Kwa kifupi haya mashirika/taasisi za serikali zimepoteza sifa muhimu ya kutumika kwa niaba ya wananchi
mfano;
POLISI:-
wanashiriki ujambazi, kutupiga mabomu, kutubambikia makesi mpaka ya kigaidi BADALA YA KUTULINDA KWA SILAHA TULIZOWAPA, WAMETUACHA SOLEMBA!!!!!
TUME YA UCHAGUZI:-
tukishajiandikisha kuwa wapiga kura wanafanya jitihada kutuhujumu tusipige kura (visingizio kibao, mara uhakiki wa wapigakura, mara ukipoteza kitambulisho cha kupigia kura form namba. ...... hawataki itumike ili upige kura) "HUJUMA DHIDI YA JAMII" siku hizi wanakuja na matamko kabisaaaaa yanayopingana na sheria ya uchaguzi, eti ukipiga kura shuruti uondoke uende nyumbani, USIKAE ZILE MITA MIA MOJA zinazoruhusiwa kisheria KUSUBIRIA MATOKEO, (lengo waitende kura yako sawa sawa na mapenzi yao)
MAHAKAMA:-
huku nisiongelee sana unaweza kutana na Jaji, kwa maamuzi yake tu ukajua kuwa pengine ana cheti tu cha sheria, si diploma wala kadigirii
TBC:-
imekuwa TBCccm
BUNGE:-
Linalevya siku hizi, mibunge haina uwezo kabisaaaaaaaa wa kuitetea jamii! Mfano, imepitisha kodi ya "laini" za simu, baada ya miezi miwili ikirudishiwa hoja ili waifute hiyo hoja itaifuta kwa kishindo NDIYOOOOOOO (yaani haikujua athari za walichokuwa wanapitisha kwa mbwembwe miezi miwili iliyopita?) Ndiyo maana hata waziri mkuu akiagiza polisi kupiga wananchi mibunge haini kosa hapo.
TBS & TFDA:-
Wanasubiri athari ijitokeze kwenye jamii kutokana na ubovu wa bidhaa ndio wakurupuke na matamko yao ya kupiga marufuku, kuonya, taarifa kwa umma...... yaani kizunguzungu.
MAGOGONI:-
"wauza unga nawafahamu" (kama kichekesho vile)
MAPENDEKEZO:
tembo,faru na twiga wanatakiwa kujilinda!!!!!!
kila mwqnanchi awe na maabara apime ubora wa bidhaa kabla ya kuinunua/kuitumia.
kila mpiga kura ahakikishe analinda haki yake ya kupiga kura, na analinda kura yake anapoipiga.
........
........
.........
.........