiyo tiketi utampa nani aitumie au utaamua kumgawia abiria mwingine yoyote atakaekuwa anasafiri? Hapo sasa itakuwa ni kujikomoa mwenyewe.Watu kama hawa ukitaka kiwakomoa wapeleke stand uwalipie nauli umpe tiketi. Kama muda upo hakikisha anapanda bus na kuondoka. Ukigundua ni Tapeli, Piga picha tuma hata polisi waendelee na majukumu ya kunyoosha taifa.
Tusiache kutenda mema, maana wengine kwa kufanya hivi wamewasaidia na malaika -Biblia
Huyo jamaa ukishamtamkia tu kuwa huna hela ya kumpa ubadilika ghafla na hataki kuendelea kuongea chochote na wewe. Ni kama ndagu kwake kwamba ili asije akakosa hela ya kutapeli kwa mtu mwingine atakaekuja akishaambiwa na huyu wa sasa kuwa hana hela asiendelee kuongea nae.Jamaa anaonekana smart kichwani, angetuliza kichwa chake naamini angeweza jipatia kipato kihalali.
Tone ilibadilika ghafla kutoka muungwana mpaka kwenda kibabe ghafla baada ya kumwambia siku nyingine; naamini ndipo pia alikukumbuka kuwa alishawahi kuvuna toka kwako.
Kweli mjini mipango😂
Unaweza kutoa mawazo yako ya namna ya kuwasaidia maana ni wengi.Pole Ila mnabidi kujua tatizo la MTU mpaka kuamua kuwa ombaomba au tapeli ni tatizo la AKILI.
Maisha ni kitendo cha mchakato na sio Ajali , MTU unayekutana naye Leo ukimtapeli na kumfanyia ubaya maana yake unakuwa umeharibu sehemu kubwa ya maisha yako.
Hivyo badala ya kuwalaumu ombaomba na matapeli ,tuangalie namna au njia bora ya sisi kumbadilisha ombaomba (tapeli) hadi kuwa MTU mwema.
When you steal from others you steal from your self keep this on your mind.
Always ur Input determines your output
tapeli lingine ni hiliHumu wapo sana katika sekta ya kuabisha watu wanafurahi sana ila sasa ukiwa unahitaji kazi hawakupi mtaji hawakupi.