Rais Samia aidha washauri wake wamemshauri vibaya au hajali Elimu. Sijui lipi kati ya hilo linatawala, maana haiwezekani ukajali elimu ya wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa kuzalisha pesa nyingi za TOZO na kuwajengea madarasa halafu wakifika chuo kikuu udharau nguvu yote uliyeijanga kwa msingi imara.
Hali ni mbaya sana vyuo vikuu vyote, wanafunzi karibu wote wameshikwa na majonzi, vilio, masikitiko na hasira nchi nzima. Rais Samia S S Ajue kuwa anawatesa wanawake wenzake, kwani akina dada vyuo vikuu sasa ni ruksa kujiuza ili wapate mlo wa siku. Kama hivi ndivyo anavyotaka, basi akina mama wajue gharama ya kuwa na Rais Mwanamke. Ni bora angeendelea na ule mfumo ambao Rais Magufululi aliuweka, kuliko hali ilivyo hivi sasa. Ondoa huyu Mwigulu anakuharibia. Kwani lazima ubadili yote Magu aliyoyafanya ndio ujulikane kuwa wewe ni Rais bora.
Kimsingi hii ni system mbaya kabisa kuwahi kutokea tokea mpango wa mikopo kwa wanafunzi kuanzishwa. Mpango wa Kikwete ulizingatia umuhimu wa kozi, wa Magu - hali ya uchumi wa familia sasa huu umezingatia nini? Kama anafanya kampeni kwa kudhani kuwa wanafunzi wa kidato cha kwanza ni wengi hivyo familia nyingi zitaguswa na kumchagua ukilinganisha na hawa wa chuo kikuu, basi ni kampeni chafu sana.
All in All Mama hapa kalikoroga. Tena kajichafulia sana. Wanafunzi tuendelee kulivalia njuga hili suala. Nyerere alisalimu amri kwa akina Sita, Mwinyi alichokipata UDSM hakisahau, Kikwete anafahamu shida aliyoipata na wanafunzi kwa kuwacheleshea boom lao, Magu akarekebisha leo Mamam anatikisa kiberiti. Ahhhh...............Kimejaaaa.