DOKEZO Taharuki yazuka, Wazazi wajaa Shule ya Msingi Ubungo NHC baada ya taarifa kuwa shule inauzwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mama Mitano tena, kwenye kila maendeleo kuna watu wata umizwa na watakao shangilia, ila kwa hili ni heko kwa serikali yangu bomoa tujenge upya. Tusipende lalamika sana kila kitu kwetu tunaona tuna onewa, maboresho mengine yana kwenda kwa garama kubwa. ifike mahali tuache kuamini Free education, free medical care, free homes etc Hakuna bure zaidi ya maziwa ya mama. Tujifunze kupambana na kuongeza bidii kila kitu bora na kizuri ni pesa. Hakuna elimu bora bila pesa. Wapo watu kibao wametoka hizi shule za kayumba wakawa watu mashughuri ila bado sio kigezo cha elimu bora. Elimu bora ni pamoja na madara ya kisasa, mazingira salama, walimu wa kutosha, chakula bora, vitabu na mitahala bora. Sasa kama tuna boreshewa tuna anza lalamika ni lini Watanzania wata anza amini karne zimebadilika vya bure ni garama hakuna vitu vya bure duniani? Mtegemea cha nduguye hufa maskini. Tafakari
 
Peleka mtoto hapo Mugabe acha kelele ambazo hazisaidii,Serikali imeamua kubadili shule iwe ya kiingereza huoni ni maendeleo hayo?Kwa maana nyingine mdogo wake na huyo utampeleka hapo asome kwa kiingreza.
Kingereza ndio maendeleo. Nchi za Afrika wanazoongea kingereza wanamaendeleo gani ? Huko chuo kikuuu ndio mlivyofundishwab? Andiko gani linasema kingereza ni maendeleo.Mnasikitisha sana ila ni wa kuwahurumia tu.
Watu wangwpi TZ wanaojua hicho kingereza wanakiongea ? Zaidi ya mashuleni hicho kingereza kinaongewa wapi ? Hio ni lugha ya makaratasi haina maendeleo yoyote. Badala ya kukuza lugha yako andelea kukuza lugha za wazungu.
Halafu kingereza mnachoongea wala wazungu hawakielewi ni bora mngekiacha tu
 
Tulipofika shuleni leo, tumeambiwa kuwa shule inavunjwa na badala yake itabadilishwa kuwa English Medium.😂
Kuna siku tutauzwa kama tulivyo
Mshana hujaona msg hapo juu eti kingereza ni maendeleo. Kuna wanatamani hata mtaani kiswahili kipigwe marufuku.
 
Hapo usikute kuna mwekezaji anataka kujenga godown la ghorofa 10 kwa ajili ya kituo cha kimataifa cha biashara Ubungo.
 
Hahahaha.
Ukitaka kujua kama kiingereza tunachofundishwa sisi wabongo tunaingizwa chaka siku mtafute Mzungu halafu ibuka naye shuleni uone walimu wa kiingereza watakavyojikanyaga.
 
Hahahaha.
Ukitaka kujua kama kiingereza tunachofundishwa sisi wabongo tunaingizwa chaka siku mtafute Mzungu halafu ibuka naye shuleni uone walimu wa kiingereza watakavyojikanyaga.
Unasema nini mkuu mie nilikuwa nakuea mc na mkslimani wa wazungu wa misaada. Aisee kingereza chetu wazungu wanaitikia mara tatu tatu hawakuelewi ila wabongo wanajifanya eti wanajua.
 
Peleka mtoto hapo Mugabe acha kelele ambazo hazisaidii,Serikali imeamua kubadili shule iwe ya kiingereza huoni ni maendeleo hayo?Kwa maana nyingine mdogo wake na huyo utampeleka hapo asome kwa kiingreza.
Kumbe kubadili shule na kuwa ya Kiingereza ni maendeleo???

Kwa nini Sasa wanachagua shule za kuzibadili na kuwa za Kiingereza badala ya kubadili shule zote kabisa zilizopo hapa Tanzania ili ziwe za Kiingereza???
 
Ndo tumefikia huku sasa kama nchi hii hali sio nzuri tunapoelekea kubaya
Hadi shure ya uma
Inamaana hapo kuna kibopa analitaka hilo eneo dah
Hahaha!!! China International Complex Mall
Kumbe Kiingereza kinaeleweka kikifundishwa kwenye shule mpya siku hizi.
Yote kwa yote: Iwe heri, na taarifa rasmi ni muhimu. Idara ya Elimu ni maafisa kibao, sio vyema akosekane hata msemaji rasmi mmoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…