Nilikuwa kama wewe miaka miwili iliopita. Nadhani hakuna thread yoyote inayohusu meditation ambayo sikuipitia, tena kwa umakini mkubwa! lakini kila nilipojaribu, wapi niliambulia patupu yaani ilikua ni kukesha macho tuu bila hata kuhisi chochote kile. Nikbmua kuacha kabisaaa. Sasa, siku moja niliamka usiku, at midnight nikajiweka vizuri kwa ajiri ya kufanya meditation (taamuli) nilijihisi na imani sana usiku huo. Nikafumba macho, hapo hapo nikaanza kuona mabadiliko ya ajabu, nilihisi kuna mtu amekaa pembeni yangu, nikawa najikaza japo niliogopa sana, ila sikufumbua macho, mara nahisi makelele mengi, yaani sauti na miungulumo ya ajabu ajabu, mara naona nyota nyingiii na mandhali kama nipo juu angani katikati ya mawe makubwa ajabu, nyota, na mauzauza yasiovumilika, ghafla mwanga mkali ukanipiga machoni, nikashinda kuvumilia nikafumbua macho, uku nikihema kwa nguvu na woga usio kifani, cha ajabu sasa kumbe haikuwa usiku wala nini, nilikuwa nimepitiwa tu na usingizi ndani ya daladala,,abilia wote mimacho kwang