Tahadhari: Kimbunga hiki/upepo mkali ukiambatana na mvua kubwa huenda vikatokea pwani ya Tanzania

Tahadhari: Kimbunga hiki/upepo mkali ukiambatana na mvua kubwa huenda vikatokea pwani ya Tanzania

Kimbunga hiki/upepo mkali ukiambatana na mvua kubwa huenda vikatokea pwani yetu hususan miji ya Lindi,Mtwara,Dar es salaam,Unguja,Mombasa,Malindi

Chanzo kinasema upepo huo unatarajiwa kati ya tarehe 21/4/2021 na 26/4/2021.

Hivyo tuchukue tahadhari na bahari kwa siku hizi,na kufuatilia utabiri wa hali ya hewa

Nchi nyingine zitakazoathirika ni pamoja na,Madagascar,Seychelles,Mayote na Msumbiji

Chanzo cha Habari@ al Jazeera news /weather report.
Kimbunga Jobo.
 
Per CNN kuna vimbunga viwili tu kama hiki vilivyoipiga Dar es salaam, mwaka 1952 na mwaka 1872 hapo mji ulikuwa bado unaanzishwa.
Kwa hiyo ni ishu serious! Mbona kama mamlaka zimezubaa!? nikikumbuka kile cha Msumbiji mwaka juzi naingiwa na hofu sana. Kama kawaida yetu tutaanza kutafutana na kukimbizana baada ya majanga.
 
Kwa hiyo ni ishu serious! Mbona kama mamlaka zimezubaa!? nikikumbuka kile cha Msumbiji mwaka juzi naingiwa na hofu sana. Kama kawaida yetu tutaanza kutafutana na kukimbizana baada ya majanga.
Msumbiji mbona hata January mwaka huu kuna kingine kilipiga.

Inaonekana kama mabadiliko ya hali ya hewa yanafanya hivi vimbunga viwe vinatokea zaidi siku hizi.

 
Kimbunga Jobo kinaelekea Tanzania, ni cha aina yake tokea 1952

Apr 22, 2021 11:22 UTC

Kimbunga kikali zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini Tanzania miongo ya karibuni kinatazamiwa kutua katika ukanda wa pwani ukiwemo mji wa Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mashirika ya kimataifa ya utabiri wa hali ya hewa, kimbunga hicho ambacho kinajulikana kama Jobo kinatarajiwa kuwa kikubwa zaidi kuwahi kutua Tanzania tangu mwaka 1952.

Kwa mujibu wa taarifa, jana kimbunga hicho kilionekana kaskazini mwa Madagascar kikiwa na kasi ya kilomita 83 kwa saa.

Utabiri unaonyesha kuwa kimbunga hicho kitapita eneo la Ushelisheli leo Aprili 22 kikiwa na kasi ya kilomita 130 kwa saa na kinatazamiwa kutua Tanzania Aprili 24 au 25.

Upepo mkali wakati wa kimbunga

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetahadahrisha kuwa kimbunge hicho cha Bahari ya Hindi kinaweza kusababisha upepo mkali na mawimbi makubwa baharini katika maeneo ya Lindi na Mtwara. Aidha kuna uwezekano wa kutokea mafuriko katika maeneo athirika.

TMA imesema itaendelea kufuatilia kimbunga Jobo na kuwapasha wananchi habari kuhusu tahadhari zinazopasa kuchukuliwa.
Kongamano lilishamaliza kila kitu
 
Kimbunga kinaitwa Jobo weekend hii kitatandika Mikoa ya Pwani, Dar es salaam ikiwemo. Mvua za kufa mtu hasa hasa Jumapili 25/April/2021


 

Attachments

Likitokea ilo Katrina nitarudisha imani na TMA.
 
Tulitakiwa tufanyaje sasa mkuu . Tupanic na kuanza kuukimbia mji?
Mkuu la msingi ni kufuata tahadhari zilizotolewa na watalaamu..hoja yangu ilikua ni wangapi wanafuatilia hizi habari?
 
Back
Top Bottom