Tahadhari: Utapeli ndani ya benki

mimi humu nakuja kupoteza muda kama kijiwe cha kahawa
usichukulie mambo ya humu serious
Point mkuu. Unaweza ukaumia watu wanavyojibizana, kumbe wajitesa... Wao wanafahamiana.
 
Ni ujinga kuibiwa wakati umeenda Bank kufanya mishe zako tu......yaani huwezi jiuliza tu kuwa unapata 3m kirahisi ivyo......hata NMB Kkoo wapo kibao tu
Hawa watu ni wataalamu wa psychologia kabisa, unajua ww labda umeenda na laki yako hapo ya ada ya watoto tena umeipata kwa msoto kweli kweli, the moment unasikia 3m ya chap akili inaanza kupanga matumizi badala ya kufikiri hii fursa gani inanifuata kizembe hiv? na huwa wanaangalia na mtu kama kwako 3m ni hela ya kawaida hawawezi kuja koz wanajua hautapanic wanatafuta mtu ambaye hiyo hela hajawaza hata kuiona kwa pamoja licha ya kuimiliki
 
Bado kwa mtu makini hata kama hiyo 3m kuipata au hujawahi kuishika ni uzembe mkubwa sana kukutana na mtu popote pale na yeye kuanza kuongelea kukunufaisha wewe hasa kipindi hiki cha uchumi mgumu na humjui......utaibiwa kama unatamaa tu na siyo vinginevyo
 
Yeah ndo wanacho deal nacho wanaamsha tamaa za mhusika kama yupo makini mission yao itakuwa imefel kama kwa mtoa maada
 
Huu ni utapeli Wa kishamba sana.

Huwa najiuliza mtu unaingiaje tamaa Kwa pesa ambayo hujaitolea jasho mpaka unaenda kutapeliwa.

Tunduma pia nimewahi kuwaona hawa washamba, mmoja anajifanya anakupita Kwa kasi huku anaongea na simu halafu mbele anadondosha Bunda la minoti ili ushoboke, hujakaa vizuri mwenzake anakuovateki anajifanya kuziwahi hizo Pesa eti ameokota, sasa ukiwa na Tamaa za fisi kujifanya macho kuona anakushawishi umfuate ili mkagawane hizo pesa. Huko sasa ndiyo wewe unageuka Fursa.
 
Tusio na Akaunti 'Benki' Uzi hautuhusu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…