TAHADHARI: Orodha ya TBS ya bidhaa 48 zisizotakiwa kuonekana sokoni...

Watanzania tukionywa hatusikii. Bidhaa hizohizo zikiachwa na kuleta madhara hapo baadae tunalalamika kwamba chombo hiki hakifanyi kazi. Daa!
 
Mimi nafkri hapo ndipo wanapo dhihirisha mfumo na taasisi goigoi wasiojua mamlaka na uwezo walio nao katika kutekeleza majukumu yao. Nilitarajia kuwa baada ya kubaini haya mapungufu katika bidha mbalimbali hatua ya kwanza ilikua nikufunga viwanda vyote vinavyozalisha au makumpuni yanayoingiza hizo bidhaa. Hiyo ingenda sambamba na kutoa taarifa kwa wanachi wasitumie hizo bidhaa. Pili wahusika wote kuchukuliwa sheri na kutoza faini kwa kusababishia madhara kwa wananchi.
Sasa wao wanaweka orodha ndefu hapa itasaidia nini kama uzalishaji unaendelea na bidhaa zinaendelea kupelekwa mitaani. Pia utamaduni wa wananchi wetu nivigumu sana kufutilia au kwenda kununua hizo bidha ukiwa na list ya hivyo vitu ili uwezekujiridhisha kama ni bidhaa halali au feki.
Serikali goigoi inapalekea taasisi goigoi. Hapo mnapanua wigo wakutafuta rushwa tu maana hakuna hatua yoyote mtaitoa kuwa fundisho nakujenga standerd za biashara.
 
LOL... Hadi Pikipiki za CHINA inaonyesha tunabeba takataka NYINGI toka CHINA
Khaa!!! usikurupuke wewe. Tuliza akili usome uelewe vizuri. Taarifa inasema kuwa muda wamatumizi ya nembo ndiyo umeisha na siyo kwamba bidhaa siyo bora. KWA KIFUPI HAWAJALIPIA KODI YA KUTUMIA NEMBO YA TBS. Mbona kuna bidhaa nyingi feki na zina nembo?? Fungua akili yako :bored:
 
Kilicho nishangaza ni kusikia eti "hawaleti" bidhaa zao! Kumbe ni mpaka walete! Kwa hivyo mtu au kampuni ikitengeneza bidhaa 100 ikapeleka ikakaguliwa na itengeneze milioni ikapeleka sokoni ni sawa? Mimi nilidhani mnakagua bidhaa moja baada ya nyingine kabla haijafikia umma kwa matumzi! Au hata kukagua zilizoko sokoni ghafla bila kutoa taarifa ingekuwa afadhali!
Mpaka muwatangazie? Kweli nia ya kutangaza ni ili walete hela kwenye ofisi zenu.
 
tuachieni hizohizo fake tuzitumie,kwa maana tumeshazoea na ndio tunazozipenda hizo.
 
ningekua na uwezo ningevunja tbs then niunde shirika la ubora na si viwango tena.
 
Wanatafuta ulaji hawa jamaa hawana jipya walikuwa wapi siku zote mpaka watu waathirike ndo waje kwa mbwembwe
 
kitu cha msingi hapa isitumike janja janja ili kuturubuni wananch fanyeni kweli ili kutunusuru na majanga
 
Mwenye kosa n muuzaj au mtengenezaj na msambazaj? Hawa TBS Wanatutangazia il iweje badala ya kuwaface wahucka, mwenye stock yake dukan atafidiwa na nan waache kutia wafanyabiashaja jamba jamba bhana
Mkuu usijali tu wafanyabiashara,jali pia na afya za wananchi mkuu.

Unakuwa kama wale watu wenye malori halafu likipata ajali kabla ya kuulizia hali ya dereva wanaulizia hali ya gari.
 
Kila kitu mnakosoa tu, TBS wasipotahadharisha pia mngelalamika. Wabongo huwa nawashangaa sana!
 
Hivi kitu gani kifanyike ili mridhike kila kinachofanywa hata kama kizuri lazima mseme vibaya,mbona mnatumika vibaya kuzidi co**m
Kutangaza tu kuwa ni bidhaa feki haitoshi, bidhaa hizo zimejaa madukani, na kingine kuna bidhaa nyingine feki zaidi hazipo katika orodha.
 
Kita kiti tunachotumia ni fake..sasa tutaponea wapi?
 
Hakuna wababaishaji kama TBS nilifikiri Ekelege akiondoka ubabaishaji utaisha kumbe ndo kwanza unaongezeka
Ubabaishaji umeshaingia kwenye mfumo, na umeshamiri sana sasa hivi. kwa hiyo mabadiliko ya viongozi siyo rahisi kubadili mfumo mzima. inataka jitihada pana zaidi. lakini pia tatizo kubwa sana la TBS ni kutoweza kusimamia hivyo viwango vyake. sawa mtu anapeleka sample yake inapimwa na kuidhinishwa kwamba amekidhi viwango. katika muda ambao anatumia hiyo nembo ya TBS, hao TBS wana uhakika gani kwamba anaendelea kutumia standard ile ile? maana inawezekana kabisa mwezi huu akatengeneza kwa standard lakini mwezi ujao akapunguza ubora na bado akaendelea kutumia nembo ya TBS! kinachotakiwa ni TBS yenyewe au kwa kushirikiana na wadau wengine, iwe na uwezo wa kufanya random sampling mara kwa mara ili kudhibiti ubora wa hizo bidhaa, kitu ambacho kwa sasa hakipo.
 
Naichukia sana TBS kwani imechangia sana watanzania kufa kwa bidhaa feki.
 

hawa TBS wameishiwa sera,mbona hawasemi tv na radio za Sony na Samsung?mazero tu!wanawasingizia watz,na hapa haimaanishi sio bora,ni kwa sababu hawajawakatia wamekasirika na kuwazushia mambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…