Wadau hebu niwaeleze kitu maana mwanzo nilikuwa sijapata info kamili..
Kiukweli kwenye account yangu ya HESLB ilikuwa inagoma kufunguka siku za nyuma ila leo hii imekubali na nimefanikiwa kuona allocations zangu za mwaka huu.
Sasa issue iko hv,allocation za mwaka huu wamezileta kama za mwaka Jana,, yaan first year kama ulipata ada 60% bac ipo hyohyo 60%. Ila uhalisia ni kwamba mwaka jana ziliwekwa allocations za miaka yote na ilikuwa inaonesha kila mwaka pesa inaongezeka..
Nasikitika kuwa bodi wàmeondoa hela zote muhimu kwa mwanafunzi kama BS, SFP, FTP.Kwahyo tutembee tu na allocation za mwaka Jana kama ulikuwa unaongezea laki 2 kwenye ada basi utaendelea kuongezea hvyohvyo.
Ila kuhusu boom bado ni changamoto mpaka leo hii wanafunzi wengi hatujapata boom, boom wanatoa kidogokidogo kama keki ya birthday vile.