Naomba nikiri hoja yangu imelenga kuleta hoja vijana wajitume na sio kuwa ombaomba ilihali wana nguvu.
View attachment 2933415
Mwaka 2023 mwezi wa 5 nikiwa natembea maeneo ya
Ubungo jirani na NBC bank alikuja kijana ambaye anaonekana kwenye video hapa na akaniambia yeye ni mwalimu amemaliza SUA na amepata kazi Songwe hivyo anaomba nimuongezee nauli ili aweze kufika. Alinifuata kwa nidhamu na kwa namna alivyokuwa akiongea
(Angalia hata hii video hapa anavyojieleza kwa ustadi) niliamini kweli ni mtu mwenye elimu yake na pengine kweli hana kazi ndio amepata. Nikaona si vibaya nikijigeuza kuwa malaika wa zamu kwake ili afanikishe safari ya kwenda Songwe alipodai amepata kazi. Nikamuuliza nauli akanitajia na na akasema aka niasi kidogo kama elfu 10, nikampa, Sikumbuki ni kiasi gani ila kama sio kwenye 40,000 maana nilihakikisha nampa nauli ya kumfikisha. Akanishukuru sana akanipa na namba yake but sikuiSave kiukweli (Good enough alikuwa na smartphone)
Tarehe 10 Machi, Mwaka 2024 nikiwa kwenye gari nimetoka Mazimbu naenda mjini, nimefika na kusimama sehemu ya mataa,
Mtu yuleyule niliyemsaidia nauli ya kwenda Songwe kwenye kazi, nimekutana nae tena na akagonga kioo na kuomba nisimame mbele baada ya mataa. Mawazo yangu nikajua pengine ameniona na amenikumbuka anataka kunishukuru kwa msaada niliowahi kumpa, Baada ya kuvuka mataa na kusimama kumsikiliza pengine anashukuru kwa msaada wa awali, nikashangaa analeta maombi ya aina ileile.
Bahati mbaya baada ya kumwambia siku nyingine aliondoka na wakat namuita ili nimkumbushe akawa ameondoka hakutaka hata kusikiliza. Wakati namtafakari hasa kuwaza umbali wa kutoka relini ambako amedai aliponiona ndio amenikimbilia, nikakumbuka kuwa Dashboard camera yangu ilikuwa on nikataka kuprove kweli aliniona tangu relini? nikaendelea kujiridhisha kuwa ni Muongo.
Baada ya kutembea takriban
Mita 400 kutoka relini, (sehemu ambayo yeye alisema ndipo aliniona na kunikimbilia) ndipo alionekana akitembea kuelekea uelekeo ambao nilikuwa nakwenda kupitia camera ya mbele. Nilipofika usawa wake mbele kidogo ndipo alionekana kuangalia gari kupitia camera ya kulia. ndipo akaamua kuja na kuvuka upande wa abiria kama anavyoonekana kupitia camera ya nyuma. na hatimaye maelezo yake ni kama anavyoonekana kupitia camera ya kushoto japo hajaonekana vizuri.
Tujihadhari na huyu mtu ni wazi atakuwa ndio mchezo wake kujipatia pesa kwa udanganyifu na pengine kafanya hivyo mikoa mingi.
Tazama Video nilipokutana nae Morogoro
View: https://youtu.be/sd2-OcpDkv0
UPDATE ZA ZA WADAU WENGINE WALIOKUTANA NA HUYU BWANA: