Taharuki iliyopo sasa vyuoni kuhusu HESLB

juzi nilikuwa Dodoma, pamechafuka wanafunzi afu wengine inaonekana bado washamba wametoka kijijini kabisa, wale wahuni ndo wanavaa vibayaa, hadi nawaonea huruma. bodi ya mikopo kwakweli inatakiwa kuwaangalia hawa watoto kwa jicho la pili, hawatakiwi kusoma kwa shida hivi, na kwa jinsi walivyo kata wafanyakazi wengi hadi leo wanakata, na serikali tunasikia huwa inapiga ngumi, si muwalipe watoto wasome shule? binafsi najua uchungu wa kusoma bila pesa kutokana na familia niliyotoka, watoto wapo hapa wamepigwa na jua na udom wanatembea umbali mrefu toka jengo hadi jengo wanaonekana wanatia huruma mnoo.
 
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kama una watu wako humu naomba hivi "Ondoa viongozi wote uliorithi kwenye Taasisi zote za umma weka wa kwako. Unachezewa mchezo mbaya kila mahali maana kuna fundo kubwa la chuki za kwa nini hayupo tena hai. Kuna genge kubwa limeshikilia hatamu kuhakikisha unapoteza Imani Kwa wananchi. Wamejipanga kuharibu huduma muhimu na tumeshaanza kujionea. Matumaini ya wananchi kwako yamekuwa miembamba Sana Sana. Ninakuombea timu yako itafakari hili. Mama amka. Ninakupenda na tunakupenda".
 
kidogo gawana na nduguzo, watu gawaneni kidogo kidogo ilimradi kila mtu apate chochote kitu. Kuliko kuwapa kingi kundi dogo la watu huku ukiwaacha wengine hoi taaban kifo cha mende. Najua inaumiza lakini ndiyo uhalisia huo, katika upimaji wa huyu tumpe ngapi na huyu ngapi bila documents ni kazi sana. Nafikir kwa wale wote waliotuma documents stahiki wamepata kulingana na vigezo na masharti. Na pengine tuje na mbinu mbadala nini kifanyike katika mchakato huu na si kulalama tu na kukosoa.
 
We Jamaa unaongea Nini asee, chuo Cha kata ndo chuo gani?? MTU anaongea kwa experience afu unajibu pumba hata hapa UDOM-Coed Hali Ni hyohyo haya wewe uliepo chuo Cha mkoa kaa kimya Basi.
Ndo maana nimemtukana Huyo.. Hawezi kuleta mambo ya kijinga kwenye vitu serious.. Utotoutoto apeleke huko kwa mama wake
 
Hapa pana ukweli kabisa
 
Kaka kwa icho kidogo wengine hawawezi kuongeza ikawa ada yote bora wangeendelea na mfumo ule ule wengine wapate wengine wakosa huo ndo mfumo wa maisha....kwa mifano kuna watu kibao watashindwa kwenda chuo coz of ada kuimalizia imagine mtu kapewa laki250 kwenye ada ya mil 1.55k we unazani iyo hela nyengine ataokota wap?
 
Ni kweli kabisa lakini hakuna namna inabidi ndugu wajichange. Angalau wanakuwa wamepunguza kitu kwa hela ya kujikimu chuoni
 
Rais Samia aidha washauri wake wamemshauri vibaya au hajali Elimu. Sijui lipi kati ya hilo linatawala, maana haiwezekani ukajali elimu ya wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa kuzalisha pesa nyingi za TOZO na kuwajengea madarasa halafu wakifika chuo kikuu udharau nguvu yote uliyeijanga kwa msingi imara.

Hali ni mbaya sana vyuo vikuu vyote, wanafunzi karibu wote wameshikwa na majonzi, vilio, masikitiko na hasira nchi nzima. Rais Samia S S Ajue kuwa anawatesa wanawake wenzake, kwani akina dada vyuo vikuu sasa ni ruksa kujiuza ili wapate mlo wa siku. Kama hivi ndivyo anavyotaka, basi akina mama wajue gharama ya kuwa na Rais Mwanamke. Ni bora angeendelea na ule mfumo ambao Rais Magufululi aliuweka, kuliko hali ilivyo hivi sasa. Ondoa huyu Mwigulu anakuharibia. Kwani lazima ubadili yote Magu aliyoyafanya ndio ujulikane kuwa wewe ni Rais bora.

Kimsingi hii ni system mbaya kabisa kuwahi kutokea tokea mpango wa mikopo kwa wanafunzi kuanzishwa. Mpango wa Kikwete ulizingatia umuhimu wa kozi, wa Magu - hali ya uchumi wa familia sasa huu umezingatia nini? Kama anafanya kampeni kwa kudhani kuwa wanafunzi wa kidato cha kwanza ni wengi hivyo familia nyingi zitaguswa na kumchagua ukilinganisha na hawa wa chuo kikuu, basi ni kampeni chafu sana.

All in All Mama hapa kalikoroga. Tena kajichafulia sana. Wanafunzi tuendelee kulivalia njuga hili suala. Nyerere alisalimu amri kwa akina Sita, Mwinyi alichokipata UDSM hakisahau, Kikwete anafahamu shida aliyoipata na wanafunzi kwa kuwacheleshea boom lao, Magu akarekebisha leo Mamam anatikisa kiberiti. Ahhhh...............Kimejaaaa.
 
Mara huku TANESCO umeme kila baada ya dakika mbili unakata
 
Elimu ni gharama siyo bongo tu hata ulaya.
So kama ni gharama sisi watoto wa masikini tusisome wasome watoto wa machief(matajiri) sio? Ama kweli aliyeshiba hamkumbuki mwenye njaa
 
jaman sisi wengine hta allocation ya mwaka huu hatujapata bado na mkopo tulipata mwaka jana...mpk xx hatuelewi na hatujui hatma..hv hawa bodi ni vipi kwan??.
 
So kama ni gharama sisi watoto wa masikini tusisome wasome watoto wa machief(matajiri) sio? Ama kweli aliyeshiba hamkumbuki mwenye njaa
Siyo mapenzi yangu ila ndivyo dunia ilivyo, wanasema masikini hana haki.
 
jaman sisi wengine hta allocation ya mwaka huu hatujapata bado na mkopo tulipata mwaka jana...mpk xx hatuelewi na hatujui hatma..hv hawa bodi ni vipi kwan??.
allocation za wanufaika kwa mwaka wa pili na tatu zitatumika zile allocation za mwaka wa kwanza. Hivyo jikadilie kwa mwaka wako wa kwanza ulipataje.
 
Pesa za tozo siyo zilizotumika katika ujenzi wa madarasa. Halafu tukisema kauli zako ni za uchonganishi baina ya raisi na wananchi wake utakataa. Kuna watu hukosa mikopo kila mwaka hivyo wamejaribu kufikia kundi kubwa kwa namna hii.
 
Hivi we Jamaa unaelewa kweli kinachozungumziwa hapa, yaan unaonekana Kama umefikia kucomment bila kusoma Uzi.
allocation za wanufaika kwa mwaka wa pili na tatu zitatumika zile allocation za mwaka wa kwanza. Hivyo jikadilie kwa mwaka wako wa kwanza ulipataje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…