Taifa letu lilianza kwa kukusanya laana badala ya baraka

Taifa letu lilianza kwa kukusanya laana badala ya baraka

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2016
Posts
14,311
Reaction score
36,056
Wasalaam wana JF

Katika tafakari zangu nimekua nijiuliza mambo mengi yanayohusu mustakabali wa taifa letu. Maranyingi ustawi wa taifa letu una kwenda mbele na kurudi nyuma kila baada ya awamu moja kwenda nyingine. Atakuja kiongozi mzuri atajenga uchumi anayefuata anabomoa.

Hali kadhalika, taifa halina consistency kwenye ajenda za kiuchumi kutoka awamu moja kwenda nyingine . Tuko kama tumechanganyikiwa vile. Taifa linaongoza kwa matamko na slogan za kisiasa na za kiuchumi zisizotekelezeka.

Mfano: Siasa ni kilimo, kilimo ni uti wa mgongo, kilimo kwanza, hari mpya kasi mpya, hapa kazi tu, na kazi iendelee. Tangu tupate uhuru matamko yamekua mengi sana, yanachosha na kuchefua.

Kwanini tunapiga hatua mbili mbele na kurudi tano nyuma? Jibu ni kwamba tulidhulumu. Tulianzisha mfumo wa ujamaa na kujitegemea, tukatoa azimio la Arusha, ambalo lilifanikisha dhuluma na unyang'anyi. Watu waliofanya kazi kwa bidii na kupata mali kihalali walinyang'anywa na kuitwa wahujumu uchumi.

Taasisi za dini ziliporwa hospitali na shule na wageni waliporwa mali na biashara zao. Kwa upofu wa fikra tulitaka kuleta usawa baina ya wavivu na wawajibikaji, wabunifu na wababaishaji, waliobarkiwa na waliochanganyikiwa. Kwa upofu huo, taifa likawa jambazi, likapora mali za watu.

Baadhi ya watu walipoteza maisha na wako mbele ya kiti cha enzi wakimlalamikia Mungu kuhusu taifa hili nyang'anyi. Watu hao wameacha wajane/wagane na yatima ambao wameishi maisha ya dhiki na manung'uniko.

Katika kusoma kwangu maandiko nimeona sehemu nyingi ambapo Mungu ametoa adhabu na laana kwa watu wanaodhulumu, laana inayopitiliza maisha ya mlaaniwa na kwenda mpaka kwa vizazi vyake. Maneno ya Mungu yanaishi na yanatolewa ushuhuda huu. Kama taifa, inatupasa tujitafakari na kuchukua hatua stahiki ili tuweze kusonga mbele.

Nawasilisha.
 
Mfumo wa kibepari ni wa kishetani ampapo wachache wanamiliki mali na wengi wanakuwa watumwa wa kutumikia wenye mali
Issue siyo mifumo,ni utekelezaji wa hiyo mifumo, sisi tulidhulumu
 
mbona haikuwa kazi ngumu, ulikuwa unaulizwa tu hii mali umeipata wapi? usipotolea majibu inakula kwako ndio maana kuna wafanyabiashara toka zama hizo mpaka leo bado ni matajiri sababu walipata utajiri wao kihalali

The same applies kwenye awamu iliopita, unaulizwa tu kwenye akaunti yako kuna m500, mshahara wako ni 1.5m umeipata wapi na huna biashara wala hisa, halafu hujibu we unategemea nini??

tukija kwenye kodi, unakuta mfanyabiashara ana turnover ya Mil.200 kwa mwaka ila unadanganya ni Mil.50 kwa miaka kama 7 hivi, nimekushtukia leo nakukokotolea kodi ya miaka yote uliyofanya udanganyifu halafu unalialia serikali imeua biashara, sasa si udanganyifu ulifanya mwenyewe?? kama tawala zilizopita zilichukua rushwa na kukuacha upete huo ni ujinga wako
 
Yaani mnavyoponda ujamaa, utafikiri huko kwenye nchi za kibepari kila mtu ana Maisha mazuri.
Wanajali utu wa mtu, watu hawabomolewi nyumba bila kufahamu watakwenda wapi. Hata kama walijenga kwa makosa wanajengewa nyumba hata kama ni chumba na sebule.
 
mbona haikuwa kazi ngumu, ulikuwa unaulizwa tu hii mali umeipata wapi? usipotolea majibu inakula kwako ndio maana kuna wafanyabiashara toka zama hizo mpaka leo bado ni matajiri sababu walipata utajiri wao kihalali

The same applies kwenye awamu iliopita, unaulizwa tu kwenye akaunti yako kuna m500, mshahara wako ni 1.5m umeipata wapi na huna biashara wala hisa, halafu hujibu we unategemea nini??

tukija kwenye kodi, unakuta mfanyabiashara ana turnover ya Mil.200 kwa mwaka ila unadanganya ni Mil.50 kwa miaka kama 7 hivi, nimekushtukia leo nakukokotolea kodi ya miaka yote uliyofanya udanganyifu halafu unalialia serikali imeua biashara, sasa si udanganyifu ulifanya mwenyewe?? kama tawala zilizopita zilichukua rushwa na kukuacha upete huo ni ujinga wako
Kwa hivyo taasisi za dini zilijenga shule na mahospitali kwa rushwa? Ujinga ni choice.
 
Wanajali utu wa mtu, watu hawabomolewi nyumba bila kufahamu watakwenda wapi. Hata kama walijenga kwa makosa wanajengewa nyumba hata kama ni chumba na sebule.
Ni kweli kabisa, ubepari uko sensitive na walipa kodi
 
Ni kweli kabisa, ubepari uko sensitive na walipa kodi
CCM inaumiza sana wanaowaita wanyonge na kiburi kime wazidi kwakua hawahitaji kura zao ili kubakia madarakani. Walichosahau ni kuwa nguvu ya umma inaweza kuwatoa madarakani.
 
CCM inaumiza sana wanaowaita wanyonge na kiburi kile waziri kwakua hawahitaji kura zao ili kubakia madarakani. Walichosahau ni kuwa nguvu ya umma inaweza kuwatoa madarakani.
Wananchi wakichefukwa hakuna wakuwazuia
 
Wananchi wakichefukwa hakuna wakuwazuia
Mitandao ya jamii imesaidia kuwaelimisha wananchi juu ya nguvu waliyonayo. Hawa viongozi wanalipwa pesa kutokana na kodi yenu hawawezi kuongea na nyinyi vile wanavyotaka.
 
Wanajali utu wa mtu, watu hawabomolewi nyumba bila kufahamu watakwenda wapi. Hata kama walijenga kwa makosa wanajengewa nyumba hata kama ni chumba na sebule.
Kwanza kwenye hizo nchi za kibepari hata hiyo ardhi utakayaojenga nyumba utaitoa wapi?

Wewe utabaki kuwa mpangaji kwenye nyumba za Landlords.

Bepari na Utu wapi na wapi?

Hao wanaiuza silaha kila siku ilimradi tu wapate pesa ndio wanaojali utu?

  • According to the Kenya Land Alliance, 20% of the population own more than 65% of productive land in Kenya
  • The Kenyatta Family leads the pack with over 500,000 acres of prime land across the country
  • The Moi and Kibaki families follow closely with thousands of hectares located in different parts of Kenya
  • Foreigners also own huge chunks of land in Laikipia county
Kuna vitu sometimes, mkizungumzia mnaishia kuchekesha tu.
 
Back
Top Bottom