Taifa lina haki ya kujua Makamu wa Rais mstaafu yuko wapi, kama amepotea atafutwe

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
17,047
Reaction score
63,206
Mnaweza kudhani kuwa kutoonekana kwa makamu wa rais mstaafu ni jambo dogo mbele ya wananchi. Hili siyo jambo dogo hata kidogo. Kutoonekana kwake hadharani kunawafanya wananchi wajiulize maswali mengi sana, miongoni mwa maswali hayo ni,
1. Je yuko hai au amekufa?
2. Je nchi hii iko salama kiasi gani kama makamu wa rais anaweza kutoonekana takriban mwezi mzima na serikali isiseme lolote juu yake.

Ukiachilia mbali hayo, hii inazidisha chuki ya wananchi kwa serikali kwa sababu inaonekana kama ni serikali fulani ya kibandidu au ya kimafia hivi!. Kama makamu wa rais anafanywa hivi je wananchi wa kawaida watafanywaje?
 
CcM wanafiki sana, wako kimyaaa
 
ok.🐒
 
Sio mtumishi wa umma, yupo zake mapumziko na maisha yake binafsi..... unataka aendelee kuripoti kwako?
Mtu aliyekua analishwa ,kuvalishaa na kila kitu anafanyiwa Bure na Kodi za watanzania hawezi kuondoka kihuni namna hiyo halafu watu wakaa kimya

Hujiulizi kwann Dr Mpango hauliziwi
 
The Nyang'aus don't care.
 
Mtu aliyekua analishwa ,kuvalishaa na kila kitu anafanyiwa Bure na Kodi za watanzania hawezi kuondoka kihuni namna hiyo halafu watu wakaa kimya

Hujiulizi kwann Dr Mpango hauliziwi
Halafu watu wakisema ameuwawa wanasema wanaleta taharuki, hili ombwe la taarifa ya alipo Nchimbi ndiyo linakaribisha kila aina ya uvumi na tetesi.
 
Barua yake ya kujiuzulu ilikuwa very clear - amestaafu siasa na utumishi wa umma.

Hii maana yake ni kwamba amechagua PRIVATE LIFE. Mwacheni former VP aishi maisha anayoyapenda asisumbuliwe.
 
Ingawa hata ex VP ni mwananchi wa kawaida ila hii hali ya watu kupotea na hakuna juhudi za dhahiri za kumtafuta linaleta kichefuchefu kwa Taifa letu.Yawezekanaje mtu kupotea kama kifaranga cha Bata?
Maisha yamekosa thamani kwa kiwango cha kutisha na haileti maana halisi.
 
Kiongozi anapoteaje kwenye nchi yenye majeshi na amri jeshi mkuu yupo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…