Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 22,269
- 58,563
Wakuu !
Wasalaam wote nawasalimu kwa jina la Jamiiforums mahali ambapo tunathubutu kuzungumza kwa uwazi mitazamo na mawazo yetu.
Shukrani zimwendee Kaka Maxence Melo kwa kutuleta hapa pamoja, watu wenye mawazo, hoja, fikra na maono tofauti.
Nimelazimika kuanzisha huu uzi kwa lengo la kuyasema ninayoyaona mimi Mtanzania wa kawaida na mwenye thamani kubwa mbele za Mungu.
Kama kichwa cha huu uzi kinavyojieleza Taifa letu linaendekeza masihara kwa faida ya nani?
Aliwahi kusema Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Mh. George Simbachawene kwamba takribani asilimia 40 ya Watumishi wa umma ni mizigo.
SERIKALI imesema takriban asilimia 40 ya watumishi wa umma hawafanyia kazi kutokana na miongoni mwao kuwa wavivu, wazembe, wagonjwa na wale ambao viongozi katika taasisi zao hawataki wafanye kazi bali wamekaa tu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, aliyasema hayo jana jijini hapa, wakati akifunga Kikao Kazi cha Tano cha siku yatu cha Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA).
Simbachawene alisema kila aliyeajiriwa serikalini amepewa majukumu ya kufanya kazi lakini utafiti uliofanywa na Tume ya Utumishi wa Umma umebainisha nguvu kazi hiyo haitumiki sawasawa.
“Utafiti umeeleza na kuangalia sababu na serikali kupata hasara. Kwa sababu mtu anapokuja katika taasisi yako analipwa mshahara na serikali, hivyo kazi yako ni kuhakikisha kila kunapokucha kila mtumishi wa umma anafanya kazi.
“Ziko taasisi na baadhi ya watumishi ambao ni wavivu. Ukiwachukua wavivu na wale wagonjwa tayari ni karibu asilimia 25 hadi 30 ya nguvu kazi haifanyi kazi kwa siku. Wako ambao wanafika katika taasisi zetu na ninyi hamuwapi kazi kwa sababu mnajiuliza na kujihoji ‘amekujaje huyu, kaletwa na nani.
“Kama ana CV (wasifu) nzito ndiyo kabisa analeta tishio katika taasisi anawekwa benchi hafanyi kazi, ‘eti huyu tutamkomesha mpaka atakapoondoka mwenyewe’,” alisema.
Zaidi Soma https://www.ippmedia.com/nipashe/ha...mishi-wa-serikali-ni-mizigo-2025-02-14-122256
Ukisoma kwa makini hiyo taarifa ya Waziri unaona kuna matatizo mengi sana kwenye utendaji wa taasisi za umma. Na Waziri mwenye mamlaka na yeye analalamika tu pasipo kuwa na majibu au suluhisho la hili jambo.
Je Wakuu mnaweza kujua au kugundua tatizo liko wapi au ni nini kinachopelekea mpaka Waziri kulalamikia hii hali?
Kuna mambo ambayo huwa yanafanyika katika taasisi za umma kama anavyolalamika Mh. Waziri pasipo kujua nini chanzo cha haya matatizo na kwanini ufanisi wa taasisi za umma upo chini kila sehemu.
Kwa mawazo yangu na fikra zangu kama kichwa cha huu uzi kinavyojieleza tatizo lipo katika mfumo wa upatikanaji wa viongozi wa kuiongoza hii Nchi kwa sababu zifuatazo....
1. Wananchi hawathaminiwi hasa unapofikia wakati wa kuwachagua wawakilishi wao majimboni, kwenye kata hata kwenye serikali ya Mtaa.
Kwa muktadha huu kama Wananchi walimchagua Athumani wa Chama fulani kuwa mwakilishi wao lakini Serikali kupitia Tume ya Uchaguzi wao wanampiga chini na kumpa Saidi wa Chama kingine hapo ndipo tatizo linapoanzia. Kwa sababu huyo mwakilishi aliyekuwa chaguo la Wananchi kupitia chama kisichokuwa pendekezo kutoka juu anapowekwa pembeni na kuwekwa mwakilishi asiyekuwa chaguo la nchi hapo ndipo tatizo huwa linapoanzia na sijui kama wanalifahamu hili au Wameamua kulifunika tu ?
Nimeandika kwamba wananchi hawathaminiwi hasa kwenye upatikanaji wa wawakilishi wao kwa sababu hali halisi ya mambo inaonekana na ukweli wa mambo umedhihirika kuanzia mwaka 2019 na kuendelea mpaka sasa. Mwakilishi chaguo la wananchi anapowekwa pembeni na kuwekwa mwingine kwa mapendekezo au maagizo maalumu unaleta shida sana kwa sababu mwakilishi huyo baadaye huenda akachaguliwa akawa Waziri anayesimamia sera za wizara fulani. Kwa sababu hakuwa chaguo la wananchi hapo ndipo malalamiko kama ya Waziri Mh. Simbachawene lazima yatokee.
Mjadala wa hili suala naomba mchangie kwenye michango mtakayotoa ili tuweze kuisaidia serikali yetu iache janja janja iruhusu na iwape wananchi haki ya Kumchagua mwakilishi ambaye anatokana na maamuzi yao sio kulazimisha yule ambaye anapendekezwa na mfumo.
Shida, tabu na aibu anayeipata na kiongozi wa nchi kwa sababu ya kukosea katika mifumo ya upatikanaji wa mwakilishi wa wananhi. Na kwa mazingira tuliyo nayo kuanzia mwaka 2019 mpaka sasa hata Watendaji wa taasisi za Umma wanafanya vile wanavyotaka kwa sababu hata viongozi wanaowasimamia hasa wizara mbalimbali walivyopatikana sio kwa njia ya haki.
Binafsi nimeyaona na nimeyashuhudia kwa macho yangu na Mimi nimekuwa mhanga wa hili jambo.
Wito wangu kwa serikali izingatie sana hili jambo lasivyo wasipolizangatia na kulichukulia kwa uzito basi matokeo yake sio mazuri huko mbele ya safari.
Hata kama kuna maoni ya Vyama vya upinzani ni muhimu kuyachukua na kuyachambua na kuweza kuyafanyia kazi. Kuwa mpinzani wa itikadi sio uadui ila ndio chachu cha maendeleo.
Mjadala ni mrefu sana nitaendelea kuuleta kwa kadri vile itakavyokuwa nakuwa na wasaa wa kufanya hivyo.