Kinumbo
JF-Expert Member
- Dec 8, 2019
- 3,039
- 5,560
Habari zenu wakuu,
Nimepita kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii nimekutana na kitu inaitwa WAKALA ONLINE. Kama ujuavyo baadhi ya watanzania wanapenda pesa za mteremko yaani wapate pesa bila kushughulika. Pia kupenda njia za mikato, hapa wajinga wengi watapigwa na kitu kizito.
Hii kitu kwa namna nilivyo ifuatilia una jiunga kisha utaweka kiasi cha pesa kupitia namba itakayo kuwepo hapo. Baada ya hapo utasubiri masaa 24 kisha utapata nusu ya faida kutokana na pesa uliyo tuma hapo awali. Mfano ukituma 1,000 baada ya masaa 24 pesa yako itakuwa imeongezeka na kuwa 1,500 hapo unaweza kutoa 500 ikabaki 1,000 kisha utasubiri masaa 24 tena utoe 500, hivyo hivyo mpaka utakapo ona umetosha kupiga maokoto.
Hii kitu bado ni mpya haina muda mrefu mpaka sasa, ila mi nahisi hapa watu wanavutiwa upepo tu mwisho wa siku watajaa kwenye mfumo na kulia kilio cha mbwa mwitu.
Je, umewahi kutana ama kuisikia hii kitu katika pita pita zako huko kwenye mitandao ya kijamii na una maoni gani? Karibu