MIXOLOGIST
JF-Expert Member
- Mar 1, 2016
- 14,311
- 36,056
Wasalaam wana JF
Katika tafakari zangu nimekua nijiuliza mambo mengi yanayohusu mustakabali wa taifa letu. Maranyingi ustawi wa taifa letu una kwenda mbele na kurudi nyuma kila baada ya awamu moja kwenda nyingine. Atakuja kiongozi mzuri atajenga uchumi anayefuata anabomoa.
Hali kadhalika, taifa halina consistency kwenye ajenda za kiuchumi kutoka awamu moja kwenda nyingine . Tuko kama tumechanganyikiwa vile. Taifa linaongoza kwa matamko na slogan za kisiasa na za kiuchumi zisizotekelezeka.
Mfano: Siasa ni kilimo, kilimo ni uti wa mgongo, kilimo kwanza, hari mpya kasi mpya, hapa kazi tu, na kazi iendelee. Tangu tupate uhuru matamko yamekua mengi sana, yanachosha na kuchefua.
Kwanini tunapiga hatua mbili mbele na kurudi tano nyuma? Jibu ni kwamba tulidhulumu. Tulianzisha mfumo wa ujamaa na kujitegemea, tukatoa azimio la Arusha, ambalo lilifanikisha dhuluma na unyang'anyi. Watu waliofanya kazi kwa bidii na kupata mali kihalali walinyang'anywa na kuitwa wahujumu uchumi.
Taasisi za dini ziliporwa hospitali na shule na wageni waliporwa mali na biashara zao. Kwa upofu wa fikra tulitaka kuleta usawa baina ya wavivu na wawajibikaji, wabunifu na wababaishaji, waliobarkiwa na waliochanganyikiwa. Kwa upofu huo, taifa likawa jambazi, likapora mali za watu.
Baadhi ya watu walipoteza maisha na wako mbele ya kiti cha enzi wakimlalamikia Mungu kuhusu taifa hili nyang'anyi. Watu hao wameacha wajane/wagane na yatima ambao wameishi maisha ya dhiki na manung'uniko.
Katika kusoma kwangu maandiko nimeona sehemu nyingi ambapo Mungu ametoa adhabu na laana kwa watu wanaodhulumu, laana inayopitiliza maisha ya mlaaniwa na kwenda mpaka kwa vizazi vyake. Maneno ya Mungu yanaishi na yanatolewa ushuhuda huu. Kama taifa, inatupasa tujitafakari na kuchukua hatua stahiki ili tuweze kusonga mbele.
Nawasilisha.