Taharuki iliyopo sasa vyuoni kuhusu HESLB

Taharuki iliyopo sasa vyuoni kuhusu HESLB

Clark boots

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2017
Posts
6,770
Reaction score
6,202
Ndugu wadau wa elimu habarini za mda huu,

Tangu kuanza kwa wiki hii inayoelekea weekend kumetokea na taharuki kubwa kwa vyuo mbalimbali hapa Nchini na inaendelea hadi da huu wanafunzi wengi tuko midomo wazi.

Issue iko hivi, baada ya vyuo kufunguliwa na wanafunzi kuanza masomo bodi ya mikopo ilianza kutoa Allocations zote kwa wanafunzo wanaoendelea na masomo(Continues), sasa cha kushangaza mpaka mda huu Luna baadhi ya wanafunzi hawajapata message za boom kwenye simu zao wala hela hata shilling 100.

Licha ya wachache kupata message za pesa na kufanikiwa kuverify bado pesa na viandikwa bado wanafunzi hawajapata yaan unatumiwa message zote za MA & BS alafu ukiverify inaingia hela ya boom tu.

Sambamba na hilo, kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo inaonesha dhahiri kuwa àllocation zetu za ada zimepunguzwa, nasema hvyo kuwa zimepunguzwa kwanini?

Kwa sababu mwaka Jana bodi ilivyotoa mikopo kwa wanafunzi walikuwa wanaonesha allocation za miaka yote kulingana na duration ya program husika, sasa ni jambo la kushangaza nakusikitisha mtu umeona toka mwaka Jana kuwa nikifika mwaka wa pili nalipiwa pesa yote ya ada alafu sasa hivi nakuta pesa imepunguzwa nalipiwa laki saba.

Binafsi Nipo chuo ni mwezi sasa ila sijapata message ya booms mpaka leo wala Kierkegaard's a hata mia kwenye account yangu ya bank. Kwenye upande wa tuition fees ndo wamepunguza kabisa hadi watu wanalia.

Jana kuna girl mmoja alikuwa analia kabisa maana hajui atasomaje bila hela ya ada. Mwaka Jana ilionesha atalipiwa pesa zote za ada kwa 100% miaka yote Leo hii anakuta allocation ya boom pekee ada ajilipie mwenyewe.

HESLB popote mlipo tunataka maelezo ya kina kuhusu haya mauzauza mnayotufanyia sababu mini, kwani tuliwalazimisha pale mwaka Jana kutuonesha allocation za miaka yote mi3? Ni bora mngetuchinja tu kama mlivyowachinja ndugu zetu hapa mwaka huu kwa kuwa 20% kuliko haya mnayotufanyia maana tungelijua moja na kama mm nisingejisumbua kuja kabisa chuoni ningelifanya mambo yangu.

Kwa hiki mlichokifanya na kama bado kitaendelea kuwa serious basi mtegemee wanafunzi wengine kuacha vyuo bila kujali wako mwaka wa ngapi.. Maana bila ada watu watasomaje? Booms zenyewe mnatoa nyie mnajisikia kana kwamba ni pesa za familia.
Yaaan mambo ni mengi ila hebu niishie hapa

HESLB sio watu kabisa,,, mpaka leo watu hatujapata booms zetu hali ya kuwa tumefaulu vizuri na uongozi wa chuo unatuambia matokeo yetu yalishatumwa kwenu kitambo tu...!!
 
Wenyewe wanasema anaupiga mwingi kwani wanufaika mikopo mwakaa huu ni wengi kuliko wote waliopata awamu 5 yote yaani miaka 5 yote ye kaifunika kwa miezi sita tu wanufaika sijui 32 elfu wakati awamu ya 5 yote ilitoa kwa wanafunzi 29 elfu.

Shida inakuja anataka kuiga aonekana amefanya ya maana sana ila ndo hivo banah na usishangae mtoto wa Wasiri akaanza kupata mkopo tena na ukawa 100%.

Wanasema wenye nchi wameshika nchi yao sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nani kakuambia? Safari kama una mtu chuo jiandae kulipa ada wanapunguza ilikradi tu wanekane wanufaika wengi apigie kampen 2025.

Sent using Jamii Forums mobile app
kwani hao watu wanaopunguziwa ni raia wa nchi gani mpaka warubunike na mpango huu. Hii mbinu si salama kabisa katika siasa zao
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wengine wazazi wameshazoea kulipa ada, HELSB mpooooo?
 
allocation za mwaka wa tatu si hadi wabandike?
Kinachobandikwa ji kilekile kinachooneka kwenye SIPA account, thus way wanatoa booms kwa mafungu yaan vile wanajisikii..?
 
Wewe uko chuo cha kata..mbona watu wana zaidi ya wiki boom limetoka na allocations wamezipata.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ilipotokea Kwa first year mlikua mnawacheka kumbe upepo unawapitia na nyie
 
Nilizani ni kwetu tu udsm kumbe kote basi mwaka huu ni wa hovyo kuliko miaka yote
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wengine wazazi wameshazoea kulipa ada, HELSB mpooooo?
kama kweli hela ya kumlipia mtoto ipo hakuna haja kabisa ya mkopo. Huwa mzigo mkubwa wakati wa marejesho.
 
We Jamaa unaongea Nini asee, chuo Cha kata ndo chuo gani?? MTU anaongea kwa experience afu unajibu pumba hata hapa UDOM-Coed Hali Ni hyohyo haya wewe uliepo chuo Cha mkoa kaa kimya Basi.
Wewe uko chuo cha kata..mbona watu wana zaidi ya wiki boom limetoka na allocations wamezipata.

#MaendeleoHayanaChama
 
kama kweli hela ya kumlipia mtoto ipo hakuna haja kabisa ya mkopo. Huwa mzigo mkubwa wakati wa marejesho.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nawaona ccs/brthrs wanavohaha na deni lao, miaka yote haliishi tyuuh. Khaaaaah
 
Back
Top Bottom