Tahadhari: Utapeli ndani ya benki

Tahadhari: Utapeli ndani ya benki

Sasa hela si zangu nikitapeliwa inakuhusu nini?

Mbona kodi zetu zinatumika kuwalipa CCM.
H
Huwa nashangaa Sana, Tena Sana huu uzi haujahusisha Siasa nashindwa kuelewa CCM imefikaje hapa!!!!!

Hivi Mkuu matako yako kweli ulikuwa unayapa mapumziko ya viboko hiyo Elimu yako ya darasa la Saba!!
 
Mkuu hayo uloandika yaka ukweli mwingi .
Wengine wanakuwa na madawa wakisha kukamata utaenda kifwata ATM kadi dako au utaenda kaunta mwenyewe kisha utatoa hela na kuwakabidhi kisha.. baada ya muda akili hukurudia kawaida na kubaki kujilaumu.

Kipindi maduka huria ya kubadili fedha yalipo kuwepo..walikuwa na kawaida ya kuzengea maeneo hayo kisha kujidai kubadili kutoka fedha ya kigeni ya aona moja kwenda nyingine (mf :Euro kwenda USD)

Na mara nyingi hufika pale anapokubaini kwamba unazo hela nyingi za kigeni.
 
Wasalaam Wakuu.

Ijapokuwa uzi kama huu ulishetwa humu juu ya utapeli ndani ya benki, lakini haukuwa umeshiba. Nikaona niwaeleze kwa undani ili tumakinike.

Kuna wale wanaopenda kujua kama nimetapeliwa ama la, ukweli ni kuwa sijatapeliwa. Ila walikuwa wanajaribu kunitapeli.

Leo asubuhi nilienda katika moja ya benki kubwa sana hapa nchini kwa nia ya kufanya miamala miwili mitatu. Sitapenda kutaja jina la benki.

Nilipofika nikaanza kujaza slip zangu. Kuna mtu (akaja pembeni yangu kwa ajili ya kujaza slip. Sikuwa na wasiwasi, nikaendelea kujaza. Nilipomaliza nikaenda kupanga foleni. Naye bila hiyana akaja kunifata kwa nyuma.

Nikakaa kama dakika mbili, akaja mwenzake. Anajidai kumuuliza, kaka ni wapi wanapobadilisha fedha za kigeni? Mimi sijawageukia nikaendelea kusogea.

Yule aliyeulizwa naye akanigusa, "eti kaka, ni wapi wanapobadilisha fedha za Kiarabu? Maana nami ni mgeni hapa". Mimi nikawaonyesha dirisha la Bureau De Change. Wakati nageuka kuwaonyesha, huyu wa kwanza akamchapa swali lingine. Kwani ni fedha zipi za kiarabu?

Jamaa akachomoa kitita kumuonyesha. Na mimi niliona pia. Kwa juu kulikuwa na noti ya dollar 100 (genuine) ya Kimarekani. Akamuuliza ni bei gani, akasema ni Dollar 15,000.

Akamuuliza kwa hiyo nitapewa bei gani kwa fedha za Kitanzania? Jamaa akachukua simu, akaenda kwenye Calculator akaandika 1,500 mara 2300. Akamuambia Utapata kama 34,000,000 TZS.

Nenda kabadili utawekewa kwenye akaunti yako. Akasema sasa sina hata akaunti ya benki. Na nasikia huwa wanauliza kiasi hiki chote nimekipata wapi. Akamuuliza, kwani wewe umekipata wapi? Akasema mishe za madini. Akamuambia hapo pagumu.

Akanigusa tena, akaniambia wewe unamshaurije jamaa? Nikamuambia aende huko ambapo hatoulizwa. Machale yakanicheza.

Jamaa nilipogeuka akamuambia, kwani wewe unatupa Tsh ngapi ili nikakubadilishie. Akasema atatoa million 3. Akamuambia fanya tano. Jamaa akalia akasema labda nne.

Akamuambia, sawa nenda nje nakuja. Huyo jamaa akasepa. Jamaa akaniuliza, twende tukachukue hela tupate cha juu.. Nikamuambia hapana..

Tukaendelea kusogea, nilipokuwa wa pili, jamaa ni watatu. Yeye pia mkononi ana slip yake. Kwamba anahitaji kuhudumiwa. Wakati wa mbele anapewa slip aondoke, akajifanya kupokea simu. Kwa hiyo hii hela nisikuwekee tena? Ahaa, nikuwekee M-Pesa eeh? Poa. Huyo akatokomea. Nikaendelea kuhudumiwa.

Tahadhari za kuchukua:
a) Kwanza, wanakuja kwenye branch ambazo zipo busy. Watu ni wengi wanaopata huduma.

b) Wanakuangalia unapojaza slip ili kuwapa nafasi wajue kama una hela.

c) Zuia tamaa yako. Usikurupuke na kufurahia umepata dili. Wewe ndiyo dili mwenyewe, wanakutafutia namna wakupige.

d) Usiwape nafasi wakushawishi. Wana ushawishi mkubwa sana. Kuendelea kuwasikiliza, kuna 80% ya wewe kulia. Wapuuzie kabisa.

e) Wana ufahamu juu ya maswala ya kibenki. Kwa hiyo kukudanganya ni rahisi mno.

f) Ukikubali kufuatana nao, kubali kuwa hela yako imeenda. Pole sana.
ASANTE KWA TAHADHARI
 
Back
Top Bottom