Wakuu,
Penye wengi, pana mengi pia. Jukwaa hili pamoja na kuwa na matangazo mengi, lakini wengine ni matapeli wakubwa sana. Tafadhali, tulishatoa angalizo na tunasisitiza tena: Mnapoamua kufanya biashara yoyote nje au ndani ya JF bila kutushirikisha msiilaumu JF.
Tunafahamu kuna ambao mmeshalizwa, tafadhali tufahamisheni ili tuweze kuwaanika (tutaanzisha thread maalum kwa ajili ya hili).
Nisisitize, IWENI MAKINI NA MATAPELI!
avatar yako imeniacha hoi!!!wakuu,
penye wengi, pana mengi pia. Jukwaa hili pamoja na kuwa na matangazo mengi, lakini wengine ni matapeli wakubwa sana. Tafadhali, tulishatoa angalizo na tunasisitiza tena: Mnapoamua kufanya biashara yoyote nje au ndani ya jf bila kutushirikisha msiilaumu jf.
Tunafahamu kuna ambao mmeshalizwa, tafadhali tufahamisheni ili tuweze kuwaanika (tutaanzisha thread maalum kwa ajili ya hili).
Nisisitize, iweni makini na matapeli!
Ni kweli kabisa kuna member humu ndani si waaminifu kabisa.Kuna mmoja januari mwaka huu aliniahidi kunipatia gari kwa Tsh. 3.5 m hadi leo sijaipata na fedha nilishampatia zaidi ya Tsh.3.8 m.Nimefadhaishwa sana na nasikitika sana na nimemwachia Mungu,maana nimepata tayari Gari lingine.Nina hakika haitamsaidia zaidi ya kumwongezea mateso na dhiki kuu ili ajue Mungu hajaribiwi.
nathani waliotapeliwa kimapenzi ni wengi sana humu
Naunga mkono hoja. Kweli humu JF kuna matapeli ingawa siyo wote. Mimi nimenunua sana kupitia JF na karibu mara zote nimeuziwa vitu genuine, kasoro mara moja. Nilinunua the so called universal solar charger for laptops and mobile phones. Muuzaji alimwaga sifa kibao mpaka nikaingia laini. Cha ajabu ni kwamba siyo charger hata kidogo bali ni kama universal battery ya laptops. Baada ya kumweleza matatizo yake muuzaji kakata mawasiliano, ingawa bado yumo JF.
Tujihadhari!!!
huyu mtu anajiita ukwelikitugani ashawahi kuniliza hela zangu! Pia alimdhulumu huyu dada sweetbaby.
ukwelikitugani, nimekusamehe ila naomba nikutaje kwa faida ya wanaJF wengine wasijedhulumiwa na wewe.
kama imethibitika ni tapeli, ifungwe akaunti yake, na ndo dawa pekee!