Taifa la Israel halina uhalali wa kumiliki Gaza

Taifa la Israel halina uhalali wa kumiliki Gaza

Kwa asili tangu mwanzo hii nchi ni mali ya waisrael, wapalestina walikuwa wapita njia wakiwa wafanya biashara ndio wakaweka makazi yao humo! Maandiko yanasema kuwa hii ni nchi waliopewa wana wa Israel na Mwenyezi Mungu mwenyewe.

Maandiko gani hayo ? na kaandika nani ??
 
Ngoja nikuambie.. Ibrahim mwenyewe alitokea Ur..kusini mwa Iraq akaenda mpaka hapo Caanan ( Philistine), na aliishi na wacaanan vizuri tu (maana yake alikuta tayari watu wapo na wanaishi hapo karne na karne. Na hata alipotaka kumuoza mtoto wake Isaka mke, alimuagiza mtumishi wake aende kwenye chimbuko lake huko Ur ndo amtafutie mke, na hakutaka aoe wacaanan..Sasa sijui unataka kusema nini, kwamba mwanzilishi wa taifa la Israel (Ibrahim) alikuta nchi hiyo ni tupu, hivyo waisrael ni nchi yao?
Mh kaka mbona umechanganya habari?????
Sijakuelewa untaka sempre Israel ndio palestine????
 
Mh kaka mbona umechanganya habari?????
Sijakuelewa untaka sempre Israel ndio palestine????
Kwani taifa la Israel lilianzishwa mwaka gani? Na kabla halijaanzishwa, hiyo nchi ilikuwa inaitwa jina gani wakati ikitawaliwa na waingereza?
 
Ukisema Israel ni Taifa Haram ( Batili / Lisilotakiwa ) unaweza ukawa unatudhihirishia ni jinsi gani labda unaugua Uwendawazimu ila hujajigundua tu kwani hata katika Kitabu Kitakatifu cha Wakristo tumejifunza kuwa hilo ndilo Taifa la Mungu sasa ukisema ni Haram ina maana hata mwenye Taifa lake hilo Mwenyezi Mungu nae ni Haram pia au?
 
biblia haijaacha kitu imeeleza wazi kabisa kati ya yakobo na esau kuwa wataunda mataifa mawili ambayo hayatakuja kuelewana hadi kiama na mdogo atakuwa na nguvu kuliko mkubwa,vita hii ilianza toka wakiwa tumboni mwa mama yao wallllikuwa wakipigana mpaka mama akajuta kwanini alibeba hiyo mimba

Nani aliandika hiyo biblia ?? tena unaongelea biblia ipi ?? Gay bible, Satanic bible, NIV , RSV, Douay au maelfu ya biblia tofauti ?+
 
Ndivyo unavyofikiri, Biblia ni kitabu cha ahadi na unabii pamoja na mambo mengine. Mungu wa Biblia Yahweh aliwaahidi mababa wa Israeli kwamba amewapa eneo hilo kwa ahadi ya milele. Wakimkosea atawahamisha na kuwaondoa hapo ila ni kwa muda tu, baadaye atawarudisha. Kumkosea walimkosea, wakaabudu miungu na misanamu, kuwaondoa aliwaondoa. Lakini wengi wao aliwarudisha miaka takriban 450 kabla ya Kristo. Wakajenga hekalu upya lakini walikuwa chini ya Waajemi, baadaye Wayunani na mwisho Warumi (wakiwa na utawala wa ndani wakati wa Herode). Baadaye wakamkosea Mungu tena wakamuua Masihi. Mwaka 70 AD Warumi wakaja tena wakawahamisha na eneo lao lijabadilishwa jina na Warumi kutoka Yudea kuwa Philistine Asia. Jina Palestine lilianzia hapo, walibaki wahayudi wachache pamoja na Wagiriki wachache. Baada ya mwaka 600AD Waarabu walianza kutanua mipaka yao na baadaye wakaeneza dini ya Kiislamu. Kwa hiyo Wapalestina wa leo ni hao Waarabu wachache walioishi eneo hilo wakichangamana na Wakristo na Wayahudi. Huu mgogoro wa sasa ni tunda la dunia kukataa na kujaribu kubadili hiyo ahadi ya milele kwa Wayahudi kwenye eneo hilo.
Nilisemahapo mwanzo kwamba Mungu wa Biblia ni Mungu wa unabii: nabii zote zinazohusu siku za mwisho duniani hapa zinawaona wayahudi wakiwa na taifa lao na Yerusalem mji wao mkuu.
Sasa tunapata shida sana kwa kujaribu kwa nguvu zote kubatilisha ahadi ya Mungu kwa mababa wa Israel (Abraham, Isaka na Yakobo ndio Israel). Hakuna nguvu, hata dunia yote ikiungana hatuwezi kuwatoa hao jamaa Yersalem. Sio kwa sababu ni wakali wa vita ila tutakuwa tunapingana na ahadi ya Mungu pamoja na neno la unabii. Ninafahamu wapo ambao haya niliyoandika hawayaamini - na ndio chanzo cha shida zote hizo zinazotokea Palestine leo. Ningetamani Dunia yote ingekubali kwamba Mungu ndio mtawala ana haki kumpa mtu yoyote eneo atakalo yeye Mungu. Sisi tukipinga tutakuwa tunapiga mateke mchongoma. Wenye masikio ya kusikia na wenye hekima wanaojitakia amani wao na watoto wao huiombea Israel amani na ustawi. Kwa sababu huwezi kumlanii mtu ambaye Mungu amembariki na tena "hakuna uchawi juu ya Yakobo".
Umeenena kweli kabisa.
 
Kwa Gaza sawa! Lakini siyo Yerusalemu na West bank.Hayo ni maeneo ya Israel kwa mjibu wa Kitabu Kitakatifu cha Biblia.
1Samweli sura ya 5 na 6: Hii ndiyo miji ya Wapalestina (Wafilist)-Gaza,Ashidodi,Gathi,Ekron na Ashikeloni.
 
Now you are talking; hapa tuko pamoja kabisa; nilicho pinga ni huyo mdau kusema eti Israel ilianza mwaka 1948.
Nazungumzia taifa la Israel sio wana waisrael
Kwani taifa la Israel lilianzishwa mwaka gani? Na kabla halijaanzishwa, hiyo nchi ilikuwa inaitwa jina gani wakati ikitawaliwa na waingereza?
Ilikua ikijulikana Palestine na kabla ya muingereza kutawala ilikua chin ya himaya ottoman baaada ya himaya ya Ottoman kuvunjwa ndio muingereza akaitawala
 
Ngoja nikuambie.. Ibrahim mwenyewe alitokea Ur..kusini mwa Iraq akaenda mpaka hapo Caanan ( Philistine), na aliishi na wacaanan vizuri tu (maana yake alikuta tayari watu wapo na wanaishi hapo karne na karne) Na hata alipotaka kumuoza mtoto wake Isaka mke, alimuagiza mtumishi wake aende kwenye chimbuko lake huko Ur ndo amtafutie mke, na hakutaka aoe wacaanan..Sasa sijui unataka kusema nini, kwamba mwanzilishi wa taifa la Israel (Ibrahim) alikuta nchi hiyo ni tupu, hivyo waisrael ni nchi yao?
Unachanganya habar Ibrahim ni mwarabu sio muisraeli.Na Ibrahim katokea Iraq.
Yeye sio muisrael
 
Nazungumzia taifa la Israel sio wana waisrael

Ilikua ikijulikana Palestine na kabla ya muingereza kutawala ilikua chin ya himaya ottoman baaada ya himaya ya Ottoman kuvunjwa ndio muingereza akaitawala
Siku zote ni Palestine.. zamani ilikuwa inaitwa Caanan nchi waliyokuwa wanakaa wafilisti ( Philistines)
 
Nazungumzia taifa la Israel sio wana waisrael

Ilikua ikijulikana Palestine na kabla ya muingereza kutawala ilikua chin ya himaya ottoman baaada ya himaya ya Ottoman kuvunjwa ndio muingereza akaitawala
Niambie, wafalme hawa walikua wanaongoza Israel ipi? Musa, Yoshua, Samson, Samuel, Saul, Daudi (king David, nadhani huyu ndio nembo halisi ya Israel, hadi meza ya kuhutubia ya waziri mkuu wa sasa hivi imeandikwa jina hilo), Suleiman/Seleman nk. Remember hawa wote walikua wafalme/viongozi miaka ya nyuma sana kabla hata ya huyo unaemwita sijui Ottoman, hao walikuwepo enzi hizo, miaka zaidi ya 700 BC.
 
Unachanganya habar Ibrahim ni mwarabu sio muisraeli.Na Ibrahim katokea Iraq.
Yeye sio muisrael
Mkuu, sio kila aliyepo mashariki ya kati n mwarabu, historia ya waarabu wote inaanzia kwa Ibrahim, waarabu ni matokeo ya mtoto wa Ibrahim aliyezaa na house girl wake, nabii Ibrahimu alipiga copy na house girl then hao watoto wa house girl ndio wakafanya mataifa ya kiarabu, by history, Iran na Iraq sio waarabu, kasome tu historia ya kawaida kabisa sio ya kidini; hao Iraq na Iran of course hata Samaria (sasa Syria ) na Misry kihistoria sio waarabu, Uislamu ndio ulikuja kuwafanya kama kitu kimoja. Historia ya kawaida tu, sio ya kidini mkuu.
 
Mh mkuu umeenda viral sana.
Kwahiyo Iraq ni wayahudi???
Km umesema waarabu wametokan na Ibrahim kuzaa na house girl wake je house girl wake ametokea ktk chimbuko gani km siyo la uarabu????
Mkuu embu fanya reasoning vzuri.
 
Niambie, wafalme hawa walikua wanaongoza Israel ipi? Musa, Yoshua, Samson, Samuel, Saul, Daudi (king David, nadhani huyu ndio nembo halisi ya Israel, hadi meza ya kuhutubia ya waziri mkuu wa sasa hivi imeandikwa jina hilo), Suleiman/Seleman nk. Remember hawa wote walikua wafalme/viongozi miaka ya nyuma sana kabla hata ya huyo unaemwita sijui Ottoman, hao walikuwepo enzi hizo, miaka zaidi ya 700 BC.
Unaongea kwa minajili ya kibiblia kaka.
 
Back
Top Bottom