Tahadhari kwa wapenzi wa supu ya pweza

Tahadhari kwa wapenzi wa supu ya pweza

Nimekuwa kama samaki kutamani nisivyoviweza,
Kama ni tanga niliapa nioe muweza,
Na kama bahati mwenzenu nilishapoteza,
Siku hizi ujanja ni kunywa MCHUZI WA PWEZA.
 
Wakuu ! Wako wapi wataalam wa afya hapa JF ? Tupeni ukweli maana BAOBAO ni mpenzi wa supu ya pwenza nk
C.C. MziziMkavu
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli kabisa mm huwa situmii mchuzi wake na mabingwa wa uchanganyaji ni magomeni
 
Ni kama ubuyu wanachanganya na sembe kidogo ndy maana watu wamekuwa addicted hasa dd zetu mabingwa ni pale magomeni kituo cha SAMANGA KABLA YA KONA UNAONGIA KULIA NA KUNA MAKABURI
 
Hii imewagusa wengi na wengi walikuwa hawajui.

Nafunguka fung'uu.
 
Duh yaani ni kulishwa 'sumu' kwa kwenda mbele. Mara pweza, mara ubuyu, mara mihogo.

Hebu tuambieni kama na kwenye mashine za kusaga unga (wa ugali) kama wanaweka na 'sembe' kidogo.
 
Hivyo vi vyakula asilia sidhani kama vinachakachuliwa

Ila mkuu kwa story yako ya kuwa pweza inapikwa na Viagra kwa ajili ya kukuza soko la hiyo bidhaa kwa wateja kuaminishwa kuwa wakila pweza wanakuwa na nguvu sana...

Pia yawezekana na wale wadada wanaouza mihogo na nazi pia wakawa wanazipiga sindano zenye Viagrabidhaa zao pia kabla ya kuzipeleka sokoni.

Cha muhimu ni wote kujitahidi sana kuwa makini na hii vitu tunavyokula ovyo njiani na kumuomba Mungu atuepushie mabalaa
 
Hivi karibuni niliamua kufanya biashara ya Pweza hivyo nikaona ni vyema nifanye utafiti wa kina kabla ya kuanza,hii ni biashara nzuri hapa Dar es salaam na mtaji wake sio mkubwa pia inatoa fursa kwa vijana wetu.

Kilichonishtua ni kuwa daktari mmoja alinieleza kuwa Pweza huongeza protein muhimu mwilini na hawana uhusiano na kuongeza Nguvu za kiume wala si kichocheo cha body metabolism.

Hapo nikapata shauku ni kwa nini wateja wa hii kitu hupata Nguvu za ziada za mambo ya kikubwa pindi tu walapo hao pweza au kunywa mchuzi wake?

Jibu lilinistua sana maana hata mie ni mpenzi wa hawa Pweza na hata supu yake. Kumbe wauzaji huwa wananunua dawa ya kuongeza nguvu za kiume Viagra aina ya Sildenafil na kuchemshia Pweza kabla ya kuwakaanga.

Nikafanya uchunguzi kwa vijana kama wanne wanaofanya wanaofanya hii biashara maaeneo ya Ferry na Kariakoo wakathibitisha kuchanganya na Viagra.

Sikuishia hapo nikaenda kwenye Pharmacy moja na kudadisi ambapo Mfamisia mmama mtu mzima alibainisha kuwa ni kweli ana wateja wengi sana wa Viagra hio ambayo ni mahususi kwa kuchanganya na Chakula au Kinywaji.

Aisee nimekoma kula Pweza wa magengeni na sikuwa na hamu ya hio biashara nono. Nawashauri wapenzi wa Sea Foods hasa Pweza wanunue moja kwa moja Sokoni Ferry na waandae nyumbani vinginevyo with time Nguvu za kiume zitaathirika kwa kutumia Viagra bila kujua.

Nafunguka funguka.

Duuuuh wanaume kaz mnayoooo....
 
Uchunguzi wa ziada ni kuwa kiwango cha Viagra ni cha juu Sana kinachochanganywa na athari zake ni mbaya
 
Ase hii ni hatari sana, lkn mi ni mpenzi sana wa mihogo na nazi.Huku wakiweka nitagundua tu, hawawezi kwanza, wataanzaje?, ila nashauri Tfda wawe watu wa kunusa sehemu tofauti tofauti, tunavyokula ni vingi ase, vingine huwezi jua.
Mi nashangaa wafanyabiashara cjui wakoje,yaani watu wanaendekeza tamaa tu. Huku mama ntilie nao wanaweka amila, kuna mahali pia niliona wanaweka mafuta ya kupikia kwenye maziwa fresh, kku Wa kisasa wanachomwa sindano za...... N.k. yaani mijitu haina uzalendo kabisaa,shenzi taipu.
 
Asante kwa kutupa mbinu ya kibiashara tuliokuwa hatujui...

Kuanzia sasa hapa gengeni kwangu hata mchemsho wa maharage natupia kitu cha viagra...

Nani kasema maharage hayaongezi nguvu za kiume....shabashhhh!!!!

Umenichekesha sana ila usieke kwenye chai
 
Dah....hii sio nzuri kabisa haijakaa poa hii,nakula sana hawa wadudu laiti ningejua aisee..mkuu CHUNGA sana vipi kuhusu ngisi,au nao wanaweza wakawa wanafanyiwa huo mchezo...
 
Last edited by a moderator:
Dah....hii sio nzuri kabisa haijakaa poa hii,nakula sana hawa wadudu laiti ningejua aisee..mkuu CHUNGA sana vipi kuhusu ngisi,au nao wanaweza wakawa wanafanyiwa huo mchezo...

Imekula kwako
 
Last edited by a moderator:
Kama ndio hivyo,basi ulaji wa pweza na supu supu yake ni "Time Bomb".
 
Back
Top Bottom