TAHADHARI: Kuna matapeli! Fuata taratibu hizi...

Huu uzi unanikumbusha mbali sana.
Miongoni mwa miujiza yangu mikubwa michache ni, kukutana na wewe, kuongea na wewe kusafiri na wewe na kuwa na namba yako.

Mungu akupe haja ya moyo wako, ninakuombea sana, kwenye nyakati zako zote, za mapito yako yote.
Kwenye dhoruba, nakuombea Amani, kwenye Amani nakuombea ustawi, ustawi zaidi na zaidi, zaidi ya mtende ulioota kwenye Oasis
 
Mmeshamkamata huyo tapeli?
 
Salaam
Naunga mkono Tangazo hili ni kweli baadhi ya watu sio waaminifu katika kufanya baishara


Ushauii
Endapo unafanya Biashara mtandaoni Tafadhali fanya yafuatayo:


Tambua Jina halisi la Muuzaji ikiwezekana muombe nakala ya kitambulisho cha taifa au uthibitisho wowote halali kuwa ni yeye
Kama ni biashara muombe Profile ya kampuni yake (Jina la kampuni, nakala ya usajili wa biashara, TIN namba,) na mawasiliano na wateja ambao alishafanya nao kazi
Omba anuani ya ofisi ake kisha nenda ukamtembelee kama ni mkoani tuma mtu unaemuamini afike ofisini kwake
Kama ni kazi au biashara ni kubwa muobe taarifa zake za fedha za mwaka
Majadiliano yenu yafanyike kwenye ofisi ya wakili au mbele ya mashahidi wa pande zote mbili mnaowaaamini

Kwa ushauri zaidi tunaweza kusawasiliana
 
Mkuu,mimi ninamfahamu tapeli mmoja aliyenitapeli ambaye ana vigezo hivo vyote.

Nilichojifunza kama mtu ambaye anafanya ninafanya biashara na watu ambao wengine hatujawahi kuonana ni kwamba Ukiona una hofu ya kutapeliwa basi do not go through with the deal.Kufanya biashara na mtu usiyemfahamu ni risk sana.Hata hivyo najua pia kuwa utapeli ni silka ya mtu.Yaani kuna watu ni matapeli regardless na wanapenda maisha ya kuwa kama DIGI DIGI hata wakiwa na vibali bado lengo lao linakuwa ni hilo hilo kutapeli.

Mimi huwa ninasheria zangu za msingi.

Kwanza if the deal is too GOOD to be true then RUN.If you are taking too much RISK then RUN.Risk what you are willing and able to loose with minimum impact.

Kuna watu humu ambao nimewahi kufanya nao DEALS kubwa hata nikikutana nao siwafahamu wala hawanifahamu.Kuna ambao tumebahatika kufahamiana na tukawa marafiki wazuri ila wengine hatujawahi onana kabisa ila nawaheshimu kwa kuwa waaminifu na ninaamini pia a wao wananiheshimu kwa kuwa muaminifu kwao.

Nilochojifunza kwa kazi za mtandaoni ni kutokuchukua RISKS za kijinga hasa unapoona kabisa hiki kitu sicho ila bado unakimbilia kwa sababu ama ya tamaa au kutafuta unafuu fulani.
 
Vp kama mtu akitaka kununua gari kwa watu wa mitandaoni. Afuate au azingatie mambo gani?.
 
Hakuna tapeli wa kudumu ... na pia mtu yoyote anaweza kuwa tapeli apatapo fursa ya kutapeli kutokana na ujinga wa mtu. La muhimu hapa watu wawe makini. Humu tupige soga na tupigane vijembe ila biashara za kweli zikafanyike TRA au kwa Balozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…