Tahadhari: Huyu ni tapeli wa Kujiaminisha?

Huyu ni smart kabisa na amejipanga
Huenda anaingiza pesa nyingi sana kwa siku
 
Sahivi utapeli nje nje kaka
 
Wananusa sana.. kuna muonekano mtu ukiwa nao ni wa Hela hela... unashawishi watu wa aina hii wakusogelee/wakusemeshe..

Kuna namna fulani mtu ukitokea maeneo mbalimbali.. unanukia hela... humalizi safari bila kuombwa ombwa hela hovyo..
 
Wananusa sana.. kuna muonekano mtu ukiwa nao ni wa Hela hela... unashawishi watu wa aina hii wakusogelee/wakusemeshe..

Kuna namna fulani mtu ukitokea maeneo mbalimbali.. unanukia hela... humalizi safari bila kuombwa ombwa hela hovyo..
Kweli aiseeee
Kuna namna pesa huwa inapiga kelele...
 
Mjini mipango.

Kuna bi'mkubwa mmoja anaprint matokeo ya darasa la 7 yale ya straight A's anatembea na watoto sijui ni wake au vipi, anapita penye mikusanyiko, mashuleni na taasisi mbali mbali akidai mtoto hana ada wala mahitaji ya shule yule bi'mkubwa akapiga hela mbaya mbovu.

Mara paap nakutana naye mikoa ya wapare na Wachagga huko anataka apige hela kwa gia ile ile na mtoto yule yule na ni mwaka ushapita, huruma yangu tu yule mama alikua anakufa siku ile, ila alipata somo naimani baada ya kumuwekwa mtu kati na raia kadhaa wenye hekima.
 
Wanachokifanya watu kama huyu aliyerekodiwa ndio kinasababisha watu wenye uwezo wa kutusaidia wasitusaidie kwa sababu kuna wachache matapeli kama hawa wametuharibia na wote tunaonekana hatusaidiki/matapeli. Huyu anachokifanya ni Uovu, hivyo kuuweka wazi uovu sio jambo baya. Usimtetee.

Amani ya Mungu iwe nawe
 
Pole Ila mnabidi kujua tatizo la MTU mpaka kuamua kuwa ombaomba au tapeli ni tatizo la AKILI.

Maisha ni kitendo cha mchakato na sio Ajali , MTU unayekutana naye Leo ukimtapeli na kumfanyia ubaya maana yake unakuwa umeharibu sehemu kubwa ya maisha yako.


Hivyo badala ya kuwalaumu ombaomba na matapeli ,tuangalie namna au njia bora ya sisi kumbadilisha ombaomba (tapeli) hadi kuwa MTU mwema.


When you steal from others you steal from your self keep this on your mind.

Always ur Input determines your output
 
Daaah, hawa ndo wanasababisha watu waishi kama wanyama....

Kwa huruma na ubinadamu, nilimtumia kiasi cha pesa kwenye simu, apate nauli ya kwenda Songwe, kula njiani na kumtumia mama watoto wake kwa ajili ya chakula cha jioni hiyo.

Alinifuata nikiingia kwenye ka-mini supermarket pale Goba, nikipanga ninunue vilevi nikaburudike, nika ahirisha ili kutoa msaada!

Pumbavu sana!
 
Wewe ni mtu wa 7 sasa kumkumbuka mtu yuleyule
 
🙏🙏 Sahihi mkuu
 
Wewe ni mtu wa 7 sasa kumkumbuka mtu yuleyule
Na mimi namkumbuka vizuri sana. Nilikutana nae mwaka jana Mbezi, Dar maeneo ya jirani na Magufuli bus terminal. Alinisimamisha na kunipa mkono wa salaam ambao mimi sikuupokea nikijifanya kupiga chafya ya ghafla maana uwa sina kawaida ya kushikana mikono na mtu nisiyemfahamu. Akaanza kunieleza kuwa ni mmoja wa watumishi wa serikali waliotumbuliwa kwa vyeti feki na sasa anatafuta nauli elfu 30 akapande magari ya IT ili awahi kazi aliyoitiwa Songwe. Uongeaji wake ndiyo huo huo wa kuchanganya lugha ya kiswahili na kiingereza maana alishajua akikutana na watu wa aina fulani akitumia mbinu hiyo ya kuchanganya lugha atawafanya kumwamini na kumsaidia. Mimi pamoja na kumsikiliza nilimshitukia na hivyo nikamwambia hapa nilipo nami sina kitu. Ajabu baada ya kumwambia vile alisonya na kuondoka kwa hasira. Wakati anaondoka kwa staili ile nilimpazia sauti na kumwambia "Oya wewe vipi? Nimekusikiliza shida yako nami nimekwambia sina hela halafu unanisonya?! Huna lolote wewe ni msanii tu na hapa kwangu umekwama". Yeye akaendelea kwenda na hasira zake. Kiukweli baada ya kuwa ameondoka baadae mimi moyoni nilibaki najilaumu kwa kumwambia maneno yale ya kumsindikizia maana pengine kweli alikuwa na shida na siyo kwamba alikuwa akifanya utapeli. Sasa kwa kumwona kwenye video hii na kwa kusoma shuhuda za wadau nimejipongeza kwa kutokupoteza hela yangu kwa tapeli maana kiukweli hela ya kumpa nilikuwa nayo mfukoni.
 
Yaani umkomoe kwa kwenda nae stendi na kumkatia tiketi? Kama haendi hiyo tiketi utampa nani aitumie au utaamua kumgawia abiria mwingine yoyote atakaekuwa anasafiri? Hapo sasa itakuwa ni kujikomoa mwenyewe.
 
Wapiga mizinga+ sound hao

Wanaishi kwa style hiyo

Ova
 
Huyo jamaa ukishamtamkia tu kuwa huna hela ya kumpa ubadilika ghafla na hataki kuendelea kuongea chochote na wewe. Ni kama ndagu kwake kwamba ili asije akakosa hela ya kutapeli kwa mtu mwingine atakaekuja akishaambiwa na huyu wa sasa kuwa hana hela asiendelee kuongea nae.
 
Unaweza kutoa mawazo yako ya namna ya kuwasaidia maana ni wengi.
Pamoja na yote bado wanachokifanya ni Utapeli wa kujipatia pesa kwa uongo. Mtu anayepata hela kwa njia hizi hawezi kupata akili ya kuendelea maana anaamini na kesho akiomba atapata.
 
tapeli lingine ni hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…