Tahadhari: Mbowe usipobadilika, kuna siku utazomewa kama Masauni

Mimi niko na Mwenyekiti Mbowe leo kaonyesha UONGOZI tukiendekeza Emotions na Ego hakuna tukachokijenga sana tutabomoa.

Kumbukeni👉 NO HATE NO FEAR!! MWAMBA TUVUSHE🫡✌️✌️✌️
Absolutely, huo ndio uongozi...

Hawa watu hawajui kuwa CHADEMA ni chama cha siasa kinachoongozwa na sheria na kanuni za vyama vya siasa na zaidi sana katiba ya nchi...

Kwa nchi zetu hizi za ki - Afrika, watawala hutega vijimitego vidogodogo tu kwa vyama imara vinavyoi - challenge serikali na chama kilichopo madarakani Ili vikiingia mkenge tu, wapate uhalali wa kufutwa kwenye orodha ya vyama vya siasa...

Let's say, mfano ingetokea fujo pale, akafa au wakafa watu wengine pale, tunadhani Msajili wa vyama vya siasa Jaji Mutungi au Sisty Nyahozya angefanya nini kwa CHADEMA...?

Obviously, wangejenga hoja ya kufutwa CHADEMA hasahasa ikizingatiwa kuwa kwa Sasa Tundu Lissu na wenzake wamejifungia sehemu kuandaa kesi kumshitaki Susity Nyahozya (Msajili Msaidizi wa vyama vya siasa) na Awadhi Hajji (Kamishina wa Mafunzo naOperesheni za Jeshi la polisi) aliyeongoza Operesheni ya kuwapiga CHADEMA kule Mbeya siku chache zilizopita bila sababu na kinyume cha sheria....

Haya mambo ni AKILI KUMKICHWA....
 
Wakati wamarekani weusi walikuwa wanapigania kutambulika kama raia wengine wa Marekani, viongozi wao walikuwa ni Martin Luther King Junior na Malcolm X. Hawa approach zao zilikuwa tofauti. Ila ( kama nakumbuka vizuri) Malcolm X alisema umuhimu wake ulikuwa kuwaonyesha watawala kuwa kama watakataa kumuelewa Martin Luther King basi wajue itabidi waelewane nae. Mbowe na Lissu ni kama Martin Luther King na Malcolm X ingawa wale hawakuwahi kuwa chama kimoja.

Amandla...
 
Mimi niko na Mwenyekiti Mbowe leo kaonyesha UONGOZI tukiendekeza Emotions na Ego hakuna tukachokijenga sana tutabomoa.

Kumbukeni👉 NO HATE NO FEAR!! MWAMBA TUVUSHE🫡✌️✌️✌️
Endeleeni kujenga huku mnauawawa,, kumbe ninyi ni wajinga kama hao wanaowateka??? Huwezi kuthamini mtu asiyejali uhai wa mwenzake,,, MTU wa namna hiyo hata mbinguni hana Thamani,,, unless kama ninyi ni waastarabu mngekaa kimyaa kama sisi tuliokuwa nyumbani tukiendelea kumuomba MUNGU wetu atunusunuru na kutuondolea simanzi inayoletwa na hawa majangiri
 
Tuiweke TANZANIA kwanza Vyama vinakuja na kuondoka iko siku kutakuwa hakuna CCM wala CHADEMA lakini NCHI itakuwepo.
🇹🇿
 
 
We unafikiri consequences ya vurugu ingekua ni nini? We unafikiri vyombo vya ulinzi vingeruhusu waziri adhuriwe na wao wako pale? Si ndo wangeua watu kwa option ya kisheria waliyonayo ya kuua ili kulinda uhai? Mbowe siyo mjinga tatizo watu mnamihemko sana
 
Haa haa🤔🤔🤔

Kumbe wewe ulikuwa nyumbani tu ukipambana kwa MAOMBI na SALA kwa Mungu...?

That was good for you....

Lakini cha ajabu unawalaumu na kututaka sisi wenzio tuliokwenda msibani tuanzishe fujo, tupigane na ikibidi tuumizane na kuuana, au siyo..?

Wewe huko nyumbani ulikuwa unamwomba MUNGU YUPI? Mungu wa fujo na vurugu shetani au Mungu wa amani na upendo...?

Hapa umeonesha ulivyo na fikra dhaifu kabisa zisizo na mtiririko wa kimantiki....!

Jisome tena kisha Rudi niambie kama nimekosea kuku - describe....
 
WAKULAUMIWA NI UMMA WA WATANZANIA, WALIORUHUSU WATESI KUFANYA UOVU BILA HOFU

View: https://m.youtube.com/watch?v=9_sx1mUoxjEFreeman Mbowe, Tundu Lissu, John Mnyika, SUGU, Dr. Slaa, Maria Sarungi na wengine wamejotolea hadi wanaishi kimagutu gutu lakini watanzania hatuwezib kufanya maandamano kama Kenya, Bangladesh, Sri Lanka n.k serikali iliyopo madarakani ikaheshimu utawala wa sheria, haki, katiba na mihimili huru ...


Hakuna serikali inaweza kutesa, kutunga sheria mbovu, kuteka raia, kupoteza watu na uovu mwingine wote bila sisi mamilioni ya raia kuwapa nguvu hiyo ....


Anaongeza hakuna vyombo vya dola na serikali iliyo madarakani inaweza kuwashinda raia wake wakiamka kulinda kura, chaguzi au kukataa kwa wingi wao kutekwa, kunyanyaswa, kupuuzwa na kuonewa ...

Anafafanua nguvu hiyo ya maovu serikali huipata vipi ..... na mwisho wa siku ni raia mamilioni wa Tanzania wanaotakiwa kulaumiwa na siyo chama tawala, serikali wala vyombo vyake vya dola maana .... nguvu hiyo wamepewa na mamilioni ya wananchi.

Pale mamilioni ya wananchi watapokataa ndiyo itakuwa mwisho wa maovu yote tunayolia kuwa bunge limetekwa, uchaguzi umeporwa, watekaji wanaendesha operesheni bila wasiwasi, matumizi ya anasa ya serikali ...


Mbinu pekee ya kukomesha haya maovu yote ni nguvu ya umma kukataa kwa kushukua hatua zifuatazo ....
 
Nimekuelewa
 
Mbowe ana busara. Kama ni madhila kashakutana nayo ya kutosha kuliko wanaCHADEMA walio wengi. Wewe Salary Slip nje ya JF ni mtoto mzuri tu kama Lilian au Vero. Huna ushujaa wowote.
 
 
Mbowe ni kiongozi shupavu!
Alichokifanya leo kimezidi kumtofautisha yeye na wakurupukaji wengi!
Sasa mngeachwa mumshambulie Masauni ndo mngemaliza tatizo la utekaji, utesaji na uuaji?
Acheni jazba. Rudini kwenye drawing board!
 
Mkuu mashabiki huwa hawaingii uwanjani wao nafasi yao ni nje ya uwanja ndiko wanakotambia.
 
Mbowe ana busara. Kama ni madhila kashakutana nayo ya kutosha kuliko wanaCHADEMA walio wengi. Wewe Salary Slip nje ya JF ni mtoto mzuri tu kama Lilian au Vero. Huna ushujaa wowote.
Mkuu wengine mashabiki na siku zote mashabiki huwa hawaingii uwanjani kucheza, nafasi yao ni kushangilia na kupiga kelele nje ya uwanja.
 
Nafikiri Mbowe alifanya vile kwa heshima ya Marehemu Mzee wetu Kibao, kwani kama zingezuka vurugu kubwa pale vyombo vyote vya habari kwa maelekezo ya dola vingeandika Chadema wavuruga mazishi ya kada wao.
 
Nafikiri Mbowe alifanya vile kwa heshima ya Marehemu Mzee wetu Kibao, kwani kama zingezuka vurugu kubwa pale vyombo vyote vya habari kwa maelekezo ya dola vingeandika Chadema wavuruga mazishi ya kada wao.
Sasa Masauni kafuata nini pale wakati wanaohusika ni Watu wake kafuata nini pale yeye si ndio Waziri wa Mambo ya ndani, taarifa imetoka siku Ile kua Mzee yule Marehemu wamemchukua Polisi alichukua hatua gani anafuata nini msibani siku nyingine watamsukumia kaburini wamfukie asiende kwenye misiba inayoonekana km amehusika watu hawana simile
 
Wanao ona mbowe kakosea, hawana jicho la kiuongozi au hawajawai kua viongozi any where.

Kauli moja tu ya kiongozi, Mtaa unaweza chafuka na watu kuuwawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…