TAHADHARI: Orodha ya TBS ya bidhaa 48 zisizotakiwa kuonekana sokoni...

TAHADHARI: Orodha ya TBS ya bidhaa 48 zisizotakiwa kuonekana sokoni...

Watanzania tukionywa hatusikii. Bidhaa hizohizo zikiachwa na kuleta madhara hapo baadae tunalalamika kwamba chombo hiki hakifanyi kazi. Daa!
 
Mimi nafkri hapo ndipo wanapo dhihirisha mfumo na taasisi goigoi wasiojua mamlaka na uwezo walio nao katika kutekeleza majukumu yao. Nilitarajia kuwa baada ya kubaini haya mapungufu katika bidha mbalimbali hatua ya kwanza ilikua nikufunga viwanda vyote vinavyozalisha au makumpuni yanayoingiza hizo bidhaa. Hiyo ingenda sambamba na kutoa taarifa kwa wanachi wasitumie hizo bidhaa. Pili wahusika wote kuchukuliwa sheri na kutoza faini kwa kusababishia madhara kwa wananchi.
Sasa wao wanaweka orodha ndefu hapa itasaidia nini kama uzalishaji unaendelea na bidhaa zinaendelea kupelekwa mitaani. Pia utamaduni wa wananchi wetu nivigumu sana kufutilia au kwenda kununua hizo bidha ukiwa na list ya hivyo vitu ili uwezekujiridhisha kama ni bidhaa halali au feki.
Serikali goigoi inapalekea taasisi goigoi. Hapo mnapanua wigo wakutafuta rushwa tu maana hakuna hatua yoyote mtaitoa kuwa fundisho nakujenga standerd za biashara.
 
LOL... Hadi Pikipiki za CHINA inaonyesha tunabeba takataka NYINGI toka CHINA
Khaa!!! usikurupuke wewe. Tuliza akili usome uelewe vizuri. Taarifa inasema kuwa muda wamatumizi ya nembo ndiyo umeisha na siyo kwamba bidhaa siyo bora. KWA KIFUPI HAWAJALIPIA KODI YA KUTUMIA NEMBO YA TBS. Mbona kuna bidhaa nyingi feki na zina nembo?? Fungua akili yako :bored:
 
Kilicho nishangaza ni kusikia eti "hawaleti" bidhaa zao! Kumbe ni mpaka walete! Kwa hivyo mtu au kampuni ikitengeneza bidhaa 100 ikapeleka ikakaguliwa na itengeneze milioni ikapeleka sokoni ni sawa? Mimi nilidhani mnakagua bidhaa moja baada ya nyingine kabla haijafikia umma kwa matumzi! Au hata kukagua zilizoko sokoni ghafla bila kutoa taarifa ingekuwa afadhali!
Mpaka muwatangazie? Kweli nia ya kutangaza ni ili walete hela kwenye ofisi zenu.
 
tuachieni hizohizo fake tuzitumie,kwa maana tumeshazoea na ndio tunazozipenda hizo.
 
ningekua na uwezo ningevunja tbs then niunde shirika la ubora na si viwango tena.
 
Wanatafuta ulaji hawa jamaa hawana jipya walikuwa wapi siku zote mpaka watu waathirike ndo waje kwa mbwembwe
 
JUL 30, 2013
Imenukuliwa kutoka kwenye gazeti la MWANANCHI-- Shirika la Viwango (TBS) limetangaza orodha ya bidhaa 48 ambazo hazitakiwi kuwepo sokoni kutokana na muda wa kuitumia nembo ya kampuni hiyo katika bidhaa zao kumalizika na wahusika kushindwa kuwasilisha bidhaa zao kwa ajili ya uhakiki kabla ya kuruhusiwa tena.Hatua hiyo ya TBS inatokana na watengenezaji wa bidhaa hizo ambazo awali zilithibitishwa na TBS na kuruhusiwa kutumia nembo yao hiyo ya ubora kumalizika na wahusika kushindwa kuwasiliana na shirika hilo kwa ajili ya uhakiki wa bidhaa zao hiz😵fisa Uhusiano wa TBS, Rhoida Andusamile aliliambia Mwananchi kuwa bidhaa hizo kuanzia hivi sasa hazitakiwi kuonekana sokoni na msako utaanza wakati wowote kuziondoa na zile ambazo zitakamatwa wahusika watachukuliwa hatua kali za kisheria.“Tumetoa tangazo lakini kabla ya hapo tuliwapa muda wawe wameleta bidhaa zao kwa ajili ya kuhakikiwa kabla ya kuruhusiwa kuendelea kutumia nembo yetu,akini wamekaidi ndio maana tumewatangazia kama utaratibu unavyoagiza” alisema Rhoida.Bidhaa ziliazoainisha katika tangazo hilo ni pamoja na
majina ya watengenezaji /wasambazaji katika mabano ni pamoja na karatasi laini ‘tissue’ za Alawi Supplies ya Zanzibar, Milk Marie Biscut za Britania, Maji ya Great Zone, Mishipi na nyavu za kuvulia samaki za Imara Fishnet, maji ya Raha na fulana za Kibo Trade.Bidhaa zingine ni matofali ya GM Gross, taulo za watoto za Hengan Sanitary, baadhi ya rangi za Chui, beteri za Dry Cell, magodoro ya Jumbo foam, sabuni za Mbasira Investment ya Shinyanga, mifuko ya plastiki ya Centaza na mafuta ya kupikia ya Sun Flower Seed (Sun Shine) na korosho zinazosambazwa na Frabho Enterprises.Pia taulo za wanawake za Sythentic Detergent (ARIEAL) za Procter&Gambler, mifuko ya B-Twill Jute na A-Twill, mifuko ya plastiki ya Tropical, mafuta ya kupikia ya Sun Flower ya A TO Z Oil Mills, Korosho za Munawar ya Mbeya, Sabuni za kunawia za Brite Chemicals, pipi, lawalawa, mipira ya kutafuna ya rangi mbili.Vilainisha vya injini (Saud Oil) za Star Composed, betri za 777 kutoka China, maji ya kunywa ya Shia yanayotengenezwa na Siha Beverage, mtindi wa Morani Dairy ya Tanga, pikipiki za Star Shineray, vigae vya Mbezi, sabuni ya Liquid Detergent, mbao zilizotiwa dawa za Mombo, Jam iliyochanganywa ya Les Group ya Musoma.Orodha hiyo pia inataja Jusi za nanasi za Unnat Fountain ya Morogoro, Maji Uluguru, springi za magari za kampuni ya TASIA, Gypsum zinazotengenezwa na Tanzania Gypsum ya Dar es Salaam, Maji ya Uzima, magodoro ya Plyfoam,Mvinyo wa nanasi wa Kivumbui ya Arusha na mabati ya RD Roofing & Wire Product.Bidhaa zingine ni unga wa sembe wa Kweniml ya Machame Kilimanjaro, boriti za Ravji Manufacturing, mafuta ya breki za magari ya Automotive Packed ya Dar es Salaam, maJi ya kunywa ya AAMFA, pikipiki za Foshan Fost za China na mvinyo wa matunda wa Victoria Food Product ya Mara pia Jibini, mtindi na maziwa ya Kyaka Milk Processing , Sabuni za kufulia za Jamii za Kampuni ya Mbasira ya Shinyanga.
kitu cha msingi hapa isitumike janja janja ili kuturubuni wananch fanyeni kweli ili kutunusuru na majanga
 
Mwenye kosa n muuzaj au mtengenezaj na msambazaj? Hawa TBS Wanatutangazia il iweje badala ya kuwaface wahucka, mwenye stock yake dukan atafidiwa na nan waache kutia wafanyabiashaja jamba jamba bhana
Mkuu usijali tu wafanyabiashara,jali pia na afya za wananchi mkuu.

Unakuwa kama wale watu wenye malori halafu likipata ajali kabla ya kuulizia hali ya dereva wanaulizia hali ya gari.
 
Kila kitu mnakosoa tu, TBS wasipotahadharisha pia mngelalamika. Wabongo huwa nawashangaa sana!
 
Hivi kitu gani kifanyike ili mridhike kila kinachofanywa hata kama kizuri lazima mseme vibaya,mbona mnatumika vibaya kuzidi co**m
Kutangaza tu kuwa ni bidhaa feki haitoshi, bidhaa hizo zimejaa madukani, na kingine kuna bidhaa nyingine feki zaidi hazipo katika orodha.
 
Kita kiti tunachotumia ni fake..sasa tutaponea wapi?
 
Hakuna wababaishaji kama TBS nilifikiri Ekelege akiondoka ubabaishaji utaisha kumbe ndo kwanza unaongezeka
Ubabaishaji umeshaingia kwenye mfumo, na umeshamiri sana sasa hivi. kwa hiyo mabadiliko ya viongozi siyo rahisi kubadili mfumo mzima. inataka jitihada pana zaidi. lakini pia tatizo kubwa sana la TBS ni kutoweza kusimamia hivyo viwango vyake. sawa mtu anapeleka sample yake inapimwa na kuidhinishwa kwamba amekidhi viwango. katika muda ambao anatumia hiyo nembo ya TBS, hao TBS wana uhakika gani kwamba anaendelea kutumia standard ile ile? maana inawezekana kabisa mwezi huu akatengeneza kwa standard lakini mwezi ujao akapunguza ubora na bado akaendelea kutumia nembo ya TBS! kinachotakiwa ni TBS yenyewe au kwa kushirikiana na wadau wengine, iwe na uwezo wa kufanya random sampling mara kwa mara ili kudhibiti ubora wa hizo bidhaa, kitu ambacho kwa sasa hakipo.
 
Naichukia sana TBS kwani imechangia sana watanzania kufa kwa bidhaa feki.
 
hapa TBS wanahitaji kutoa elimu kwanza,
manake hivi vigae tangu mwaka 1991 kabla sijaja mjini vilikuwa vinatengenezwa na kuuzwa...vimeanza kuwa sub-standard lini?Je ni muda gani mtu atajua kuwa bidhaa fulani imeshashuka kiwango kama ilikuwa inafikia viwango hapo kabla?!?

hawa TBS wameishiwa sera,mbona hawasemi tv na radio za Sony na Samsung?mazero tu!wanawasingizia watz,na hapa haimaanishi sio bora,ni kwa sababu hawajawakatia wamekasirika na kuwazushia mambo
 
Back
Top Bottom