Nadhani hapa sasa tukubaliane kutokukubaliana, Mimi na Mchambuzi sio wahubiri, wala mafundisho yetu ya meditation hatujasema ni mafundisho ya dini fulani, tumetoa mafundisho kwa watu wote wa dini zote, maadam umejitabaisha wewe umejiconfine kwenye Biblia, them keep your confinment kwenye Biblia, ambayo imekuja imeikuta meditation tayari ipo, Yesu amekuja amaikuta maditation ipo, ameitumia, ameifundisha ameondoka na kuiacha meditation ipo, kama kupitia Mafundisho ya Yesu, Bibilia na Ukristu, kuna specific meditationa za Kikristu tuu, then natoa wito kwa Wakristo wote, fuateni meditation ya kwenye Bibilia, sisi wengine tuendelee na darasa la meditation ya watu wote!.
Mimi ni Mkiristu, Mkatoliki, mama yangu ni Born Again!. Sisi Wakatoliki tunaipiga pombe kama kawa, Divai hadi Altareni kwa hoja kuwa huo ndio muujiza wa kwanza wa Bwana wetu Yesu Kristo, alioufanya kwenye harusi ya Kana!. Mama yangu haamini katika pombe, akiamini kunywa pombe ni dhambi kwa mujibu wa imani yake, na kutusisitiza tuokoke tujiunge na dini za wokovu, baadhi ya wadogo zangu wameokoka na sisi wengine tumekomaa na kuendelea kusimama na Kanisa Moja, Takatifu la Mutume, ambalo ndilo pekee Bwana wetu Yesu Kristu aliliacha, hivyo kutobabaishwa na hivi vijikanisa lukuki vinavyoibuka kama uyoga na kutuhubiria Pombe ni dhambi!. Hivyo ndivyo ninavyokuona wewe na mahubiri yako humu kuwa Tahajudi ni upagani!. Endelea na unachoamini, na sisi tuache tuendelee kuwafundisha watu kujitambua hadi kufikia kiwango cha kutodanganyika na hivi vidini vya uongo uongo vyeme wahubiri wanaotumia nguvu za giza kuwapoteza watu wa Mungu!.
Please keep your way and let us keep our way na kama vipi, unaweza kuanzisha uzi wako wa "Jifunze Kufanya Tahajudi ya Kikristu" ili Wakristu wafanye Tahajudi ya kwenye Biblia!.
Pasco