Taifa letu linaendekeza masihara kwa faida ya nani?

Taifa letu linaendekeza masihara kwa faida ya nani?

Kwanza kabisa Waziri Simbachawene naye ni tatizo, ajirekebishe kwanza ndipo atoe lawama upande wa pili.

Wizara yake wameshindwa kuweka misingi imara kwa watumishi wa Umma ili waonekane weak then wayumbishwe na kunyanyasika.

1. Je, wamefanya tafiti wakatambua kuwa kuna taasisi wameajiri mtumishi hana kiti na meza ya kufanyia kazi? Hana computer wala ofisi haina simu ya ofisini? Mtumishi anatumia Computer na simu yake huku wakipokezana meza na kitu na mtumishi mwingine? Huku majukumu akipatiwa na kejeli juu kama atachelewa kumaliza kazi.

2. Ofisi hawafanyi matengenezo ya viyoyozi, taa, fan, milango, madirisha, paa huku pesa za viongozi kula zipo za kutosha. Mazingira kama hayo mtumishi wa chini atafanya kazi gani? Yaani ofisini inakuwa sehemu ya mateso.

3. UTUMISHI wenyewe wameanzisha portal inayoitwa ess kwa ajili ya kurahisisha na kupunguza changamoto za watumishi wa umma; yaani mtumishi anashida ya kuhamia sehemu anaona atafanya kazi comfortable akiwa karibu na Familia yake lakini bado mfumo haina majibu ya maombi yake takribani mwaka mzima...wakati mwingine analazimika kutoka Bukoba kwenda Dodoma kuwakumbushia suala la kwenye mfumo.

4. Waziri wa Watumishi ndiye tatizo; wakati mwingine anaongea maneno yenye karaa sana anawaambia wakuu wa taasisi wa wasikae na malalamiko ya watumishi kwa zaidi mwezi then yeye ofisi yake inakaa na taarifa ya malalamiko ya watumishi zaidi ya mwaka.

Kama Wizara yako hawako tayari kujirekebisha basi kaa kimya usiwapigie wengine kelele ya kujirekebisha.
 
Back
Top Bottom