CharmingLady
JF-Expert Member
- Apr 16, 2012
- 18,296
- 12,972
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Usiseme utajaribu shem bali unatakiwa kuanza hata leo hii yaani sasa hivi.......... LOL
Before you join the party...Fahamu kuwa ''meditation" is a Cult. pia na zaidi ya yote ni Anti-God. kama unaamini uwepo wa mungu ipo siku utaacha dini yako.leo nitafanya
nione matokeo yake
Before you join the party...Fahamu kuwa ''meditation" is a Cult. pia na zaidi ya yote ni Anti-God. kama unaamini uwepo wa mungu ipo siku utaacha dini yako.
fanya utafiti binafsi.
Mkuu LifeHacker,Nawashangaa sana hasa watanzania wanaopenda kuchukuliwa na kila aina ya upepo. Hii ni dini, paganism, kuna watu wanaonekana kuhamasika na kuanza kujifunza au kujaribu wakati huo huo wanajiita wakristo! Hakika hamjui mlitendalo! Soma hapa:
Meditation - Wikipedia, the free encyclopedia
Kuna aina nyingine ya paganism inayofanana na hii nayo ni scientology: Scientology - Wikipedia, the free encyclopedia na zingine Pasco alishawahi kuzielezea zinaitwa psychic powers: List of psychic abilities - Wikipedia, the free encyclopedia
Hizi ni imani za kipagani, nazo ni derivatives au components za wicca: Wicca - Wikipedia, the free encyclopedia, witchcraft: Witchcraft - Wikipedia, the free encyclopedia, spells: Spell (paranormal) - Wikipedia, the free encyclopedia na magic: Magic (paranormal) - Wikipedia, the free encyclopedia
Halafu Mtambuzi unadriki kusema wakristo wanatumia rozari! Rozari ndio nini na wapi wakristo wameambiwa waitumie kwenye Biblia? Sema Waroma (organization) sio wakristo.
Jamani waonyeni watu wasiende katika njia hizi ziendazo upotevuni.
CC: warumi, Samaritan, Majimoto, Himidini, Ablessed, everlenk, LORDVILLE
Mkuu LifeHacker,
Usitake kudanganya watu humu na kuwatisha kuhusu Tahajudi/meditation na kuilinganisha na paganisim, hadi kuwatishia kuwa ni uchawi!. No!, sio kweli!.
Meditation ni concentration on focus to gain insight ambayo ndio source of powers!.
Hata Yesu alifanya meditation!.
Kwenye mada yangu hii Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. Wengi wanazo Ila Hawajitambua!.
Nimezungumzia Sisi binadamu wote tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, God is Power!, na ametupa hizo powers kwa kila mmoja wetu, (Omnipresence), pale alipotupulizia pumzi ya uhai!. Ili kuweza kuzitumia hizo powers, lazima ufanye meditation to get insight, na kuzifungulia zilikofungiwa!.
Kwenye uzi ule, pia nilimzungumzia shetani na source yake, na nikawatahadhirisha watu humu kuwa hata shetani, naye pia ana powers na pia yuko popote, na ili kuzitumia nguvu za shetani, pia watu hufanya meditation!.
Pia nikatoa somo kuhusu Nguvu za Mungu ni "Nguvu za Mwanga" (Powers of Light) na nguvu za shetani ni "nguvu za giza", "powers of darkness" na kutoa angalizo kubwa na makini kabisa kuwa "the deviding line" between "Powers of Light" and "powers of darkness" ni very thin!. Nikasema Yesu alituonya kuwa sio kila anayeita "Bwana Bwana!", ni wangu!", "Watakuja watu, watafanya ishara kwa jina langu lakini sio wangu!", akimaanisha sio kila Mhubiri anayefanya miujiza kwa kuhubiri kwa Jina la Yesu, ndio anatumia nguvu za Mungu!, wengine wanatumia nguvu za giza!. Wako wengi wetu humu duniani, wanafuata dini fulani na mafundisho fulani wakidhani ndio wanamtumikia Mungu, kumbe wanamtumia shetani bila kujijua kwa sababu shetani nae ana nguvu na amepozi kama mungu!.
Ili kuweza kuijua "kweli" ni lazima ufanye meditation, ili uweze kufunuliwa!.
Hata baadhi ya Walokole kibao tuu, kwenye ibada zao za mikesha, wanafanya meditation, na pale wanapofunuliwa na kunena kwa lugha, wengi wakiamini huyo ndio "Roho Mtakatifu!", its not necessarily so!, nyingine ni "liroho!" hivyo bila meditation huwezi kuijua kweli na bila kujua unaweza kuingizwa chaka!.
Mkuu Mtambuzi yuko very right, watu wafanye Tahajudi wajitambue!. Hata wewe Mkuu MdukuziMaisha (LifeHacker) nilikusoma mahali uko deep!, kitendo tuu cha kushika vitabu vitakatifu kama Biblia Takatifu au Quaraan Tukufu, kuvisoma huku umetulia!, ni Tahajudi Tosha!.
Pasco.
Mkuu Pasco,
Ufunuo au kupata insight kwa mkristo kupo kwenye Biblia na mtu hahitaji kufanya meditation ili aweze kufunuliwa, bali kwa kusikia Neno kwa usahihi, kulisoma na kwa kuomba ili Roho wa Mungu amwongoze katika kulielewa na kulitenda. Neno meditation kama lilivyotumika kwenye Biblia lina maana ya kutafakari kwa makini au kwa kina kuhusu jambo fulani "to think, conteplate, devise, ponder" sometimes to "sigh or murmur", Biblia haiwaambii watu wafanye practices kama alivyoonyesha Mtambuzi.
Yesu hakufanya meditation (kwa jinsi mlivyoielezea) na wala hakuhitaji kwa sababu Yeye ni AllMighty: Omnipotence - All powerful, Omnipresence - He is not limited by time and space, He is everywhere at all times, Ominiscience - All Knowing.
Kwa mjibu wako au wengine meditation lengo lake ni kumpa mtu focus, insights na powers, Yesu ni Mungu na Nguvu, uwezo, mamlaka, insights zote zatoka kwake, na ni designer wa foci, sasa afanye meditation ili iweje? Ili nani ampe uwezo gani? He is infinite God.
Biblia inaposema mwanadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu unadhani maana yake ni kwamba anaweza kuwa na nguvu na uwezo kama Mungu? La hasha, nguvu za Mungu hata 1 over trillion mwanadamu hana. Mungu anaposema mwanadamu ameumbwa kwa mfano wake huhusianisha zaidi na mambo ya utakatifu - kwamba mwanadamu anaweza kuendelea kubadilika na kufanana naye kwa kuwa na utakatifu au ameumbwa na asili ya utakatifu kama alivyo Mungu na atakuwa mtakatifu kamili (kwa waliookoka) siku atakaponyakuliwa na kwenda mbinguni. Kwa habari ya nguvu Mungu amesema kila leo mwanadamu uwezo wake ni very limited.
Hauhitaji kufanya meditation kama ulivyoilezea ili kuijua kweli - Neno la Mungu ni kweli, and it's very apparent. Meditation ni imani, iwapo utaigeukia hiyo na kuacha imani ya Kikristo unamtumikia mungu mwingine na sio Mungu wa Biblia. Mtu anafunuliwa kwa njia ya Roho Mtakatifu kupitia Neno la Mungu.
Na kuhusu habari ya kunena kwa lugha ni ishara ambazo zilifanywa wakati mitume wanasimika Neno la Mungu (wakati wanaweka msingi). Kwa sasa hizo huduma zimesitishwa, hazipo. Kunena kwa lugha sio kelele zisizokuwa na mpangilio wenye maana au kuongea lugha ambazo haziexist kama wafanyavyo watu siku hizi, bali ni mtu asiyejua lugha fulani kupata uwezo wa kuiongea kiufasaha na pia Biblia inasema katika kanisa wanaweza kunena wawili au watatu na lazima awepo mtu wa kutafsiri. Mfano mzuri ni siku ya Pentekoste, watu walinena kilugha kwa maana ya kuongea lugha ambayo hapo awali hawakuwahi kujifunza wala kuijua na watu wengine waliweza kusikia na kuelewa walichokuwa wakisema na kushangaa. Unakuta watu wanalia kanisa zima halafu milio kama ya wanyama na ndege huku hakuna mfasiri hata mmoja! Hiyo sio kunena kilugha ni drama/movie.
Mtu anapata Roho mtakatifu pale tu anapompokea Kristo. Wokovu, kupokea Roho mtakatifu, kusamehewa dhambi; vyote vinatokea concurrently.
Kuijua kweli ni kupitia Neno la Mungu na si vinginevyo. Na Neno la Mungu linasema ukiwa na Imani ndogo tu kama punje ya haradali unaweza hata kuhamisha mlima (hiyo nguvu umeiongelea)! Unaona kwamba haya mambo yanafanyika kwa imani. Sawa imani inaweza kuwa ni ya giza au mwanga kama ulivyosema.
Meditation ni "cult", ni kitu kinachooshiria imani nyingine, inahusisha alteration of mind na kucreate scenes ya mambo ambayo hayapo, badala ya kumfanya mtu ajitambue inamfanya awe convoluted kwa sababu anakuwa subjected to an environment where he/she does not fit naturally.
Meditation ni dini/imani
"Meditation has been practiced since antiquity as a component of numerous religious traditions and beliefs.[SUP][6][/SUP]" - wiki.
"The history of meditation is intimately bound up with the religious context within which it was practiced." - wiki
Kuna references nyingi including vitabu vinavyoelezea how meditation the way you have stipulated is a religion/belief system. Kama nilivyosema, meditation, scientology, wicca, spell, magic, witchcraft ni intermingled practices in the sense that they borrow from each other!
Labda juve2012 na 2013 wana mchango wao kuhusu hili