Taifa Bila Vyombo vya Habari Huru na Imara ni Taifa Mfu. Gazeti la MwanaHalisi Lisamehewe Kuandika Ukweli?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
59,804
Reaction score
134,593
Wanabodi,
Hii ni makala yangu kwenye gazeti la Mwananchi la leo, ambapo nimeibua hoja 4 nikiuliza kama wajua kuwa Taifa lisilo la mhimili wa Nne ulio huru na imara ni kama taifa mfu kwasababu ile mihimili mitatu ya Serikali, Bunge na Mahakama, itakuwa huru kujivinjari na madudu ya kila aina, huku hakuna yeyote anayeyaibua madudu hayo. Na kitendo cha Watanzania kufanyiwa madudu ya ajabu, huku wamenyamaza kimya na kutulia tuu bila kuuliza lolote, ni kuwa ni tumekuwa kama mazuzu!. Mazuzu ni majitu ambayo unaweza kuyafanyia kitu chochote cha ajabu ajabu, na yenyewe yanakuwa yametulia tuu, as if nothing happened!. Kilichomtokea makamu wao wa rais waliyemchagua, kujiuzulu ghafla, bila kutoa sababu, kisha kufutwa uanachama wake wa chama chake kinyume cha katiba ya JMT, bila kuelezwa sababu au bila wao kuambiwa makosa yake, huku wametulia tuu, hakuna yeyote anayeuliza chochote, wala kujua mahali mtu huyo alipo, yuko na hali gani, ni maisha tuu yanaendelea as if nothing happened, huu ni uzuzu!. Uzuzu huu, unasababishwa na kutokuwepo mhimili wa 4 huru na imara. Tungekuwa na mhimili wa 4 huru na imara, saa hizi ungekuwa umeishafanya IJ ya kujua VP alifanya makosa gani, Watanzania by now wangekuwa wanajua what really happened, wangekuwa wanajua saa hizi yuko wapi na ana hali gani!. Mwisho nimetoa wito kuwa japo gazeti la Mwanahalisi limefungiwa kwa kuandika habari bila mizania, nimeshauri gazeti hilo lisamehewe kwasababu kitu ilichokiandika ni kitu cha ukweli, kosa la ukosefu wa mizania ni kosa dogo ukilinganisha na ukweli ulioibuliwa na Mwanahalisi, au kwa vile sisi ni mazuzu, hivyo hili gazeti liendelee tuu kufungiwa kwa kufanya makosa ya kizuzu, ili liwe fundisho kwa vyombo vingine vyote vya habari visifanye makosa ya kizuzu!, ni bora Taifa la Tanzania kuwa taifa la mazuzu waliotulia, kuliko kuwa taifa la watu informed wanao uliza uliza na hoji hoji mamlaka vitu ambavyo hawapendi vijulikane!.
mhimili wa nne.jpg

Nchi nyingi duniani, huendeshwa kwa mihimili mitatu rasmi, Serikali, Bunge na Mahakama, lakini pia kuna mhimili wanne, ambao ni Mhimili usio rasmi, huu ni mhimili wa Habari, The Media, ambao kwa nchi za wenzetu unaitwa “The Fourth Protocol, au The Fourth Estate”

Jukumu kuu la msingi la uandishi wa habari ni upashanaji wa habari, kwa nia ya kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha, ila jukumu la media kama mhimili ni kuwa mlinzi wa jamii husika “watchdog of the society” kwa kutoa habari kutoka ile mihimili mitatu rasmi na kuwafikishia wananchi na jamii, na wakati huo huo kutoa habari za kinachotokea kwenye jamii na kuwafikishia mamlaka, kiingereza wanaita a two way traffic.

Ili mhimili huu wa media au fani hii ya uandishi wa habari, iweze kutekeleza majukumu yake ya uhimili kikamilifu, inahitaji watu sio tuu wenye ewezo wa kusomea fani ya uandishi wa habari ili kupata sifa za kuwa mwandishi wa habari, fani hii inamuhitaji mwandishi wa habari kuwa na kipaji cha kuwa na pua yenye uwezo wa kunusa habari , inaitwa “nose for news”

Hii “nose for news” ni uwezo wa kuinusa habari fulani na kuiandika kabla haijatokea. Waandishi wenye pua kali, yenye uwezo huo, ndio wale wenye uwezo wa kuandika habari za uchunguzi, “investigative journalism, IJ”, yaani kuibua habari, ambapo kwa vyombo vya habari vya Tanzania ya sasa, hili halifanyiki sana, kwasababu, nyingi ya habari za uchunguzi, mwisho wake huwa zinaibua madudu ya mamlaka hivyo ama chombo cha habari kinashukiwa, ama mwandishi wa habari za uchunguzi anashukiwa, ama wote wawili mwandishi na chombo chake wanashukiwa, wanasulubiwa!.

Kashfa nyingi zimeibuliwa na waandishi wa habari za uchunguzi, zikiwemo kashfa maarufu ya Loliondo iliyoibuliwa na mwandishi wa habari Stan Katabalo wa gazeti la Mfanyakazi, kashfa ya IPTL, kashfa ya Escrow, kashfa ya Richmond iliyomng'oa Waziri Mkuu , Edward Lowassa madarakani, na kashfa nyingine mbalimbali.

Ni mwandishi Saed Kubenea na gazeti lake la Mwanahalisi, kupitia Toleo No. 571 la Agosti 6 hadi 12, 2026, lenye kichwa cha habari "Nchimbi agoma kujiuzulu"ndie aliyeibua hii kashfa ya sasa ya kuondolewa kwa Makamu wa Rais Balozi Dr. Emmanuel Nchimbi madarakani kwa kutumia chanzo fiche ndani ya kikao cha NEC.

Idara ya Huduma za Habari (MAELEZO) ikasitisha leseni ya gazeti la MwanaHALISI kwa miezi sita (6) kuanzia tarehe 19 Agosti, 2026 kutokana na kukiuka sharti la 3 katika Leseni ya machapisho linalovitaka vyombo vya habari kuzingatia Sheria ya Huduma za Habari (Sura 229) na Kanuni zake (2017)

Taarifa ya Maelezo ilisema Taaluma ya uandishi wa habari ni taaluma adhimu na inayohitaji kutumiwa kwa umakini na uangalifu wa hali ya juu ili kuepusha upotoshaji na kuhakikisha jamii inapata habari sahihi, za ukweli na ambazo kutafutwa, kuchakatwa na kuchapishwa kwake kumezingatia Sheria, Ka-nuni, weledi na misingi ya taaluma ya uandishi wa habari inayotumika kote duniani.

Kosa la Mwanahalisi ni kutokuweka uthibitisho mahali popote alipochukua jitihada za ku-wahoji hata mmoja wa viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) au watu waliokuwa wajumbe wa kikao hicho, mathalani, Katibu Mkuu, Katibu Mwenezi au Afisa Habari wa Chama cha Mapinduzi (ccm), ili kuthibitisha hayo yanayodaiwa kuwa yalijadiliwa katika kikao hicho, baada ya kuwa ameambiwa na vyanzo fiche.

Sifa kuu ya chombo cha habari makini ni kutafuta ukweli, kusema ukweli, kuandika ukweli na kutangaza ukweli, seek the truth and the truth will set you free, kanuni kuu ya uandishi wa habari, cardinal rule ni "tell nothing but the truth".

Sasa kwa vile yote gazeti la Mwanahalisi waliyo yaandika, kuhusu Nchimbi kugoma kujiuzulu, hatimaye yamekuja kutokea kweli, Makamu Rais kujiuzulu, na kitendo cha kufutwa uanachama wa CCM, ni uthibitisho kuwa mwanzo aligoma kujiuzulu, hivyo hata baada ya kujiuzulu, kitendo cha CCM kumfutia uanachama wake, ni uthibitisho tosha ameadhibiwa kwa kufutwa uanachama wake wa CCM, japo CCM haikutoa sababu, Gazeti la Mwanahalisi lilisha andika sababu.

Gazeti la Mwanahalisi, ndilo gazeti pekee linaloandika habari za uchunguzi, kitendo cha kuendelea kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi, kumewakosesha Watanzania hata kujua tuu kosa la aliyefutiwa uanachama!, gazeti hilo lingekuwepo, saa hizi taifa lingeishahabarishwa makamu rais mstaafu saa hizi yuko wapi, hivyo kupunguza taharuki ya nini kimempatsa. Kulifungia gazeti pekee la IJ, ni kaburi la habari za kiuchunguzi Tanzania.

Hivyo, natoa wito kwa Idara yetu ya Habari Maelezo, japo ni kweli gazeti la Mwanahalisi limefanya makosa ya kuchapisha habari isiyokuwa na mizania, lakini kwa vile kilichoandikwa, kimekuja kutokea kweli, gazeti lisamehewe huku tukiendelea kupigania kuundwa kwa Baraza Huru la Habari.

Mungu Ibariki Tanzania.

Mzee Pasco.
 
View attachment 3666303

Mzee P,alaaniwe alianzisha mfumo wa kupora press card,fine kuwa kubwa,fungia chombo na Sheria haramu za habari na wanaozilinda.
 
Ukimtetea mwanahabari mwisho wa siku utajikuta uko peke yako huku unayemtetea akimsifu anayemsurubu.
 
Mr P. Kama unakiri kuwa ile mihili mitatu(3) iliyopo ambayo kisheria ni mihili huru lakini haiko huru na kufanya wengi kuwa MAZUZU kama ulivyosema, tatizo hzpo si kuongeza mfumo wa nne japo ni wa muhimu na unaweza kuongezwa. Ieleweke tu kuwa hata ukiongezwa wa nne na wa tano baro inaweza iwe huru kimaandishi na kisheria lakini ikawa sio huru kiutendaji.
Haina maana kupoteza muda mwingi kushughulikia matokeo bila kuamua kutibu chanzo cha tattizo lenyewe. Itakuwa na maana sana kama tutaamua kujua kwanini mihili mitatu iliyopo, ambayo kisheria na kikatiba ni mihimili huru haiko huru kiutendaji na kufanya sasa tuwe unachosema MAZUZU yaani hatuwezi kuhoji Iwe ni mahakamani , bungeni au kupata majibu ya kiserkali kile tunachotakiwa kujua
Jambo lingine ni kujiuliza ni kweli kuwa mihili hii yote mitatu iliyo huru haiko huru Kweli? au iko huru sisi ndio hatuoni? tumeamua kutengeneza taswira zetu wenyewe kwa kuona hakuna uhuru wa hiyo mihili? Tujiulize maswali kuwa ni kweli Bunge haliko huru? kuwa ni kweli Mahakama haiko huru kusimamia sheria na kuzitofasri Tujiulize kuwa ni kweli kuwa serkali haiko huru kusimamia sheria zitekelezwe? Lkini jingine la kujiuliza ni hili Je uko mhimili uliomeza mihimili mingine? kwa maana ya kuwa aidha Bunge, Mahakam au Serkali ummemeza wenzake na unawaamuru wafanye kile unataka? Kama jibu ni Ndio basi hoja si kuanzisha mhimili wa nne , Kama ni Hapana kwanini hakuna uhuru wa hii mihili mitatu iliyopo?
Hapa unaweza ukaona shida kuwa mhimili mmoja umepewa nguvu kubwa za kuimeza mihili mingine Kikatiba na hapa si kosa la yeyote anakuwa kwenye ngazi, tatizo ni KATIBA.
Kama Rais amepewa mamlaka ya kuamua nani awe Jaji Mkuu wa Mahakama , Nani awe nani kwenye vyombo vya kusimamia sheria ngazi ya serkali, basi hata angekuwa nani aliowateua watakuwa watiifu kwa Mteuaji , na ni kweli Rais lazima ateue watu atakaweza kufanya nao kazi ili kufikia azma yalipanga kuiendeleza nchi hili ni HAKIKA huwezi kuteua mtu wa kukangusha.
Katiba ndio ina shida wala si Excutive, wala Bunge au Mhakama, halafu hii katiba haikuweka pia kuwa ziwekwe sheria za kufanya check and balance. Mfano ni nani anawajibisha na nani kwa namna gani?
Mhimili wa nne kama utawekwa na top wake akawa Mteule wa Rais hapo hakuna mhimili huru tena. Kma wakuu wa mihili hii wangekuwa wanatokana na matakwa ya walio wengi i.e watu , tena wanaweza kuwajibishwa kirahisi na kushughulikiwa kwa uwazi hili lingekuwa na ubora lakini nani wa kumuajibisha mteule? sana sana ataenguliwa Uteuzi na atateuliwa mwingie, Mwendelezo wa teua tengua teua tengua sinema haiishi.
Ninaweza kusema Mrais wetu wanajitahidi sana kufanya kazi tukiwa tumewatwisha mzigo mzito halafu tunakaa pembeni kuwalaumu wakati hatuwapa usaidizi, hivyo wanafanya kwa utashi wao na kupambana sana kufanya maendeleo kwenye mfumo uliopa majukumu makubwa bila nyenzo za usaidizi. Hivi Rais atawajua watu tabia zao wote katika Taifa lenye watu takribani mil 60? Tutasema vetting commitee, sawa alkini maamuzi ya mwisho ni yake na anawea kubambikwa akajua tayari kitu kinaharibika.
Ni hayo kwa uchache
Tuwe raia Wema. Tutiane moyo na kusaidiana. Tuwe na Mungu Mioyoni. Yesu Anakuja Upesi
 
Reply hii ni ndefu kidogo Ila ina Uchambuzi wa kina hivyo soma kwa utulivu.

HAPO CHINI NIMEWEKA UCHAMBUZI WA KINA, KISOMI NA KITAALUMA, KWANINI MUHIMILI WA NNE NI MUHIMU na KWANINI HAUPASWI KUWA MIKONONI MWA WAANDISHI WA HABARI.

Pascal Mayalla hoja yako ina nguvu, na tukio hili la Mwanahalisi ni ushahidi wa moja kwa moja wa jambo ninalolisimamia kwa muda mrefu. Naomba nichangie kwa mtazamo tofauti kidogo, siyo wa kupinga msingi wa hoja yako, bali wa kuonesha wapi udhaifu wa kimuundo ulipo.

Umeeleza vizuri dhana ya The Fourth Estate, mhimili usio rasmi wa habari. Lakini hapo hapo umegusa, bila kukusudia, udhaifu wake mkubwa: neno "usio rasmi." Chombo kisicho na hadhi rasmi ya kikatiba hakina ulinzi wa kikatiba, na tumeuona ushahidi wake wiki hii hii. Gazeti pekee lililokuwa na "pua ya habari" kali kuliko vyote, ndilo hasa lililofungiwa, na aliyelifungia ni Idara ya Habari iliyo chini ya Serikali, ambayo ndiyo pia inaweza kuguswa moja kwa moja na habari inayochunguza mambo ya ndani ya chama tawala. Hii siyo bahati mbaya, ni mfumo unaotarajiwa kufanya kazi hivyo: mwenye kudhibiti leseni na mwenye kuguswa na habari ni chombo kimoja.

Mzee pascal Naomba nikupe Taarifa hizi Hili wote pamoja tuone kama Vyombo vya Habari vinafaa kuwa Ndio Muhimili wa Nne wa Taifa.

Kwa mujibu wa taarifa za kimataifa, tarehe 9 Machi 2026 Shirika la Aga Khan la Maendeleo ya Kiuchumi lilikubaliana kuuza hisa zake zote za asilimia 54.08 za Nation Media Group, gazeti kubwa zaidi la Afrika Mashariki, kwa Rostam Aziz, mfanyabiashara wa Kitanzania, kupitia kampuni yake ya Taarifa Ltd, hatua iliyomaliza uhusiano wa miaka 66 wa familia ya Aga Khan na shirika hilo, ambalo kwaasili Ndio Roho ya kihabari ya kenya. Wachambuzi wa habari waliibua wasiwasi mara moja kutokana na uhusiano wake wa kibiashara na viongozi wa kisiasa wa kikanda, wakihoji kama uhuru wa uhariri wa taasisi hiyo utaendelea kulindwa.?
Pia Hata Mhariri Mkuu Mstaafu wa NMG mwenyewe alihoji hadharani kama Rostam Aziz ni mwekezaji mmoja tu kuna wawekezaji wengine walio nyuma yake.?
(Hoja yangu hapa ni kwamba Chombo cha Kitaifa cha Kenya ambacho ni Muhimili wa Nne Hupo reheni kuathilika kutokana na hushilika wa mwekezaji, Nguvu ya Umiliki wa hisa, Maadili ya kihabari na Uzalendo wa dhati Kwa Taifa)

Ndiyo maana nasimamia kwamba badala ya kutegemea vyombo vya habari kama mhimili usio rasmi, tunahitaji kuweka usimamizi wa habari kwenye chombo cha kikatiba chenye ulinzi wa moja kwa moja dhidi ya matumizi mabaya ya mamlaka ya leseni. Pia kuweka Mihimili wa Nne Rasmi kabisa Ambapo kazi yake kubwa ni Kusimamia Misingi ya kitaifa.

Rasimu iliyopo www.katibampya.com inaunda Tume ya Haki Habari, Maadili na Uhusiano kwa Ibara ya 214, na muundo wake unaziba hasa pengo tuliloliona wiki hii.

Kwanza, Ibara ya 214(7) inakataza waziwazi Mkurugenzi wa Tume kutotokana au kunathibitishwa na Jeshi, Polisi, Usalama wa Taifa, au mamlaka yenye maslahi ya kisiasa. Mamlaka ya kudhibiti habari haiwekwi tena mikononi mwa idara ya kiserikali inayoweza kuathiriwa na maslahi ya chama tawala.

Pili, Ibara ya 214(3)(b) inatoa waziwazi haki ya kikatiba kwa vyombo vya habari kuhoji, kuchunguza, na kufanya uchambuzi wa kina juu ya suala lolote linalomhusu raia au taasisi ya umma. Hii si hisani, ni haki iliyowekwa kikatiba.

Tatu, na hili ndilo linalozuia hasa kilichotokea kwa Mwanahalisi, Ibara ya 214(5)(c) inatamka waziwazi: mamlaka ya Tume hii hayataruhusiwa kutumika kuzuia au kukandamiza uhuru wa habari. Zaidi, Ibara ya 214(5)(d) inaweka ngazi za adhabu, kuanzia mazungumzo, hadi marekebisho ya maudhui, hadi hatua za kinidhamu, lakini inasisitiza kwamba Tume "kamwe haitazuia chombo cha habari kufanya kazi zake kwa uhuru bila sababu za msingi." Kufungiwa kabisa kwa miezi sita ni hatua ya mwisho kabisa, siyo ya kwanza, na lazima ithibitike kuwa na sababu za msingi, siyo uamuzi wa haraka wa kiutawala.

Nne, Ibara ya 214(5)(e) inalazimisha maamuzi yote ya Tume kuhusu habari kuwekwa hadharani na kutolewa sababu rasmi, isipokuwa kwa masuala ya usalama wa Taifa. Hii ina maana uamuzi wa kufungia gazeti usingeweza kuachwa bila maelezo ya wazi kwa umma.

Changamoto inayokumba Kenya Kwa sasa ni mambo mawili na ni ukweli kwamba hata hapa kwetu Tusije tukaweka Vyombo vya Habari kama Muhimili wa Nne Bali Tuweke Muhimili wa Nne kama Muhimili wa Usimamizi wa Misingi ya taifa.
1. Muundo wa Vyombo vya Habari kuwa Ndio Muhimili wa Nne unaathiliwa na Mamlaka yake ya Udhibiti Yaani Serikali.

2. Muundo wa Vyombo vya Habari kuwa Ndio Muhimili wa Nne unaathiliwa na Mtu mmoja Mwenye uwezo wa kifedha kuhodhi Muhimili mzima Kwa Mlango wa nyuma.

Kwa hiyo tofauti kati ya mfumo wa sasa na huu ninaoupendekeza si kwamba mmoja unaunga mkono uhuru wa habari na mwingine haungi mkono. Ni kwamba mfumo wa sasa unaweka mamlaka ya adhabu mikononi mwa chombo kile kile kinachoweza kuguswa na habari husika,

Kwakuwa Mimi sio mwanahabari au sipo kwenye Taaluma ya Habari, Naomba Niseme kwamba Sina hukumu kuhusu usahihi wa habari ya Mwanahalisi waliyowai kuitoa. Hoja yangu ni kwamba mfumo unaomruhusu mtu mmoja au idara moja kuamua kufungia sauti pekee ya uchunguzi bila mchakato wa kikatiba ni mfumo dhaifu, bila kujali ni nani yupo madarakani Kwa wakati huo.

Ninakualika, Mzee Pasco, kwa uzoefu wako mkubwa wa uandishi wa habari, kusoma Ibara ya 214 kikamilifu na kuipima kwa jicho la mtaalamu: je muundo huu ungeliweza kuzuia kile kilichotokea kwa Mwanahalisi wiki hii?

PENDEKEZO LANGU LA KUTATUA CHANGAMOTO HII ZOTE NI HILI.
Mwanzo Nilisema kwamba Vyombo vya Habari kuwekwa Ndio Muhimili wa Nne ni Hatari lakini nikasema Muundo Bora ni kuweka Mihimili wa Nne Rasmi wenye Jukumu la Usimamizi wa Misingi yote ya Kitaifa, naomba Niseme Hivi katika Rasimu ya Katiba iliyopo kwenye Tovuti Tajwa imeanzisha Muundo wa Mihimili minne ya Kitaifa, Yaani.
1. Baraza la Usimamizi wa Taifa
2. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
3. Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
4. Mahakama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwenye Muundo Huu limeongezeka Baraza la Usimamizi wa Taifa kama Mamlaka ya Kimuungano Kati ya Tanganyika na Zanzibar, Mamlaka ya Usimamizi wa Misingi ya Kitaifa, Tathimini na Ndio Mlinzi wa ufuasi wa Katiba, Yaani anasimamia Katiba ifuatwe iwe na wafuasi, sio Mtu Mwenye Madaraka kuamua kuifuata Kwa hiyali yake Bali Kwa Lazima kama Katiba itamkavyo. Kwa lugha ya mchezo kwenye Hili ni Sawa na kusema Baraza Ndio refa wa Taifa pale Uhuru wa Habari au Mamlaka nyingine kupita Mipaka yake Basi Baraza linairudiaha Mamlaka hiyo kwenye Mstari Bila kuchukuwa Utendaji wa kla siku wa Mamlaka au Taasisi hiyo.

Kwenye Rasimu hiyo Baraza la Usimamizi wa Taifa limetamkwa katika Ibara ya 98 mbaka 116 niwaomba Kuisoma, kuichambua na kuisambaza Rasimu hiyo kadri iwezekanavyo.

Swali la Kikatiba: ikiwa Mamlaka ya kiserikali au nyingine yoyote imekataa Kwa Makusudi kufuata Katiba, Je kuna Mamlaka ya Kutoa muongozo na kuiladhimisha Mamlaka hiyo kufuata ufuasi wa Katiba...?

Rasimu kamili ipo www.katibampya.com
 
Kila kitu hapo ni siasa tu, ila vyombo vya habari au taasisi za habari (Media Institutions) vyapaswa kuwa ni vyombo huru (Independent Watchdog) ambapo kazi zake kubwa ni kuhabarisha umma, kukosoa utawala na kuchunguza masuala mbalimbali kwa uwazi, bila upendeleo na kwa kufuata misingi ya uandishi wa habari na sheria zilizopo.

Sasa tukienda kwenye uandishi wa habari za kiuchunguzi kwamba una lengo la kutafuta ukweli, kuonyesha kasoro na mapungufu na kuimarisha uwajibikaji chini ya msingi wa kwamba demokrasia ni pamoja na kukubali kuwajibika.

Hivyo tukisema ni "The Fourth State" ni kweli mhimili uso rasmi lakini ni "ESSENTIAL" yaani mhimili wenye umuhimu kwa jamii ambayo siku zote yautegemea mhimili huo "The Fourth State" kuingiliana na mihimili mingine ya uraisi, Bunge na Mahakama kwamba mihimili hiyo mitatu yatambua kuwa upo UMUHIMU wa majukuu ya The Fourth State kutekelezwa.

Majukumu hayo ni pamoja na ile misingi mitatu kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha na sasa hivi kuisogeza jamii karibu zaidi kupata habari hizo.

Pili., kufanya kazi ya kumulika mihimili hiyo mitatu.

Tatu, kutoa habari kwa pande zote yaani kwa umma na pia kwa vyombo vya serikali ikiwemo ile mihimili mitatu.

Hii yamaanisha kwamba vyombo vya habari ni lazima (nasisitiza ni LAZIMA) viwe huru kuuliza, kuchunguza na kukosoa Utawala bila woga.

Kwa mfano pamoja na kwamba Saed Kubenea amefanya uchunguzi wake na kajiridhisha kwamba habari hizo ni za uhakika wa asilimia 100, Mwanahalisi ilipaswa kuitaarifu CCM na serikali (MAELEZO) kwamba wako mbioni kutoa taarifa hiyo ambayo wameipata kwa njia zozote zile kurekodi au makabrasha.

CCM na Serikali wao wapaswa kuthibitisha au kukanusha madai hayo lakini pia kuruhusu habari hiyo itoke na kisha umma ujulishwe.

Hapa twazungumzia uwajibikaji , haki ya kidemokrasia ya kutoa na kupata habari, umuhimu wa "The Fourth State", haki ya IJ kutekeleza majukumu yake na uhuru wa vyombo vya habari kufanya kazi yake bila woga.

Lakini pia IJ nayo ni lazima ionyeshe kuzingatia utaalam na miiko ya uandishi wa habari zake kwa kuutafuta ukweli na kuuthibitisha kabla habari haijatoka, kutumia vyanzo vinoaminika na kuwa na ushahidi na sio uzushi au uvumi.

Pia IJ yapaswa kuzingatia uwiano kati ya maslahi ya umma na usawa vitu ambavyo vitaondoa migogoro na taharuki, kuzngatioa sheria zilizopo, usalama wa taifa na kulinda uhuru wa uhariri kutoka kwa ushawishi wa siasa au biashara.

Kwa mfano jukwaa la wahariri ni kifungo kwa vyombo vya habari kwenye kuwa huru kuhoji au hata kuuliza suali nje ya mada. Chombo chochote cha habari kiwe huru kumsaka mhusika yeyote na kutaka interview ili mradi mwandishi ana credentials zote.

Mwisho, bado vyombo vya habari Tanzania haviko huru na vinapokosa uhuru umma unakuwa wakosa kuhabarishwa au mara nyingi kupewa habari zisizokusudiwa (misinformation) na ndo kuzaa neno Mazuzu, umma unabakia kuwa mazuzu kama asemavyo mkuu Paschal.

Vyombo vya habari kwa sasa vimekuwa na shinikizo la kisiasa lilopelekea vingi kutoa habari kichawa na za upande mmoja na pia vingine kununuliwa kama ulivyosema mkuu hapo juu na hiyo ni corporate capture.

Kwahiyo kama alivyosema mkuu mrxtz2026 hapo juu kwamba rasimu ya jaji Warioba yapendekeza hiyo mihimili minne na vyombo vya habari viingizwe kwenye mhimili wa Baraza la Usimamizi wa Kitaifa ambapo vyombo hivyo vitatekeleza majukumu yake yaani kama aitavyo kaka Sammy Awami , "well- functioning media ecosystem" kwamba vyatekeleza shughuli zake kwa kuzingatia sheria na hapohapo kuvilinda dhidi ya kufungiwa kila mara na kuharibu uwezo wake wa kujiendesha.

Mhimili huu utaondoa baadhi ya kamba zilizopo za kutoka jukwaa la wahariri, MAELEZO na Ithibati ambazo zin alengo la KUDHIBITI uandishi unozingatia taaluma. Mhimili huo utawezesha umma kutambua umuhimu wa IJ na mwisho (hili ni muhimu) kudhibiti umiliki unohodhi vyombo vingi vya habari au kwa neno la monopolies.
 
Kwanza kabisa Naunga mkono hoja
"well- functioning media ecosystem",
Pili naomba nikuweke sawa kidogo kama si kukosoa. Pale uliposema
Kwahiyo kama alivyosema mkuu mrxtz2026 hapo juu kwamba rasimu ya jaji Warioba yapendekeza hiyo mihimili minne na vyombo vya habari viingizwe kwenye mhimili wa Baraza la Usimamizi wa Kitaifa
Nadhani ulikuwa unafikilia rasimu ya katiba iliyo kwenye tovuti ya www.katibampya.com ni rasimu ya jaji Joseph sinde warioba. Jibu ni Hapana..

Rasimu hiyo
ya ni Maoni pendekezi ya mrxtz2026 kwenda kwa umma, mamlaka za nchi, taasisi mbali mbali za kisheria na taifa kwa ujumla kama mchango wake wa kisomi, kitaaluma na kijamii kama mtanzania.

Hivyo kutokana na Elimu ya sheria za kikatiba za kimataifa alizozipata duniani na katika vyuo vikuu mbali mbali africa kama Mkufunzi na SJD ya sheria ametoa maoni ya katiba yenye muundo wa dola lenye mihimili minne ikiwa ni rasimu kamili ya katiba yenye sura 14 na ibara 321.

Nikuombe kama utapendezwa kuujua kiundani muundo huo hasa baraza la usimamizi wa taifa basi limetajwa katika ibara ya 98 mbaka ibara ya 116 ya rasimu hiyo ya katiba.

Asante na naunga mkono hoja zako zote na kukupongeza kwa uchambuzi wako wa kina.
 
Wanabodi,
Hii ni makala yangu kwenye gazeti la Mwananchi la leo, ambapo nimeibua hoja 4 nikiuliza kama wajua kuwa Taifa lisilo la mhimili wa Nne ulio huru na imara ni kama taifa mfu kwasababu ile mihimili mitatu ya Serikali, Bunge na Mahakama, itakuwa huru kujivinjari na madudu ya kila aina, huku hakuna yeyote anayeyaibua madudu hayo. Na kitendo cha Watanzania kufanyiwa madudu ya ajabu, huku wamenyamaza kimya na kutulia tuu bila kuuliza lolote, ni kuwa ni tumekuwa kama mazuzu!. Mazuzu ni majitu ambayo unaweza kuyafanyia kitu chochote cha ajabu ajabu, na yenyewe yanakuwa yametulia tuu, as if nothing happened!. Kilichomtokea makamu wao wa rais waliyemchagua, kujiuzulu ghafla, bila kutoa sababu, kisha kufutwa uanachama wake wa chama chake kinyume cha katiba ya JMT, bila kuelezwa sababu au bila wao kuambiwa makosa yake, huku wametulia tuu, hakuna yeyote anayeuliza chochote, wala kujua mahali mtu huyo alipo, yuko na hali gani, ni maisha tuu yanaendelea as if nothing happened, huu ni uzuzu!. Uzuzu huu, unasababishwa na kutokuwepo mhimili wa 4 huru na imara. Tungekuwa na mhimili wa 4 huru na imara, saa hizi ungekuwa umeishafanya IJ ya kujua VP alifanya makosa gani, Watanzania by now wangekuwa wanajua what really happened, wangekuwa wanajua saa hizi yuko wapi na ana hali gani!. Mwisho nimetoa wito kuwa japo gazeti la Mwanahalisi limefungiwa kwa kuandika habari bila mizania, nimeshauri gazeti hilo lisamehewe kwasababu kitu ilichokiandika ni kitu cha ukweli, kosa la ukosefu wa mizania ni kosa dogo ukilinganisha na ukweli ulioibuliwa na Mwanahalisi, au kwa vile sisi ni mazuzu, hivyo hili gazeti liendelee tuu kufungiwa kwa kufanya makosa ya kizuzu, ili liwe fundisho kwa vyombo vingine vyote vya habari visifanye makosa ya kizuzu!, ni bora Taifa la Tanzania kuwa taifa la mazuzu waliotulia, kuliko kuwa taifa la watu informed wanao uliza uliza na hoji hoji mamlaka vitu ambavyo hawapendi vijulikane!.
View attachment 3666303
Nchi nyingi duniani, huendeshwa kwa mihimili mitatu rasmi, Serikali, Bunge na Mahakama, lakini pia kuna mhimili wanne, ambao ni Mhimili usio rasmi, huu ni mhimili wa Habari, The Media, ambao kwa nchi za wenzetu unaitwa “The Fourth Protocol, au The Fourth Estate”

Jukumu kuu la msingi la uandishi wa habari ni upashanaji wa habari, kwa nia ya kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha, ila jukumu la media kama mhimili ni kuwa mlinzi wa jamii husika “watchdog of the society” kwa kutoa habari kutoka ile mihimili mitatu rasmi na kuwafikishia wananchi na jamii, na wakati huo huo kutoa habari za kinachotokea kwenye jamii na kuwafikishia mamlaka, kiingereza wanaita a two way traffic.

Ili mhimili huu wa media au fani hii ya uandishi wa habari, iweze kutekeleza majukumu yake ya uhimili kikamilifu, inahitaji watu sio tuu wenye ewezo wa kusomea fani ya uandishi wa habari ili kupata sifa za kuwa mwandishi wa habari, fani hii inamuhitaji mwandishi wa habari kuwa na kipaji cha kuwa na pua yenye uwezo wa kunusa habari , inaitwa “nose for news”

Hii “nose for news” ni uwezo wa kuinusa habari fulani na kuiandika kabla haijatokea. Waandishi wenye pua kali, yenye uwezo huo, ndio wale wenye uwezo wa kuandika habari za uchunguzi, “investigative journalism, IJ”, yaani kuibua habari, ambapo kwa vyombo vya habari vya Tanzania ya sasa, hili halifanyiki sana, kwasababu, nyingi ya habari za uchunguzi, mwisho wake huwa zinaibua madudu ya mamlaka hivyo ama chombo cha habari kinashukiwa, ama mwandishi wa habari za uchunguzi anashukiwa, ama wote wawili mwandishi na chombo chake wanashukiwa, wanasulubiwa!.

Kashfa nyingi zimeibuliwa na waandishi wa habari za uchunguzi, zikiwemo kashfa maarufu ya Loliondo iliyoibuliwa na mwandishi wa habari Stan Katabalo wa gazeti la Mfanyakazi, kashfa ya IPTL, kashfa ya Escrow, kashfa ya Richmond iliyomng'oa Waziri Mkuu , Edward Lowassa madarakani, na kashfa nyingine mbalimbali.

Ni mwandishi Saed Kubenea na gazeti lake la Mwanahalisi, kupitia Toleo No. 571 la Agosti 6 hadi 12, 2026, lenye kichwa cha habari "Nchimbi agoma kujiuzulu"ndie aliyeibua hii kashfa ya sasa ya kuondolewa kwa Makamu wa Rais Balozi Dr. Emmanuel Nchimbi madarakani kwa kutumia chanzo fiche ndani ya kikao cha NEC.

Idara ya Huduma za Habari (MAELEZO) ikasitisha leseni ya gazeti la MwanaHALISI kwa miezi sita (6) kuanzia tarehe 19 Agosti, 2026 kutokana na kukiuka sharti la 3 katika Leseni ya machapisho linalovitaka vyombo vya habari kuzingatia Sheria ya Huduma za Habari (Sura 229) na Kanuni zake (2017)

Taarifa ya Maelezo ilisema Taaluma ya uandishi wa habari ni taaluma adhimu na inayohitaji kutumiwa kwa umakini na uangalifu wa hali ya juu ili kuepusha upotoshaji na kuhakikisha jamii inapata habari sahihi, za ukweli na ambazo kutafutwa, kuchakatwa na kuchapishwa kwake kumezingatia Sheria, Ka-nuni, weledi na misingi ya taaluma ya uandishi wa habari inayotumika kote duniani.

Kosa la Mwanahalisi ni kutokuweka uthibitisho mahali popote alipochukua jitihada za ku-wahoji hata mmoja wa viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) au watu waliokuwa wajumbe wa kikao hicho, mathalani, Katibu Mkuu, Katibu Mwenezi au Afisa Habari wa Chama cha Mapinduzi (ccm), ili kuthibitisha hayo yanayodaiwa kuwa yalijadiliwa katika kikao hicho, baada ya kuwa ameambiwa na vyanzo fiche.

Sifa kuu ya chombo cha habari makini ni kutafuta ukweli, kusema ukweli, kuandika ukweli na kutangaza ukweli, seek the truth and the truth will set you free, kanuni kuu ya uandishi wa habari, cardinal rule ni "tell nothing but the truth".

Sasa kwa vile yote gazeti la Mwanahalisi waliyo yaandika, kuhusu Nchimbi kugoma kujiuzulu, hatimaye yamekuja kutokea kweli, Makamu Rais kujiuzulu, na kitendo cha kufutwa uanachama wa CCM, ni uthibitisho kuwa mwanzo aligoma kujiuzulu, hivyo hata baada ya kujiuzulu, kitendo cha CCM kumfutia uanachama wake, ni uthibitisho tosha ameadhibiwa kwa kufutwa uanachama wake wa CCM, japo CCM haikutoa sababu, Gazeti la Mwanahalisi lilisha andika sababu.

Gazeti la Mwanahalisi, ndilo gazeti pekee linaloandika habari za uchunguzi, kitendo cha kuendelea kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi, kumewakosesha Watanzania hata kujua tuu kosa la aliyefutiwa uanachama!, gazeti hilo lingekuwepo, saa hizi taifa lingeishahabarishwa makamu rais mstaafu saa hizi yuko wapi, hivyo kupunguza taharuki ya nini kimempatsa. Kulifungia gazeti pekee la IJ, ni kaburi la habari za kiuchunguzi Tanzania.

Hivyo, natoa wito kwa Idara yetu ya Habari Maelezo, japo ni kweli gazeti la Mwanahalisi limefanya makosa ya kuchapisha habari isiyokuwa na mizania, lakini kwa vile kilichoandikwa, kimekuja kutokea kweli, gazeti lisamehewe huku tukiendelea kupigania kuundwa kwa Baraza Huru la Habari.

Mungu Ibariki Tanzania.

Mzee Pasco.
Kumbuka huo mhimili kamwe auwezi kua na nguvu kuliko hiyo mitatu maana huo mhimili sio rasmi na autende kuringana na makubaliano ..mwisho huo mhimili una marengo tofauti kuringana na dhima na hitaji lake.
 
Kumbuka huo mhimili kamwe auwezi kua na nguvu kuliko hiyo mitatu
Sijasema popote muhimili huo wa nne uwe na nguvu kuliko ile mihimili mitatu, kinachotakiwa ni mhimili huo wa nne uwe imara kutimiza majukumu yake kikamilifu, wakuu wa ile mihimili mitatu wakifanya madudu, mhimili wa nne unawakomalia na kuwafurusha!.

Mfano Tanzania tungekuwa na mhimili wa 4 imara, kwa lile tukio la October 29, kuna mtu angefurushwa ofisini!.
P
 
Okay,kwani tukio la 29 Oktoba huyo mhimili wa nne si ndiyo kwa kiasi kikubwa ulichochea vurugu,fujo,hasara,wizi na risasi. Mhimili wa nne kwanza huko kwenu mnautumia vibaya asa kwa maslahi yenu nyie wamiliki wa huo mhimili.
 
Wanabodi,
Hii ni makala yangu kwenye gazeti la Mwananchi la leo, ambapo nimeibua hoja 4 nikiuliza kama wajua kuwa Taifa lisilo la mhimili wa Nne ulio huru na imara ni kama taifa mfu kwasababu ile mihimili mitatu ya Serikali, Bunge na Mahakama, itakuwa huru kujivinjari na madudu ya kila aina, huku hakuna yeyote anayeyaibua madudu hayo. Na kitendo cha Watanzania kufanyiwa madudu ya ajabu, huku wamenyamaza kimya na kutulia tuu bila kuuliza lolote, ni kuwa ni tumekuwa kama mazuzu!. Mazuzu ni majitu ambayo unaweza kuyafanyia kitu chochote cha ajabu ajabu, na yenyewe yanakuwa yametulia tuu, as if nothing happened!. Kilichomtokea makamu wao wa rais waliyemchagua, kujiuzulu ghafla, bila kutoa sababu, kisha kufutwa uanachama wake wa chama chake kinyume cha katiba ya JMT, bila kuelezwa sababu au bila wao kuambiwa makosa yake, huku wametulia tuu, hakuna yeyote anayeuliza chochote, wala kujua mahali mtu huyo alipo, yuko na hali gani, ni maisha tuu yanaendelea as if nothing happened, huu ni uzuzu!. Uzuzu huu, unasababishwa na kutokuwepo mhimili wa 4 huru na imara. Tungekuwa na mhimili wa 4 huru na imara, saa hizi ungekuwa umeishafanya IJ ya kujua VP alifanya makosa gani, Watanzania by now wangekuwa wanajua what really happened, wangekuwa wanajua saa hizi yuko wapi na ana hali gani!. Mwisho nimetoa wito kuwa japo gazeti la Mwanahalisi limefungiwa kwa kuandika habari bila mizania, nimeshauri gazeti hilo lisamehewe kwasababu kitu ilichokiandika ni kitu cha ukweli, kosa la ukosefu wa mizania ni kosa dogo ukilinganisha na ukweli ulioibuliwa na Mwanahalisi, au kwa vile sisi ni mazuzu, hivyo hili gazeti liendelee tuu kufungiwa kwa kufanya makosa ya kizuzu, ili liwe fundisho kwa vyombo vingine vyote vya habari visifanye makosa ya kizuzu!, ni bora Taifa la Tanzania kuwa taifa la mazuzu waliotulia, kuliko kuwa taifa la watu informed wanao uliza uliza na hoji hoji mamlaka vitu ambavyo hawapendi vijulikane!.
View attachment 3666303
Nchi nyingi duniani, huendeshwa kwa mihimili mitatu rasmi, Serikali, Bunge na Mahakama, lakini pia kuna mhimili wanne, ambao ni Mhimili usio rasmi, huu ni mhimili wa Habari, The Media, ambao kwa nchi za wenzetu unaitwa “The Fourth Protocol, au The Fourth Estate”

Jukumu kuu la msingi la uandishi wa habari ni upashanaji wa habari, kwa nia ya kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha, ila jukumu la media kama mhimili ni kuwa mlinzi wa jamii husika “watchdog of the society” kwa kutoa habari kutoka ile mihimili mitatu rasmi na kuwafikishia wananchi na jamii, na wakati huo huo kutoa habari za kinachotokea kwenye jamii na kuwafikishia mamlaka, kiingereza wanaita a two way traffic.

Ili mhimili huu wa media au fani hii ya uandishi wa habari, iweze kutekeleza majukumu yake ya uhimili kikamilifu, inahitaji watu sio tuu wenye ewezo wa kusomea fani ya uandishi wa habari ili kupata sifa za kuwa mwandishi wa habari, fani hii inamuhitaji mwandishi wa habari kuwa na kipaji cha kuwa na pua yenye uwezo wa kunusa habari , inaitwa “nose for news”

Hii “nose for news” ni uwezo wa kuinusa habari fulani na kuiandika kabla haijatokea. Waandishi wenye pua kali, yenye uwezo huo, ndio wale wenye uwezo wa kuandika habari za uchunguzi, “investigative journalism, IJ”, yaani kuibua habari, ambapo kwa vyombo vya habari vya Tanzania ya sasa, hili halifanyiki sana, kwasababu, nyingi ya habari za uchunguzi, mwisho wake huwa zinaibua madudu ya mamlaka hivyo ama chombo cha habari kinashukiwa, ama mwandishi wa habari za uchunguzi anashukiwa, ama wote wawili mwandishi na chombo chake wanashukiwa, wanasulubiwa!.

Kashfa nyingi zimeibuliwa na waandishi wa habari za uchunguzi, zikiwemo kashfa maarufu ya Loliondo iliyoibuliwa na mwandishi wa habari Stan Katabalo wa gazeti la Mfanyakazi, kashfa ya IPTL, kashfa ya Escrow, kashfa ya Richmond iliyomng'oa Waziri Mkuu , Edward Lowassa madarakani, na kashfa nyingine mbalimbali.

Ni mwandishi Saed Kubenea na gazeti lake la Mwanahalisi, kupitia Toleo No. 571 la Agosti 6 hadi 12, 2026, lenye kichwa cha habari "Nchimbi agoma kujiuzulu"ndie aliyeibua hii kashfa ya sasa ya kuondolewa kwa Makamu wa Rais Balozi Dr. Emmanuel Nchimbi madarakani kwa kutumia chanzo fiche ndani ya kikao cha NEC.

Idara ya Huduma za Habari (MAELEZO) ikasitisha leseni ya gazeti la MwanaHALISI kwa miezi sita (6) kuanzia tarehe 19 Agosti, 2026 kutokana na kukiuka sharti la 3 katika Leseni ya machapisho linalovitaka vyombo vya habari kuzingatia Sheria ya Huduma za Habari (Sura 229) na Kanuni zake (2017)

Taarifa ya Maelezo ilisema Taaluma ya uandishi wa habari ni taaluma adhimu na inayohitaji kutumiwa kwa umakini na uangalifu wa hali ya juu ili kuepusha upotoshaji na kuhakikisha jamii inapata habari sahihi, za ukweli na ambazo kutafutwa, kuchakatwa na kuchapishwa kwake kumezingatia Sheria, Ka-nuni, weledi na misingi ya taaluma ya uandishi wa habari inayotumika kote duniani.

Kosa la Mwanahalisi ni kutokuweka uthibitisho mahali popote alipochukua jitihada za ku-wahoji hata mmoja wa viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) au watu waliokuwa wajumbe wa kikao hicho, mathalani, Katibu Mkuu, Katibu Mwenezi au Afisa Habari wa Chama cha Mapinduzi (ccm), ili kuthibitisha hayo yanayodaiwa kuwa yalijadiliwa katika kikao hicho, baada ya kuwa ameambiwa na vyanzo fiche.

Sifa kuu ya chombo cha habari makini ni kutafuta ukweli, kusema ukweli, kuandika ukweli na kutangaza ukweli, seek the truth and the truth will set you free, kanuni kuu ya uandishi wa habari, cardinal rule ni "tell nothing but the truth".

Sasa kwa vile yote gazeti la Mwanahalisi waliyo yaandika, kuhusu Nchimbi kugoma kujiuzulu, hatimaye yamekuja kutokea kweli, Makamu Rais kujiuzulu, na kitendo cha kufutwa uanachama wa CCM, ni uthibitisho kuwa mwanzo aligoma kujiuzulu, hivyo hata baada ya kujiuzulu, kitendo cha CCM kumfutia uanachama wake, ni uthibitisho tosha ameadhibiwa kwa kufutwa uanachama wake wa CCM, japo CCM haikutoa sababu, Gazeti la Mwanahalisi lilisha andika sababu.

Gazeti la Mwanahalisi, ndilo gazeti pekee linaloandika habari za uchunguzi, kitendo cha kuendelea kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi, kumewakosesha Watanzania hata kujua tuu kosa la aliyefutiwa uanachama!, gazeti hilo lingekuwepo, saa hizi taifa lingeishahabarishwa makamu rais mstaafu saa hizi yuko wapi, hivyo kupunguza taharuki ya nini kimempatsa. Kulifungia gazeti pekee la IJ, ni kaburi la habari za kiuchunguzi Tanzania.

Hivyo, natoa wito kwa Idara yetu ya Habari Maelezo, japo ni kweli gazeti la Mwanahalisi limefanya makosa ya kuchapisha habari isiyokuwa na mizania, lakini kwa vile kilichoandikwa, kimekuja kutokea kweli, gazeti lisamehewe huku tukiendelea kupigania kuundwa kwa Baraza Huru la Habari.

Mungu Ibariki Tanzania.

Mzee Pasco.
Mzee P,abgaalia asitymwe Mwaipopo kufuata press card yako Tu😌🤔
 
Waandishi wenzangu wa habari na vyombo vyetu vya habari, kuna wito wetu hapa, https://www.jamiiforums.com/threads...wa-habari-nawaita-hapa.2474333/#post-56896006
Tasnia ya habari Tanzania ni mfu.
Imejaa watu waoga, wajinga, wapumbavu, machawa, waganga njaa, na walamba makalio.
Japo haya ni maneno makali na machungu, huu ndio ndio ukweli kuhusu media yetu , lazima tukubali kuumeza,
Sasa nyie wenzetu wa hapa Tanzania mna kubwa sana la kujifunza toka kwa wenzenu wa Marekani.
Asante kwa taarifa hii, media ya Tanzania, tutajifunza kwa media wenzetu wa Marekani kwasababu waandishi wote wa habari wanafanana na nchi zote duniani zinafanana, Tanzania tuko sawa na Marekani, tutajifunza kwa wenzetu.

Hili la Tanzania kujifunza vitu kutoka kwa Wamarekani, pia nimewahi kushauri
Hivyo kuna vitu vizuri vya kujifunza kutoka kwa wenzetu, tujifunze.

Mzee Pasco
 
Selikali ya Huyu mama ni Selikali ya Kishenzi sana.

Pumbavu zake.
 
Back
Top Bottom