TAHADHARI: Orodha ya TBS ya bidhaa 48 zisizotakiwa kuonekana sokoni...

TAHADHARI: Orodha ya TBS ya bidhaa 48 zisizotakiwa kuonekana sokoni...

sasa hizi bidhaa wananchi si wananunua bila kujua.. Kwa sababu wananchi wasionunua magazeti si wanauziwa? Serikali bana!

kwahiyo unashauri je? Wapite nyumba hadi nyumba?
 
Na bado utavikuta sokoni vinauzwa kama kawaida. Wafanya biashara wa Bongo noma. TBS lakini nao naona wameamua kusafisha madudu yao. Mashine wanazotumia kwanza kuhakiki viwango nyingi ni outdated.


Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Wamewatangazia ili wakazifiche upite msako blah blah halafu wakauziwe watu wa vijijini kwa bei ya promosheni!!!!!!

Hivi kweli unamtangazia muhalifu kuwa ntakutafuta jumatatu ijayo??!!!!

Wonderland

Labda washakula chao na hapo wanafanya kupotezea wajinga tu!
 
hao waliotajwa hapo ni vidagaa kwani tunaona kuwa wanamakampuni makubwa ndo hasa wanaotumia mwanya hoiu kupiga changa la macho kwa kuchakachua chini ya kivuli cha kampuni lao kubwa.
 
Wamewatangazia ili wakazifiche upite msako blah blah halafu wakauziwe watu wa vijijini kwa bei ya promosheni!!!!!!

Hivi kweli unamtangazia muhalifu kuwa ntakutafuta jumatatu ijayo??!!!!

Wonderland

....'Maandalizi' ya Idd hayo, Mkuu Olesaidimu!🙂
 
Kwa vile ukaguzi hufanywa na TBS kubandika mihuri yao kabla ya bidhaa kusambazwa, imekuwaje hususani kwa viwanda vya ndani wakaruhusu bidhaa duni zisambazwe kwa walaji af ndo wazuie?!
 
JUL 30, 2013

...hazitakiwi kuonekana sokoni na msako utaanza wakati wowote kuziondoa na zile ambazo zitakamatwa wahusika watachukuliwa hatua kali za kisheria.


“Tumetoa tangazo lakini kabla ya hapo tuliwapa muda
wawe wameleta bidhaa zao kwa ajili ya kuhakikiwa kabla ya kuruhusiwa kuendelea kutumia nembo yetu,akini wamekaidi ndio maana tumewatangazia kama utaratibu unavyoagiza” alisema Rhoida.


Ofisa Uhusiano wa TBS, Rhoida Andusamile aliliambia Mwananchi kuwa bidhaa hizo kuanzia hivi sasa


Kwenye red wana maana gani, kwani mfanyabiashara wa mtaani yeye atajuaje kama watengenezaji hawajapeleka tena bidhaa kupimwa? Wakifanya msako mitaani ili kuondoa bidhaa hizo na kumuacha mtengenezaji/agent wa bidhaa hiyo hawaoni kama hawatatakuwa wanawatendea haki mfanyabiashara (Whole/Retail Traders) huyo?

Je, kama mfanyabiashara alinunua mzigo mkubwa hapo kabla na biashara inatoka polepole, mzigo wake utaondolewa sokoni kwa sababu ya mzalishaji hajaenda ku-renew nembo ya TBS? Vyombo vya serikali ni vidhaifu sana vinakimbilia kumuadhibu muuzaji mganga njaa na vinaogopa kuwakabili wazalishaji moja kwa moja!

kwenye
blue ni nani anawajibu wa kuomba uthibitisho TBS, je ni mfanyabiashara au mzalishaji? Inatakiwa mzalishaji ndiye afuatwe na afungiwe uzalishaji na siyo muuzaji! Kama watakwenda kuziondoa bidhaa hizo madukani basi TBS watakuwa wanatumia vichwa kufuga nywele tu na si kufikiri.
 
TBS hawana mandate ya kupima ubora wa mafuta ya alizeti na korosho. Wenye mandate hiyo ni TFDA, tunasubiri tamko la TFDA kuhusu ubora wa mafuta ya alizeti na korosho. Katika hili TBS wanabaki na jukumu la kukagua ubora wa vifungashio (packaging) tu wala siyo ubora wa mafuta au korosho zenyewe.

Afteral TBS imeshakosa credibility ya kusimamia ubora wa bidhaa za viwandani hapa nchini baada ya kashfa kubwa kubwa toka enzi ya Mwakyembe na mbaya zaidi kashfa ya utapeli chini ya Charles Ikelege. Inahitajika taasisi nyingine yenye credibility lakini si TBS hii. Vinginevyo taasisi hii ifanyiwe overhaul ya nguvu ili ipate kuaminiwa tena na watanzania.
 
Kwa kifupi haya mashirika/taasisi za serikali zimepoteza sifa muhimu ya kutumika kwa niaba ya wananchi
mfano;

POLISI:-
wanashiriki ujambazi, kutupiga mabomu, kutubambikia makesi mpaka ya kigaidi BADALA YA KUTULINDA KWA SILAHA TULIZOWAPA, WAMETUACHA SOLEMBA!!!!!

TUME YA UCHAGUZI:-
tukishajiandikisha kuwa wapiga kura wanafanya jitihada kutuhujumu tusipige kura (visingizio kibao, mara uhakiki wa wapigakura, mara ukipoteza kitambulisho cha kupigia kura form namba. ...... hawataki itumike ili upige kura) "HUJUMA DHIDI YA JAMII" siku hizi wanakuja na matamko kabisaaaaa yanayopingana na sheria ya uchaguzi, eti ukipiga kura shuruti uondoke uende nyumbani, USIKAE ZILE MITA MIA MOJA zinazoruhusiwa kisheria KUSUBIRIA MATOKEO, (lengo waitende kura yako sawa sawa na mapenzi yao)

MAHAKAMA:-
huku nisiongelee sana unaweza kutana na Jaji, kwa maamuzi yake tu ukajua kuwa pengine ana cheti tu cha sheria, si diploma wala kadigirii

TBC:-
imekuwa TBCccm

BUNGE:-
Linalevya siku hizi, mibunge haina uwezo kabisaaaaaaaa wa kuitetea jamii! Mfano, imepitisha kodi ya "laini" za simu, baada ya miezi miwili ikirudishiwa hoja ili waifute hiyo hoja itaifuta kwa kishindo NDIYOOOOOOO (yaani haikujua athari za walichokuwa wanapitisha kwa mbwembwe miezi miwili iliyopita?) Ndiyo maana hata waziri mkuu akiagiza polisi kupiga wananchi mibunge haini kosa hapo.

TBS & TFDA:-
Wanasubiri athari ijitokeze kwenye jamii kutokana na ubovu wa bidhaa ndio wakurupuke na matamko yao ya kupiga marufuku, kuonya, taarifa kwa umma...... yaani kizunguzungu.

MAGOGONI:-
"wauza unga nawafahamu" (kama kichekesho vile)

MAPENDEKEZO:
tembo,faru na twiga wanatakiwa kujilinda!!!!!!
kila mwqnanchi awe na maabara apime ubora wa bidhaa kabla ya kuinunua/kuitumia.

kila mpiga kura ahakikishe analinda haki yake ya kupiga kura, na analinda kura yake anapoipiga.

........
........
.........
.........
 
Hawa hawajalipa ada ya kutumia nembo. Zinatafutwa fedha tuu kwa ajili ya uendeshaji wa tbs.
 
sasa hizi bidhaa wananchi si wananunua bila kujua.. Kwa sababu wananchi wasionunua magazeti si wanauziwa? Serikali bana!

"... bidhaa 48 ambazo hazitakiwi kuwepo sokoni kutokana na muda wa kuitumia nembo ya kampuni hiyo katika bidhaa zao kumalizika na wahusika kushindwa kuwasilisha bidhaa zao kwa ajili ya uhakiki kabla ya kuruhusiwa tena." ...

BIDHAA HAZINA SHIDA TATIZO TBS WANATAKA WALIPWE FEES ZA NEMBO SASA MATANGAZO YAO YAMEKAA KIFITINA AS IF BIDHAA HAZIFAI. SASA IKIWA WAMEWEKA JINA LA BIDHAA YA KAMPUNI KIMAKOSA JE!? WAPO TAYARI KULIPA FIDIA KWA UPOTOSHAJI!?
 
mbona hamna product ya electronic hata moja ambazo kwa kweli ndio nyingi feki kuanzia simu, extension cables, pasi nk kwa mfano nununa pasi ya hawa jamaa wanaotembeza mtaan ukifika home ukiiwasha tu kuna mawili either Main circuit breaker ita trip au ile pasi moto wa kunyoshea nguo hautatosha kabisa!!!
 
Sidhani kama Serikali kupitia TRA iko makini kwa sababu hapa ukiangalia tatizo lipo kati ya Watengenezaji wa bidhaa hizo na TRA na si kati ya serikali na wenye maduka ya jumla ambao wanawauzia retailers na pengine consumers. Serikali haioni inatengeneza mgogoro mwingine usio wa lazima? Wenye maduka kosa gani hapa? Serikali isijifanye jinga.
 
Wananchi wasiwe na wasiwasi, swala hapa sio ubora wa bidhaa, ila ni kuwa bidhaa zilizotajwa zimekuwa kwenye soko kwa njia halali na vibali cha TBS, sasa vibali vimefika mwisho, Vinatakiwa kulipiwa tena , ila inaonyesha bado wanatumia vibali vya TBS ambavyo havijalipiwa.
 
Back
Top Bottom