Taifa lina haki ya kujua Makamu wa Rais mstaafu yuko wapi, kama amepotea atafutwe

Taifa lina haki ya kujua Makamu wa Rais mstaafu yuko wapi, kama amepotea atafutwe

Kuna watu wananufaika na huo usenge wa kupoteza watu ,Ila kuna muda unakuja kibao kitageuka na wataonja dhulma hii pia
 
Mnaweza kudhani kuwa kutoonekana kwa makamu wa rais mstaafu ni jambo dogo mbele ya wananchi. Hili siyo jambo dogo hata kidogo. Kutoonekana kwake hadharani kunawafanya wananchi wajiulize maswali mengi sana, miongoni mwa maswali hayo ni,
1. Je yuko hai au amekufa?
2. Je nchi hii iko salama kiasi gani kama makamu wa rais anaweza kutoonekana takriban mwezi mzima na serikali isiseme lolote juu yake.

Ukiachilia mbali hayo, hii inazidisha chuki ya wananchi kwa serikali kwa sababu inaonekana kama ni serikali fulani ya kibandidu au ya kimafia hivi!. Kama makamu wa rais anafanywa hivi je wananchi wa kawaida watafanywaje?
Wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki ndiyo wakulaumiwa. Walitakiwa wawe wa kwanza kusema chochote kama mambo hayako sawa. Ila bado naunga mkono hoja yako, hata sisi wananchi tunatakiwa tuhoji kwa sababu alikuwa ni kiongozi wa umma.
 
Kuna watu wananufaika na huo usenge wa kupoteza watu ,Ila kuna muda unakuja kibao kitageuka na wataonja dhulma hii pia
Walishaonja wengi tu lakini inaonekana hawajifunzi. Pengine hii siyo njia nzuri ya kumfunza mtu aliye kwenye ulaji.
 
Sio mtumishi wa umma, yupo zake mapumziko na maisha yake binafsi..... unataka aendelee kuripoti kwako?
Ilishawahi kutokea 1984 wakati aliyekua Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Rais wa Zanzibar Aboud Jumbe Mwinyi alipoitwa Dodoma na kulazimishwa kujiuzulu vyeo vyake vyote.

Wakati anataka kupanda ndege kurudi Zanzibar "akaombwa" na Rais Nyerere ambaye pia alikua Mwenyekiti wa CCM (CCM ilikua ina miaka 7 tangia izaliwe 1977) Mwalimu Nyerere apitie kwanza Dar es Salaam na alipopanda ndege na kushuka Dar akajikuta anaelekezwa pa kwenda ambapo akapelekwa nyumbani kwake Mjimwema Kigamboni

Alipotaka kuwapigia simu watoto wake akakuta simu imekua disconnected (wakati huo simu za mezani). Na hakua na namna nyingine ya mawasiliano na familia yake. Hakuruhusiwa kutoka nje ya uzio wa nyumba yake

Mzee Jumbe mwenyewe anasema katika maandishi rasmi yaliopo kwenye kitabu chake na vitabu vingine kadhaa kwamba alipo ona hali hiyo akamshukuru na kukabidhi hatma yake kwa Mungu akijua chochote kinaweza kutokea kwake wakati wowote

Mzee aliishi katika kizuizi cha nyumbani muda mrefu hadi mwisho wa kipindi cha pili cha utawala wa Mzee Mwinyi ambapo angalau alipewa uhuru wake na sasa akawa anajishughulisha na mambo ya dini na uandishi wa historia

Ila alikua na masikitiko, hasira na uchungu mwingi kwa watu wawili. Wa kwanza ni aliyekua msaidizi wake wa karibu Maalim Seif Sharif Hamad na wa pili ni Mwalimu Nyerere

Mzee Aboud Jumbe Mwinyi hakuridhishwa na muundo wa muungano kama ulivyo na alichokiita "ubabe" wa serikali ya muungano kutaka kumeza mamlaka ya Zanzibar

Kwa upande mwingine ilikua ni dhambi isiyosameheka kwa Mwalimu Nyerere kuhoji uhalali au muundo wa muungano labda iwe ni mjadala wa kuelekea serikali moja na si vinginevyo.

Aidha Mzee Jumbe alihisi ameuzwa na Maalim Seif hadi kupelekea kudhalilishwa kwake kwa kuvuliwa madaraka yake yote na kuwa sio tu mwananchi wa kawaida bali kuwekwa kizuizini

Mzee Jumbe alishuhudia Maalim Seif akifukuzwa CCM. Na katika uchaguzi wa mwanzo wa vyama vingi 1995 wakati Maalim Seif akigombea Urais wa Zanzibar huku sera ya chama chake ikiwa ni muungano wa serikali tatu Mzee Jumbe alikua akilaani kimyakimya kwa watu wake wa karibu kua duniani humu watu hawaaminiki hasa wanasiasa wana sura mbilimbili. Sijui mwenyewe alikua anakumbuka nini

Mzee Jumbe hakuwahi wala hakutaka kabisa kukutana na Maalm Seif hadi pale alipofiwa na mwanae miaka ya mwisho ya 1990s na Maalim alihudhuria msiba pale Mjimwema. Mzee Jumbe wakati huo alikua mtu mzima na macho yake yalishapoteza nuru hivyo alikua haoni

Watoto wake walimpeleka Maalim alipokaa Mzee Jumbe akampa mkono kisha ndio wakamtambulisha kwake kwamba huo mkono ni wa nani. Mzee Jumbe akaitikia salam na ile pole lakini kwa haraka zikampitia zile kumbukumbu za machungu ila sasa wakati mwingi umepita na yeye alishasamehe, wakasalimiana

Katika vitu ambavyo Maalim Seif hakuwahi kuvijibu kwa ufasaha ni hili suala la kumsaliti kwa Nyerere Mzee Jumbe(lakini haya ya mwisho ni maoni yangu mimi mwenyewe na naomba nisiendelee)

Yote yapo kwenye vitabu vinvyopatikana maduka makubwa ya vitabu. Tusomeni historia ya nchi yetu
 
Ina maana hata rafiki yake mzee warioba hajajitokeza tena kusema kama alimpata kwenye simu au bado haipatikani lakini nadhani familia yake wangeitisha press nadhani yupo ameamaua kujifungia
Warioba alisema kila akimpigia simu hapatikani na alitaka kwenda kwake kumuona akaonywa kuwa achague kati ya kuishi au kupotea.
 
Mnaweza kudhani kuwa kutoonekana kwa makamu wa rais mstaafu ni jambo dogo mbele ya wananchi. Hili siyo jambo dogo hata kidogo. Kutoonekana kwake hadharani kunawafanya wananchi wajiulize maswali mengi sana, miongoni mwa maswali hayo ni,
1. Je yuko hai au amekufa?
2. Je nchi hii iko salama kiasi gani kama makamu wa rais anaweza kutoonekana takriban mwezi mzima na serikali isiseme lolote juu yake.

Ukiachilia mbali hayo, hii inazidisha chuki ya wananchi kwa serikali kwa sababu inaonekana kama ni serikali fulani ya kibandidu au ya kimafia hivi!. Kama makamu wa rais anafanywa hivi je wananchi wa kawaida watafanywaje?
Atakuwa amedhibitiwa mahali.
 
Ina maana hata rafiki yake mzee warioba hajajitokeza tena kusema kama alimpata kwenye simu au bado haipatikani lakini nadhani familia yake wangeitisha press nadhani yupo ameamaua kujifungia
Basi kama ameamua kuwa hivyo maana yake ni kwamba hata yeye hajui nini maana ya mtu kuwa ni Public figure !
Kwahiyo ni kazi bure hata kumuongelea 😳 !
 
Back
Top Bottom