Ahsante, japo dunia ya leo inaweka suala la miditisha kwenye kukazia fahamu ama kutuliza akili, kwenye tamaduni za muda mrefu katika ujuzi, elimu na nidhamu za kiimani na dini kama Bara Hindi, kuna kupambanua mengi katika sura, muktadha na bidii ya kufungua milango ya fahamu, uwezo na taamuli.
Hapo juu umeweka vitendo nidhamu-mkao kadhaa kama ni tahajudi kwa maana ya miditisha hivyo si miditisha hasa ila kiufasaha wa mambo vinaanguakia kwenye vitu kama 'Dharana' ama 'Tratak' kwa mafundi wa mambo hayo. Hebu tazama 'dhyana' na halafu angalia 'vipassana' ni vitu gani na vinachimbukia wapi... Yoga ina mengi kwa mfano, lakini yenyewe hasa ndiyo hutumia maunganio ya mwili, akili na nafsi roho ili kunasibu mfunguko ama mkunjukuko wa fahamu kuelekeo kwenye utambuzi usio wa kawaida wa maumbo, hisia, misukumo na uhalisia wa nje na ndani wa yote. Unaweza kuwa kwenye nidhamu za kiyoga kwa ajili ya afya ya kimwili na kiakili. Lakini daraja bora kabisa ni Yoga itakayokusaidia kujitambua ulipo kuiingiliana na kosmosi yote. Yoga si dini, ni nidhamu na safari ya kiroho. Miditisha nayo katika daraja la ubora wake wenyewe kabisa si kitendo cha kiimani au dini tu ila ni sayansi kamili ya uzima na fahamu. Yoga daima hutimilizwa na miditisha lakini kwa uhuru kamili, hakuna kutumia namna nyenzo ya kukazia fahamu ili kubadili utumikishi wa akili na uwezo wake wote hata ule wenye kuweza kuleta yale yaliyozaidi ya kawaida kwa maana ya uhusiano wa 'boddhi' na 'siddhi' kwenye maarifa ya Yoga; bali ni kuachana na akili yenye na basi kurudi kwenye asili yenyewe ya uhai na uzima wote. Hiyo ndiyo huwa ni wokovu kamili na taamuli kamili... Kweli ya Mwisho.