Tahadhari mnaopenda kuchukua wasichana warembo

Tahadhari mnaopenda kuchukua wasichana warembo

Kuna siku nilikua natoka mitaa ya kinyerezi ndanindani
Kwenda barabarani kutafuta usafiri.
Ilikuwa ni usiku karibia sa tatu hivi na nilikua nategemea kuondoka
na watu fulani ikawa tofauti.
Mimi ni muoga sana kutembea usiku nikamuona mkaka anapita
nikamsimamisha tuongozane.
Njiani akawa ananisimulia kua kuna simba,mbele kidogo
akanitongoza nikajua anajisumbua mbele kila mtu ataenda kivyake
eh! Si akataka tumalizane palepale..
Sijui lilitoka wapi lile wazo,nikamjibu kwa upole tu kuwa
mimi ni Jini na ningependa kwenda nae kwangu tukamalizane huko.
Alishtuka akaniangalia miguu nikamwambia "najua mawazo yako
unataka kuona kwato zangu"
Kaka aliomba msamaha nikajifanya simsikii hadi tukafika barabarani.
Wanaume huo ujasiri na tamaa viwe na mipaka.

Hehehehhehe.....itabidi niibe huu ujuzi siku nikikutana na mtu usiku alafu akaanza kunisumbua!!
 
Hadithi nyingi nimesikia kutoka kwa watu ambao wamesia hizo hadithi kutoka kwa watu wengine!! hata sikumoja sijapata mtu aliyekutwa na tukio....mimi naona hizi ni kama zile hadithi za mababu zetu kujaribu kutuonya tuwe na maadili mazuri!! it works...wanaume wanaogopa
 
Hehehehhehe.....itabidi niibe huu ujuzi siku nikikutana na mtu usiku alafu akaanza kunisumbua!!

Hahahahahaha unataka kujifanya jini siyo LOL! Ndiyo hapa utajuta kuzaliwa! Unajifanya jini jamaa anakwambia twende tu! Kijasho chembamba kitakutoka!

Aluta continua, dunia imejaa hatari kila mahali, hakuna kuacha ikikukumba hiyo ni ajali yako. Utakwepa jini la mapenzi utakutana na jini omba omba, si mnakumbuka kile kisa cha Salender Bridge!

Hivi machangudoa majini wapo pia?
 
Good thing I dont believe in majini!
 
Mungu walinde tu, hawa kaka, baba, babu, na watoto wa kiume.
Ikiwezekana waokoe tu, na uwalinde kwa ulinzi wa kipekee kabisa.
Dah!!!!
Mbona umewasahau wadada na akina mama? Kuna majini ya kiume pia!
 
Binafsi I dont support tabia ya mwanaume kujiokotea msichana ambaye hamjui na kwenda kulala naye.Ila najua wapo watu wa aina hiyo na ndio hao yanawakuta,lakini kwa kuwasaidia tu ndugu zanguni endapo utakutana na jini ni rahisi sana kumfahamu kabla hata hujaendelea na mambo yako.Mtazame machoni,na ukiona hana "eye blinking" basi huyo sio binadamu wa kawaida na umuepuke.Kwa kuwa binadamu wote akikutazama lazima macho yanafunga(kupiga kope)tofauti na majini ambayo yenyewe huwa hayana hali hiyo na yanatazama moja kwa moja,na likishakushtukia unalitazama machoni huwa yanajitahidi kukwepesha macho hivyo kwa njia hiyo itakuwia rahisi sana kuligundua,nawatakia kila la kheri katika harakati zenu watafutaji wa one night stand kwani najua mpo humu.

He! Paka una mautalaamu na mambo ya majini kumbe
 
Dr. wa Ukweli, mimi naomba kuuliza, vipi imeshakutokea nini??? Naona kama una details za kutosha...

mifano hi ipo ila siyo mimi kuna my friend naishi nae ilimtokea maeneo ya posta, alikuwa anatokea IFM akiwa anadrive kwa mbele akaona bint mzuri amesimama pale karibu na jenfo la kitegauchumi majira ya saa 6 usiku alipo mkaribia akasimamisha gari ili amsemeshe aondoke nae, kabla hajamsemesha ghafla akamwona yupo ndani ya gari siti ya nyuma wakati milango yote ipo locked hajui kapita wap........ akawa kama kachanganyikiwa vile alichofanya ni kukimbiza gari hadi kariakoo pake sokoni penye watu wengi akasimama akashuka akamwacha mrembo/jini knye gari akakimbia kwa miguu hadi magomeni. asubuh yake akatuma mtu mwingne akachukue ile gari pale kkoo bahati nzuri akaikuta ipo salama.
 
Hehehehhehe.....itabidi niibe huu ujuzi siku nikikutana na mtu usiku alafu akaanza kunisumbua!!

ukikutana na mwanaume aliyepinda atakuambia hata mimi ni jini tumekutana twende tu tukamalizane.
 
DU HIII NI HATARI SANA KAMA NI KWELI JAMNI MANA SISI MIDUME HUA TUNAPAPATIKA NA WALE WAZURI!DU YASIJE KUNIKUTA MIE:usa2:
 
wewe unatuombea tukutane na majini? mbaya wewe

Sio mbaya, hata mimi namuunga mguu. Tunawapenda wa kwetu wa ukweli, tunataka wabaki na sisi, sisi, ndo maana tunataka wakumbane nayo hili liwe fundisho watulie, tulee watoto vizuri.
 
Wanaume mnaopenda kuchukua wasichana warembo hususani kama umekutana nae siku moja na kumtaka kimapenzi ikibidi kusex nae siku hiyo hiyo ni hatari sana.
mtaani sasa hivi majini wanawake yamejaa sana, utaona ni mrembo kama malaika kumbe jini utamdu muda si mrefu utapotea au utapata madhara

hakikisha msichana unaetaka kuwa nae kimahusiano unamjua vizuri eithe anaishi wap, anafanya kazi wap, marafiki zake ni nani, alisoma wapi na ufanye uchunguzi wa kina kabla hajaparamia majini!

majini watu ni wengi wanapita mabaa usiku au njiani wamesimama mchana/usiku wanarembua kweli kweli tuwe makini kwa hilo nina mifano hai wameonekana.

Kwenye mawindo yangu wakati wote nina kamfupa ka kitimoto kwenye walet yangu. Majini hayana nafasi kabisa kabisa na Mchungaji
 
mifano hi ipo ila siyo mimi kuna my friend naishi nae ilimtokea maeneo ya posta, alikuwa anatokea IFM akiwa anadrive kwa mbele akaona bint mzuri amesimama pale karibu na jenfo la kitegauchumi majira ya saa 6 usiku alipo mkaribia akasimamisha gari ili amsemeshe aondoke nae, kabla hajamsemesha ghafla akamwona yupo ndani ya gari siti ya nyuma wakati milango yote ipo locked hajui kapita wap........ akawa kama kachanganyikiwa vile alichofanya ni kukimbiza gari hadi kariakoo pake sokoni penye watu wengi akasimama akashuka akamwacha mrembo/jini knye gari akakimbia kwa miguu hadi magomeni. asubuh yake akatuma mtu mwingne akachukue ile gari pale kkoo bahati nzuri akaikuta ipo salama.

Dah!!!!!!!!! Hii kali. Na hadithi ikaishia hivyo tu. Jini alijamsumbua tena, mpe pole. Nadhani atakuwa amepata somo zuri sana. Na siku nyingine hasitamani, tamani.
 
Sio mbaya, hata mimi namuunga mguu. Tunawapenda wa kwetu wa ukweli, tunataka wabaki na sisi, sisi, ndo maana tunataka wakumbane nayo hili liwe fundisho watulie, tulee watoto vizuri.

sasa ukimwombea akutane na jini,...... majini mengine yanamapenza moto moto ndio hatarudi tena badae yanamchukua moja kwa moja bora achukue malaya/changudoa kuliko akutane na jini
 
sasa ukimwombea akutane na jini,...... majini mengine yanamapenza moto moto ndio hatarudi tena badae yanamchukua moja kwa moja bora achukue malaya/changudoa kuliko akutane na jini

Loh!!!!!!!! Dokta wa ukweli, mbona unaniogopesha. Pole pole bwana.
 
Back
Top Bottom