King Kong III
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 56,205
- 79,515
Kimbunga Jobo.Kimbunga hiki/upepo mkali ukiambatana na mvua kubwa huenda vikatokea pwani yetu hususan miji ya Lindi,Mtwara,Dar es salaam,Unguja,Mombasa,Malindi
Chanzo kinasema upepo huo unatarajiwa kati ya tarehe 21/4/2021 na 26/4/2021.
Hivyo tuchukue tahadhari na bahari kwa siku hizi,na kufuatilia utabiri wa hali ya hewa
Nchi nyingine zitakazoathirika ni pamoja na,Madagascar,Seychelles,Mayote na Msumbiji
Chanzo cha Habari@ al Jazeera news /weather report.
Kwa hiyo ni ishu serious! Mbona kama mamlaka zimezubaa!? nikikumbuka kile cha Msumbiji mwaka juzi naingiwa na hofu sana. Kama kawaida yetu tutaanza kutafutana na kukimbizana baada ya majanga.Per CNN kuna vimbunga viwili tu kama hiki vilivyoipiga Dar es salaam, mwaka 1952 na mwaka 1872 hapo mji ulikuwa bado unaanzishwa.
Msumbiji mbona hata January mwaka huu kuna kingine kilipiga.Kwa hiyo ni ishu serious! Mbona kama mamlaka zimezubaa!? nikikumbuka kile cha Msumbiji mwaka juzi naingiwa na hofu sana. Kama kawaida yetu tutaanza kutafutana na kukimbizana baada ya majanga.
hahahaWote tunajua TMA hawana uwezo huo, wasitishe watu.
Kama mnabisha, ngoja muone.
Kongamano lilishamaliza kila kituKimbunga Jobo kinaelekea Tanzania, ni cha aina yake tokea 1952
Apr 22, 2021 11:22 UTC
Kimbunga kikali zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini Tanzania miongo ya karibuni kinatazamiwa kutua katika ukanda wa pwani ukiwemo mji wa Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mashirika ya kimataifa ya utabiri wa hali ya hewa, kimbunga hicho ambacho kinajulikana kama Jobo kinatarajiwa kuwa kikubwa zaidi kuwahi kutua Tanzania tangu mwaka 1952.
Kwa mujibu wa taarifa, jana kimbunga hicho kilionekana kaskazini mwa Madagascar kikiwa na kasi ya kilomita 83 kwa saa.
Utabiri unaonyesha kuwa kimbunga hicho kitapita eneo la Ushelisheli leo Aprili 22 kikiwa na kasi ya kilomita 130 kwa saa na kinatazamiwa kutua Tanzania Aprili 24 au 25.
Upepo mkali wakati wa kimbunga
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetahadahrisha kuwa kimbunge hicho cha Bahari ya Hindi kinaweza kusababisha upepo mkali na mawimbi makubwa baharini katika maeneo ya Lindi na Mtwara. Aidha kuna uwezekano wa kutokea mafuriko katika maeneo athirika.
TMA imesema itaendelea kufuatilia kimbunga Jobo na kuwapasha wananchi habari kuhusu tahadhari zinazopasa kuchukuliwa.
Full kichefu chefu yaani. Dah.Jobo Ndugai
Sidhan if TMA hata wanajua nn kinaendelea manake nimeona cnn ndio imetangazaLikitokea ilo Katrina nitarudisha imani na TMA.
Maneno gan aisee[emoji28]RIP WANA DAR ES SALAAM
Wengne tupo dar kimasomo unatutisha [emoji23]RIP WANA DAR ES SALAAM
Mkuu la msingi ni kufuata tahadhari zilizotolewa na watalaamu..hoja yangu ilikua ni wangapi wanafuatilia hizi habari?Tulitakiwa tufanyaje sasa mkuu . Tupanic na kuanza kuukimbia mji?
NILISEMA.. Hawa jamaa hawa.. Mi naona watumbuliwe wote..Likitokea ilo Katrina nitarudisha imani na TMA.