DOKEZO Taharuki yazuka, Wazazi wajaa Shule ya Msingi Ubungo NHC baada ya taarifa kuwa shule inauzwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Imeuzwa kweli hiyo tayari!
 
Wazazi mmeitwa kwenye kikao, halafu wahusika hawapo!
Haya, mshukuruni mama Kisha rudini kwenu!
 
Haivunjwi ila itakuwa inatumia lugha ya kiingereza TU! Tena mfurahi watoto wenu watajua kiingereza! Tz ni nchi ya hovyo sana, nchi zote 54 zilizotawaliwa na mwingereza ni Tanzania TU haitumii kiingereza kuanzia nursery mpaka chuo kikuu!
 
Peleka mtoto hapo Mugabe acha kelele ambazo hazisaidii,Serikali imeamua kubadili shule iwe ya kiingereza huoni ni maendeleo hayo?Kwa maana nyingine mdogo wake na huyo utampeleka hapo asome kwa kiingreza.
Ata pale mwanza kuna shuke serikali ili badili saivi ni english medium walio jiweza waka endelea wasio jiweza waka amishiwa shule jirani ya kawaida
 
Hii ni video ikionyesha wazazi wakiwa na taharuki
Your browser is not able to display this video.
 
Eneo la shule kubadilishwa matumizi sio ishu jambo la msingi ni wanawahamishia wapi
 
Mkuu yote sawa, kwa hao watoto wao hawana haki ya kuboreshwa???

Kwani hao watoto hawana haki ya kujua Kiingereza???

Kwanini wasipewe kipaumbele???

Mkuu serikali inapojenga majengo mapya au kukarabati shule nyingine huwa inahamisha wanafunzi???

Kuna maswali mengi kuliko majibu. Loliondo in Dar!!!
 
Wameuza Loliondo na Bandari zetu sembuse shule?
 
Swala la muda, wneo potential sana ilo. Wakienda likizo December hawarudi. January wote waende Mugabe.

Maendeleo hayana chama.
 
PPP
 
 

Attachments

  • 354506.jpg
    14.5 KB · Views: 2
Nakubaliana na wewe sana mkuu ila mambo mengine yana maana ilio jificha, vitu vingine kama watanzania tuna jitakia, wanao fanya hayo tumewapa dhamana sisi, wanao takiwa kutusemea tumewapa dhamana sisi. wakati wa kulia tuna lia na kulalamika sisi wakutusemea ana kuwa hayupo tena. Je nani ame tuloga watanzania? Tafakari kz walio wengi bado wamelala usingizi mzigo tuna shabikia zaidi kuliko kufanya maamuzi ya maisha yetu ndio mana tuna tumika na kutupwa kama hivi. So wacha watu wale mwarubaini wao mpaka pale wata amka wakute safari ina endelea ukitaka kwenda mbali nenda mwenyewe ukitaka kusogea sogea wewe nenda nao wote matokeo ndio haya sasa. Kesho hata nikisikia Yanga wamenunua hilo eneo wana jenga uwanja sawa tu maana bado tulio wengi hatujui wajibu wetu.
Conclusion; wacha tulio wapa dhamana watu buruze mpaka pale tuta pata akili kuwa bila sisi wao ni hakuna.
 
Ngoja na mimi niende kuandamana, nimesoma hapo miaka 31 iliyopita, enzi za mwalim mkuu banda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…