Dr Lizzy
Platinum Member
- May 25, 2009
- 31,009
- 60,629
Kuna siku nilikua natoka mitaa ya kinyerezi ndanindani
Kwenda barabarani kutafuta usafiri.
Ilikuwa ni usiku karibia sa tatu hivi na nilikua nategemea kuondoka
na watu fulani ikawa tofauti.
Mimi ni muoga sana kutembea usiku nikamuona mkaka anapita
nikamsimamisha tuongozane.
Njiani akawa ananisimulia kua kuna simba,mbele kidogo
akanitongoza nikajua anajisumbua mbele kila mtu ataenda kivyake
eh! Si akataka tumalizane palepale..
Sijui lilitoka wapi lile wazo,nikamjibu kwa upole tu kuwa
mimi ni Jini na ningependa kwenda nae kwangu tukamalizane huko.
Alishtuka akaniangalia miguu nikamwambia "najua mawazo yako
unataka kuona kwato zangu"
Kaka aliomba msamaha nikajifanya simsikii hadi tukafika barabarani.
Wanaume huo ujasiri na tamaa viwe na mipaka.
Hehehehhehe.....itabidi niibe huu ujuzi siku nikikutana na mtu usiku alafu akaanza kunisumbua!!