Tahakiki ya hotuba ya Rais Samia Bungeni, 14 Novemba 2025: Mazingira, Madhumuni, Muundo, Mazuri, Mabaya, Mapengo na Mapendekezo

Tahakiki ya hotuba ya Rais Samia Bungeni, 14 Novemba 2025: Mazingira, Madhumuni, Muundo, Mazuri, Mabaya, Mapengo na Mapendekezo

Doctor Mama Amon

Platinum Member
Joined
Mar 30, 2018
Posts
2,311
Reaction score
3,513
​
Samia Bungeni.png

Tahakiki ya hotuba ya Rais Samia Bungeni, 14 Novemba 2025: Mazingira, Madhumuni, Muundo, Mazuri, Mabaya, Mapengo na Mapendekezo

1. Utangulizi


Mnamo tarehe 14 Novemba 2025, Rais Samia alitoa hotuba ya kufungua Bunge la 13, akiwa bungeni Dodoma.

Hivyo, hapa chini najadili muundo, maudhuo, mtiririko, mazuri, mabaya, mapengo na mapendekezo stahiki.

2. Mazingira ya hotuba

Kabla ya kulihutubia Bunge Rais Samia alikagua gwaride rasmi nje ya Bunge lililoandaliwa na vyombo vya ulinzi na usalama. Wanagwaride walimwimbia wimbo wa Taifa na Wimbo wa Afrika Masharika.

Kisha Rais Samia aliingia bungeni na kuwahutubia wabunge, mabalozi, watumishi wa umma, mawaziri wakuu wastaafu, wageni waalikwa, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usala walioko ofisini na wastaafu, na Taifa zima kwa ujumla.

Hata hivyo, Rais Samia alizindua bunge ambalo uhalali wake unapingwa na umma kwa sababu kwamba, tukiachana na kura za kupikwa, hakuna mbunge wala diwani aliyepata kura halali za kutosheleza yeye kutangazwa mshindi.

Usahihi wa imani ya umma unaimarishwa na ukweli kwamba, wakati Rais Samia anazindua Bunge, bado kuna uhalifu wa kiuchaguzi unaendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Dar es Salaam, katika Kata ya Kwembe, Jimbo la KIbamba, Wilayani Ubungo.

Huko Kwembe kuna zoezi la upigaji wa kura feki linaendelea, hata baada ya tarehe 29 Oktoba 2025.

Lengo la Tume ya Jaji Mwambegele ni kutengeneza kura za Rais na Wabunge, ili kura za kwenye masanduku ziweze kuwiana na takwimu feki za ushindi wa Rais na Wabunge, ambazo tayari zimetangazwa kihalifu na Tume Huru ya Uchaguzi.

Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wanaujua fika ukweli kuhusu uhalifu huu. Lakini bado wakubwa hawa nimeona wameambatana na Rais Samia asiye na uhalali akiwa analihutubia Bunge lisilo na uhalali.

3. Madhumuni ya hotuba

Madhumuni ya hotuba ya Rais Samia yalikuwa ni kuzindua Bunge la 13 kwa kufanya mambo mawili.

Mosi ni kujenga matumaini kwa kuweka mwelekeo wa kisera wa kazi za serikali kati ya 2025 na 2030 chini ya serikali ya awamu ya sita.

Na pili ni kutangaza mikakati ya kuponya majeraha ya kisaikolojia, kisiasa, kiuchumi, kifamilia na kijamii yaliyotokana na mchakato wa uchaguzi mkuu wa 2025.

4. Muundo wa hotuba

Nakala ya hotuba iliyochapishwa na kuwekwa mtandaoni, na kuwekwa katika tovuti ya Wizara ya Mawasiliano, inao urefu wa kurasa 26, imeandikwa kwa mtiririko wa aya baada ya aya bila vichwa vidogo vya maneno ili kumwongoza msomaji, na inayo maneno 6,820. (Nimeambatanisha).

Kwa kuangalia mtiririko wa maudhui, naona kuwa Rais Samia aligawanya hotuba yake katika maeneo makuu matatu:

  • Kukiri kuwepo kwa tukio la mauaji ya halaiki,
  • Mkakati wa maridhiano, na
  • Dira ya kiuchumi na kijamii kulekea 2030.
5. Mazuri ya hotuba
  • Amekubali kuwa maandamano ya 29 Oktoba 2025 yalifanywa na Watanzania.
  • Amekiri kuwa kuna uharibifu na upotevu wa mali ulifanywa na baadhi ya waandamanaji.
  • Ameelza kusikitishwa kwake na ukweli kwamba kuna watanzania wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa kutokana na maandamano hayo.
  • Ametoa pole kwa familia zilizofiwa na watoto wao.
  • Ametamka kuwa kunahitajika maridhiano ya kitaifa kwa ajili ya kuponya nafsi na kuliunganisha Taifa.
  • Amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kutofautisha kati ya waandamanaji na wahaini, kuwasamehe waandamanaji wote, na kutaka waachiwe mara moja.
  • Amekubali umuhimu na ulazima wa Kuundwa kwa Tume ya Uchunguzi (Enquiry Commission) kwa ajili ya kuchunguza mazingira, sababu, na matokeo ya vurugu za msimu wa uchaguzi.
  • Ametoa mwelekeo wa kisera kwa kufupisha ilani ya CCM kwa ufundi mkubwa
  • Ameufanya ustawi wa vijana, ambao ni 60% ya watanzania wote, kuwa kipaumbele cha serikali kwa kuamua kuwaundia Wizara kamili.
    • Ajira: Lengo ni kutengeneza ajira milioni 8.5 ifikapo 2030.
    • Nishati: Lengo ni kuongeza uzalishaji umeme maradufu kutoka Megawati 4,000 hadi Megawati 8,000 na kusukuma mradi wa kihistoria wa Gesi Asilia (LNG) wa Dola Bilioni 42.
    • Miundombinu: Lengo ni kukamilisha miradi yote ya SGR, kukarabati TAZARA, na kupanua bandari zote kubwa.
    • Madini: Lengo ni kuanzisha Mfuko wa Wakfu wa Madini.
    • Vijana: Lengo ni kuunda Wizara kamili ya Vijana na kutoa Shilingi Bilioni 200 kwa mitaji ya vijana na wanawake.
    • Uwajibikaji: Lengo ni kuhakikisha kuwa watumishi wa umma wanabadilika. "Watendaji msipobadilika, tutawabadilikia," alisema Rais Samia.
Hata hivyo, mazuri haya yanakosa mvuto kwa sababu ya mauaji ya halaiki ya vijana ambao sasa hawawezi kunufaika na mipango hii.

Vijana wengi wameuwawa kwa kupigwa risasi kwa sababu tu ya kuikosoa serikali kwa hoja, ambazo baadhi yake zinajibiwa wakiwa tayari kaburini.

6. Mabaya ya hotuba

  • Rais Samia anasema kuwa ameunda Tume ya Uchunguzi wakati anayepaswa kuchunguzwa ni yeye mwenyewe.
  • Ameendeleza kuimba wimbo wa uwongo aliousema tarehe 03 Novemba siku ya kuapa, alipodai kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilifanya kazi nzuri, akiisifia kwa ufanisi.
  • Kauli hizi ni za kujitoa ufahamu kwa makusudi na haziwezi kukubalika huku uraiani ambako tunajua idadi ya wapiga kura kwa kila kituo kupitia kwa mawakala wa siri waliowekwa na asasi za kiraia.
  • Kwa mfano tu: Kwa mujibu wa mwangalizi wasiri katika kituo cha Kibada kule KIgamboni, karibu n dispensari ya St. Joseph, walifika wapiga kura 40 pekee.
  • Ameendelea kutumia maneno tata “upotevu wa maisha” bila kukiri kwamba huo “upotevu wa maisha” ni “mauaji ya halaiki” yaliyosababishwa na utovu wa nidhamu wa vyombo vya dola vya ndani na nje ya nchi vilivyokuwa vinasimamiwa na yeye Rais Samia chini ya kiapo chake cha kwanza cha Urais alichokula Machi 2021.
7. Mapengo ya hotuba
  • Rais Samia hajakiri kuwa yeye ndiye aliyekodisha wanajeshi kutoka Uganda, Zambia na Zanzibar na kuwaleta hapa nchini wakiwa dhini ya "chain of command" iliyo nje ya mfumo wa JWTZ, na hivyo kuiweka Tanzania katika mikono ya "uvamizi wa kigeni" yaani "foreign occupation," jambo ambalo linamwondolea sifa ya kuwa kiongozi nchini Tanzania.
  • Hajalaani mauaji ya halaiki yaliyotokea katika wiki ya uchaguzi, maana "kueleza sononeko" sio kulaani.
  • Hajatamka mkakati wa kupambana na ufisadi wala rushwa.
  • Hajakemea utekwaji na mauaji holela ya Wananchi wanaoikosoa serikali.
  • Hajaongelea mageuzi katika tume ya uchaguzi.
  • Hajaongelea mchakato wa kupata Katiba mpya.
  • Hajatamka Watu wangapi wamekufa, idadi ya majeruhi, na mkakati wa serikali kwa ajili ya kutoa huduma muhimu kwa majeruhi.
  • Hajaeleza ni hatua gani zitachukuliwa dhidi ya maofisa wa vyombo vya dola waliofanya mauaji ya waandamanaji wasio na silaha, pamoja na raia waliofuata nyumbani mwao na kuuwawa kihuni.
  • Hajaeleza ni kwa nini alikubali miji mikuu ya Tanzania ikaliwe na majeshi ya kigeni, yaani iwe chini ya "foreign occupation," kwa siku tano tangu 29 Oktoba mpaka 03 Novemba 2025.
  • Hajawasaidia Watanzania kupata jawabu kwa swali lifuatalo: Je, mauaji ya waandamanaji na watu baki yaliyotekelezwa na vyombo vya ulinzi na usalama katika wiki ya uchaguzi wa Oktoba 2025 ni matokeo ya operesheni halali ya kijeshi, operesheni halali ya kipolisi au mauaji holela yaliyo haramu kisheria, na nani aliamuru mauji hayo?
  • Yaani, Rais Samia amekwepa kabisa kujibu swali lifuatalo: "Were the targeted killings of demonstrators and others during an election week in October 2025 legitimate armed-conflict operations, law enforcement operations or punishable extra-judicial killings, and, under whose authority were they conducted?"
  • Kama Rais Samia angetafakari kwa utulivu na kujibu swali hili angeelewa haraka na kukubali rai kwamba anapaswa kujiuzulu mara moja.
8. Tathmini ya hotuba ya hotuba

Lengo la hotuba ya kufungua Bunge lilifanikiwa kwa 55%. Napunguza 45% kwa sababu ya mabaya na mapengo niliyoyataja hapo juu.

Lakini hasa, napunguza 45% kwa sababu ya Rais Samia kushindwa kujibu swali lifuatalo:

Je, mauaji ya waandamanaji na watu baki yaliyotekelezwa na vyombo vya ulinzi na usalama katika wiki ya uchaguzi wa Oktoba 2025 ni matokeo ya operesheni halali ya kijeshi, operesheni halali ya kipolisi au mauaji holela yaliyo haramu kisheria, na nani aliamuru mauji hayo yatekelezwe?

Wakati mauaji haya yanatekelezwa bado Rais Samia alikuwa ni mkuu wa nchi, Rais na Amiri Jeshi Mkuu chini ya kiapo cha Urais cha mwaka 2021.

Kwa ajili ya kuonyesha ukubwa wa tatizo hili, nataka nieleze kidogo kuhusu tofauti kati ya mambo mawili.

Jambo la kwanza ni mbinu za makabiliano ya kivita (“armed-conflict paradigm of security forces deployment”) kati ya vyombo vya dola na raia.

Na jambo la pili ni mbinu za makabiliano ya kipolisi (“law enforcement paradigm of security forces deployment”) kati ya vyombo vya dola na raia.

Sera zetu zinatofautisha operesheni za kivita na operesheni za kipolisi

Sera yetu ya usalama wa taifa inatambua mgawanyo wa majukumu ya kijeshi na majukumu ya polisi ili jeshi na polisi wafanye majukumu tofauti kwa uwazi na wasiingiliane katika maeneo ya nidhamu ya kila mmoja.

Wakati kusudi la jeshi ni kupigana vita kati ya nchi yetu na majirani, kusudi la polisi ni kusimamia utekelezaji wa sheria za jinai za ndani ya nchi.

Hata "vitisho vya eneo la kijivu" kama vile biashara ya dawa za kulevya, uhalifu uliopangwa au ugaidi vinahitaji ujuzi wa uchunguzi wa hali ya juu na kufuata taratibu za kujenga kesi pamoja na ushirikiano wa karibu na mamlaka. Hizi ni kazi za polisi.

Wafanyakazi wa jeshi, kwa upande mwingine, wamefunzwa kulinda eneo la taifa kutokana na vitisho vya kijeshi vya kigeni na wamepewa silaha zilizoundwa kuwaua adui, badala ya kuwakamata au kuwalemaza.

Uhuru wa kijeshi katika kutumia nguvu ya mauti dhidi ya watu

Hasa, wakati wa vita, wanajeshi wana kibali cha kuua mahasimu wao, kuwalemaza, na kukamata, kama wakiamua hivyo.

Wanayo hadhi ya upendeleo inayowapa kinga dhidi ya mashtaka kwa vitendo ambavyo kwa kawaida vingehesabiwa kama mauaji haramu kisheria, shambulio la jinai, utekaji nyara, na kadhalika.

Hakuna kizuizi cha kuangalia uwiano wa nguvu itakayotumika kinachotakiwa kuangaliwa kabla ya kuwaua wapiganaji wa adui wakati wa vita, mradi tu kuwepo na faida yoyote ya kijeshi ya kuhalalisha kufanya hivyo.

Na hakuna sharti la kuwataka wanajeshi kutumia nguvu kama hatua ya mwisho kwenye shughuli zinazolenga kumuua adui vitani. Mlengwa anaweza kuuawa kwa risasi ya moto, hata kama kukamatwa kwake kungekuwa rahisi zaidi.

Majeshi pia yana haki ya kusababisha viwango vya uharibifu wa mali za majirani, ambavyo haviwezi kuvumilika katika mazingira ya operesheni za kipolisi wakati wa amani ya ndani ya nchi.

Uharibifu wa huu unamaanisha madhara yasiyokusudiwa yanayosababishwa kwa wahusika wasiolengwa moja kwa moja, hasa raia na mali zao, wakati wa operesheni ya kijeshi.

Wapiganaji wana haki ya kutumia nguvu ya mauti na kupokea kinga dhidi ya mashtaka kwa mauaji yanayofanywa kwa mujibu wa sheria za kijeshi.

Mashambulizi halali ya kijeshi hayajumuishi tu wapiganaji, lakini pia raia ambao watashiriki moja kwa moja au kikamilifu katika kushirikiana na upande wenye uhasama dhidi ya jeshi.

Mipaka ya kipolisi katika kutumia nguvu ya mauti dhidi ya watu

Hata hivyo, haki hizi za makabiliano ya kijeshi zinatumika tu wakati wa vita. Nje ya vita, wapiganaji na hata polisi wenye silaha, wanapigwa marufuku kumuua mtu yeyote isipokuwa tu kama ni kwa sababu ya kujilinda dhidi ya hatari ya wazi.

Mfumo wa utekelezaji wa sheria za kipolisi huwachukulia watu walio upande hasimu kama wahalifu, wanaopaswa kukamatwa, kushtakiwa, na kupewa haki ya kujitetea, kabla ya kutiwa hatiani na kuadhibiwa.

Polisi wana haki ya kutumia nguvu ya kuua kulingana na kanuni ya uwiano, kanuni ya utofauti, kanuni ya tahadhari, na kanuni ya suluhisho la mwisho. Lakini, hawana kinga dhidi ya mashtaka kwa mauaji yanayofanywa kinyume na kanuni hizi.

Kwa hiyo, chini ya "mfumo wa utekelezaji wa sheria za kipolisi," nguvu ya kuua inahesabiwa haki tu wakati inapokuwa ndiyo njia pekee ya kufikia lengo muhimu la kuzuia tishio kubwa, na nguvu inayotumika inapaswa isiwe kubwa kuliko inavyohitajika ili kufikia lengo hilo.

Kwa kifupi, basi, tunayo mifumo miwili ya kisheria kuhusu matumizi ya nguvu dhidi ya watu walioko upande hasimu. Kuna sheria za kijeshi na sheria za jinai.

Mifumo hii inazo kanuni maalum zinazoongoza matumizi ya nguvu ya mauti dhidi ya watu katika mazingira tofauti, na kanuni hizi ndio huonyesha utofauti kati ya mifumo hii miwili.

Kanuni zinazoongoza matumizi ya nguvu ya mauti dhidi ya watu

Kadiri matumizi ya nguvu ya mauti yanavyohusika, tofauti kuu kati ya sheria za kijeshi na sheria za kipolisi zinaweza kufupishwa kama ifuatavyo:

(1) Kanuni ya ulazima (necessity): Chini ya mfumo wa uhasama wa kijeshi, ulazima wa kijeshi kutumia nguvu dhidi ya mlengwa halali ni kanuni ya kawaida.

Kwa maneno mengine, dhana ni kwamba mahasimu wanaweza kushambuliwa kihalali moja kwa moja kwa lengo la kuwaua.

Kwa upande mwingine, chini ya mfumo wa uhasama wa kipolisi, kanuni ya ulazima ina maana kwamba matumizi ya nguvu lazima yawe suluhisho la mwisho na nguvu inaweza kutumika tu ili kufuata lengo halali, kama vile kujilinda, kutekeleza ukamatwaji wa halali, kuzuia kutoroka kwa mtu aliyefungwa kisheria, au kutuliza ghasia.

(2) Kanuni ya uwianifu (proportionality): Kanuni za mfumo wa makabiliano ya kijeshi zinakataza shambulio dhidi ya mpiganaji halali ikiwa shambulio hili linaweza kutarajiwa kusababisha upotevu wa maisha ya raia, majeraha kwa raia, uharibifu wa vitu vya raia, au mchanganyiko wake, ambao ni mwingi kama ukilinganisha na faida halisi na ya moja kwa moja ya kijeshi inayotarajiwa.

Kwa maneno mengine, kanuni ya uwianifu inalinda raia walio karibu na vitu vya walengwa kutokana na uharibifu ambao ungekuwa mwingi kama tukilinganisha na faida halisi na ya moja kwa moja ya kijeshi inayotarajiwa kutokana na shambulio.

Na katika mfumo wa makabiliano ya kipolisi, matumizi ya nguvu lazima yaepuke vifo au majeraha ya watu wanaokabiliwa.

(3) Kanuni ya tahadhari (precaution): Kanuni hii inahitaji wapiganaji wa kijeshi kuchukua tahadhari ya mara kwa mara ili kuwaokoa raia, na vitu vya raia.
Kinyume chake, chini ya makabiliano ya kipolisi, tahadhari zote lazima zichukuliwe ili kuepuka, kadri iwezekanavyo, matumizi ya nguvu kama hayo, na si tu kifo cha raia au jeraha au uharibifu wa vitu vya raia.

(4) Uhalali wa kisheria: Taifa lazima litunge sheria na kanuni kuhusu mipaka ya matumizi ya nguvu kwa ajili ya kuwaongoza maafisa wao.

Yaani, mfumo wa kisheria na kiutawala lazima udhibiti hali zote zinazozunguka matumizi ya nguvu kwa kuonyesha nani, lini na vipi nguvu zinapaswa kutumika. Pale matumizi ya nguvu yanapokatazwa na miongozo lazima maofisa watii miongozo hiyo.

(5) Uwajibikaji: Shughuli za utekelezaji wa sheria lazima zipangwe kwa uangalifu ili kuepuka, kadiri iwezekanavyo, matumizi ya nguvu na kupunguza hatari kwa watu wasiohusika.

Na matukio ya vifo au majeraha lazima yaripotiwe haraka kwenye mamlaka husika.

Aidha, matumizi yoyote ya nguvu kupita kiasi, au vinginevyo kiholela, lazima yachunguzwe ipasavyo, na inapohitajika, yaadhibiwe kama kosa la jinai na/au kuchukua hatua za kinidhamu kulingana na uzito wa kesi.

Maafisa wakuu na maafisa wa serikali walio chini ya amri yao wanapaswa kuwajibishwa kutokana na matumizi ya nguvu isivyo halali.

Kwa hivyo, mawakala wa serikali wanapaswa kutajitahidi, kwa kiwango kikubwa iwezekanavyo, kupunguza majeraha na heshima na kuhifadhi maisha ya binadamu.

Kwa muhtasari, "mfumo wa makabiliano ya kipolisi" na "mfumo wa makabiliano ya kijeshi" ni mifumo miwili tofauti ya kisheria ya matumizi ya nguvu, ambayo kimsingi hutofautishwa na aina ya hali na sheria zinazotawala.

Mfumo wa makabiliano ya kipolisi, unaotumika wakati wa amani, unaongozwa na sheria ya haki za binadamu na unahitaji kiwango cha chini cha nguvu kinachohitajika, mara nyingi kinacholenga kukamata badala ya kuua.

Kwa upande mwingine, mfumo wa makabiliano ya kijeshi, au mfumo wa sheria ya vita, hutumika katika hali za migogoro ya uhasama wa kivita na inaruhusu matumizi mapana ya nguvu hatari ili kumdhoofisha au kumpunguza nguvu adui kwa kumwua.

Aina tofauti za mbinu za kukabili watu kwa nguvu

Kwa hivyo, tunao mfumo wa "ngazi tofauti za matumizi ya nguvu" ambao huwapa maafisa wa kijeshi na maafisa wa polisi miongozo ya kawaida kuhusu ni nguvu kiasi gani inaweza kutumika dhidi ya mtu anayeonekana kuvunja sheria katika mazingira fulani.

Mfano mmoja wa mfumo wa ngazi hizo unazo hatua sita zifuatazo: Uwepo wa afisa, Amri za maneno, Vidhibiti laini, Vidhibiti vigumu, Silaha za Kati, na Silaha za Nguvu ya Kuua.

(1) Uwepo wa afisa eneo la tukio- utaalamu, sare, na mkanda wa matumizi wa afisa wa kutekeleza sheria na chombo au gari lenye alama ambalo afisa anafika eneo la tukio.

(2) Amri za maneno - mwelekeo wazi na unaoeleweka wa maneno na afisa anayemlenga mtu.

(3) Udhibiti laini - Matumizi ya kiwango cha nguvu ambacho kina uwezekano mdogo wa kusababisha uharibifu wa tishu laini au kuvunjika kwa mfupa.

(4) Mbinu za Kujibu kwa Ukali - kiasi cha nguvu ambacho kina uwezekano wa kusababisha uharibifu wa tishu laini au kuvunjika kwa mfupa au kuwasha ngozi, macho, na utando wa ngozi ya puani.

(5) Silaha zenye nguvu za kati – kiasi cha nguvu ambacho kingekuwa na uwezekano mkubwa wa kusababisha uharibifu wa tishu laini za mwili au kuvunjika kwa mifupa. Mfano ni fimbo inayonesanesa, fimbo ngumu, dawa ya pilipili, risasi za mpira, mbwa wa polisi, n.k.

(6) Nguvu ya kuua – nguvu yenye uwezekano mkubwa wa kusababisha kifo au jeraha kubwa la mwili.

Aina za watu wanaopaswa kukabiliwa kwa nguvu ya mauti

Katika matumizi ya mfumo wa "ngazi tofauti za matumizi ya nguvu," vitendo vya mhusika vimeainishwa ili afisa aweze kubaini haraka ni kiwango gani cha nguvu kinachoruhusiwa na ambacho kinaweza kuwa muhimu ili kumlazimisha mhusika kufuata sheria.

Hapa chini naeleza jinsi mhusika anavyonainishwa kwa kuzingatia iwapo ni mtiifu au mkaidi, mchokozi au sio mchokozi, mwenye madhara au asiye na madhara.

(1) Mtiifu na mpole (Passive compliant)- mtu anayetambua mamlaka ya uwepo wa maafisa na kufuata amri za maneno za afisa.

(2) Mkaidi na mtukutu (Passive resistor)- mtu anayekataa kufuata amri za maneno za afisa lakini hapingi majaribio ya maafisa kuchukua udhibiti chanya wa kimwili juu yao.

(3) Mkaidi na mtukutu bila madhara (Active resistor)- mtu ambaye hafuati amri za maneno, anapinga majaribio ya afisa kuchukua udhibiti chanya wa kimwili juu yao, lakini hajaribu kumdhuru afisa.

(4) Mkaidi na mtukutu mwenye madhara (Active aggressor)- mtu ambaye hafuati amri za maneno, anapinga majaribio ya afisa kuchukua udhibiti chanya wa kimwili juu yao na anajaribu kusababisha madhara kwa afisa au wengine.

Kwa ujumla, watu wasio na msimamo na wapinzani hai huanguka chini ya viwango vya 1-3 vya matumizi ya nguvu, huku wavamizi hai huanguka chini ya viwango vya 4-6.

Maafisa wa jeshi na polisi wamefunzwa kutumia kipimo sahihi cha nguvu ndani ya mfululizo kulingana na vitendo na uainishaji wa mtu huyo.

Licha ya ukweli huu wa kisheria, kulingana na kile kilichotokea wakati wa wiki ya uchaguzi, ni wazi kwamba, sera ya muda ya usalama iliundwa na ilitawala shughuli za usalama.

Sera hii, inaonekana, ilihitaji kwamba waandamanaji washughulikiwe chini ya "mfumo wa makabiliano ya kijeshi," ambapo waandamanaji hutendewa kama wapiganaji wasio na haki ya kuishi.

Mbinu hii inapingana na "mfumo wa makabiliano ya kipolisi," ambapo mkosaji lazima azuiliwe kisheria na kushtakiwa katika mahakama ya kiraia, badala ya kuuawa kwa kupigwa risasi za moto.

Hakukuwa na tangazo la vita wala tangazo rasmi la hali ya hatari. Kwa hivyo, mauaji yaliyotokea katika wiki ya uchaguzi ni "mauaji haramu kisheria" yaani "extrajudicial killing."

Maana ya “mauaji haramu kisheria” yaani "extrajudicial killing"

Kulingana na Profesa William J. Aceves (2018), katika makala yake, "When Death Becomes Murder: A Primer on Extrajudicial Killing," iliyochapishwa katika jarida la Columbia Human Rights Law Review, Toleo la 118 Juzuu ya 50, kuanzia 117-184, fasili bora ya “extrajudicial killing”, yaani “mauaji haramu kisheria,” ni kama ifuatavyo:

"Kwa mujibu wa fasili rasmi, mauaji haramu kisheria hutokea wakati ambapo: (1) afisa wa umma au mtu mwingine anayetenda kwa kuchochewa au kwa ridhaa au kukubaliwa na afisa wa umma au mtu mwingine anayetenda kwa nafasi rasmi; (2) ambaye matendo yake yalikuwa ya kukusudia au ya uzembe; (3) na yakasababisha kifo kimoja au zaidi; (4) na ambaye alijua au angepaswa kujua kwamba kifo kinaweza kutokana na matendo yake; (5) na ambaye alishindwa kuzingatia viwango vyovyote vinavyohusiana na matumizi ya nguvu, ikiwa ni pamoja na kanuni za umuhimu, utofauti, uwiano, na tahadhari; (6) na ambaye matendo yake hayakuidhinishwa na mchakato wa kimahakama kwa mujibu wa kanuni za utawala wa sheria." (uk. 144-45).

Yaani:

“By definition, an extrajudicial killing occurs when: (1) a public official or other person acting at the instigation of or with the consent or acquiescence of a public official or other person acting in an official capacity; (2) whose acts were intentional or negligent; (3) and resulted in one or more deaths; (4) and who knew or should have known that death may result from their acts; (5) and who failed to comply with any relevant standards regarding the use of force, including the principles of necessity, distinction, proportionality, and precaution; (6) and whose acts were not authorized by legal process orcomplied with the rule of law.” (p. 144-45).

Ni maoni yangu kwamba, kwa mujibu wa fasili hii, Rais Samia na wasaidizi wake katika vyombo vya ulinzi na usalama wanayo kesi ya kujibu mbele ya mahakama za kimataifa.

Sasa tunafahamu kwamba, watekelezaji walikuwa ni watu wamevaa nguo za kiraia. Watanzania na wasio watanzania walihusika. JWT wakajikuta katikati ya mapolisi na mamluki wa kigeni.

Kutokana na ushahidi ambao umeanza kuvuja kupitia picha za siku ya tukio, sasa inaonekana kuwa Watanzani wengi wa aina hii walitoka kitengo cha ulinzi wa Rais, yaani Presidential Security Unit (PSU).

Lakini, baadhi ya watu hawa walitambulika kuwa Waganda, wengine walitoka Zambia, na baadhi walitoka Zanzibar.

Tarehe 31 usiku, katika kikao kilichofanyika makao makuu ya Jeshi Upanga, maswali mengi yalielekezwa kwa Mkuu wa Majeshi (CDF) bila kupatiwa majibu.

Nani aliruhusu nchi yetu kuvamiwa na majeshi ya kigeni? Amiri Jeshi Mkuu alipata wapi mamlaka ya kukodi majeshi? Walikuja kufanya nini?

Kama wageni walikuja kumsimika Rais Samia, tena baada ya umma kukataa kumpigia kura Rais Samia, Rais Samia ni Rais wa Watanzania?

Kwa hiyo, ni lazima Rais Samia aliongelee jambo hili kwa ukamilifu. Wala halihitaji kuundiwa Tume, maana yeye anajua kila kitu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka jeshini, yeye Samia alimwambia CDF kuwa "nimeamua kukuongezea nguvu kutoka nje". Mpaka hapo hakuna haja ya kuchunguza jambo hili. Majibu yako mezani.

Kwa ujumla, mtu anayeelewa tofauti kati ya “armed conflict paradigm of security management” na “law enforcement paradigm of security management,” na aliyeona kilichotokea kati ya tarehe 29 Oktoba 2025 na 03 Novemba 2025, hawezi kukubali kuendelea kuongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

9. Hitimisho na Mapendekezo

Kwa ufupi, ni hitimisho langu kwamba, Tanzania hatuna Mkuu wa Nchi, hatuna Amiti Jeshi Mkuu, na hatuna Rais kwa sababu moja tu: Samia Suluhu Hassan ni tishio namba moja kwa usalama wa Taifa la Tanzania.

Anataka kuwa rais wa yatima, wajane na familia zenye majonzi ya kudumu, lakini hilo haliwezekani.

Hivyo, Samia Suluhu Hassan anapaswa kufahamu kuwa Watanzania wengi wanataka yafuatayo yafanyike haraka:

  • Katiba mpya yenye kutamka serikali moja au serikali tatu.
  • Tume huru ya uchaguzi
  • Kurudiwa kwa uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani
  • Kufutwa kwa kesi za uhaini hewa zilizobuniwa kabla, wakati ba baada ya 29 Oktoba 2025.
  • Wahusika waliotekeleza mauaji wa Waandamaji watafutwe, wakamatwe na kufikishwa kwenye mahakama.
  • Rais Samia awajibike kwa kujiuzulu ili kulinda Usalama wa Taifa la Tanzania.
  • Makamu wa Rais aongoze kipindi cha mpito kuelekea katiba mpya na hatimaye uchaguzi wa haki.

 

Attachments

Back
Top Bottom